Na Is haka Mohamed Rubea, Pemba.
MCHANGO wa dini katika masuala mbali mbali ni muhimu katika kufanikisha lengo ya jambo lolote lile ambapo limepangwa kufanyika kwa mafanikio na kupelekea mageuzi.
Tumekuwa tukishughudia dini zikitumika kwenye masuala mengi ya kijamii, yale ya kitaifa na wakati mwengine hata suala la mtu binafsi.
Mtanzamaji katika Makala hii tunaangalia mchango wa dini katika kuimarisha usawa wa kijinsia hapa Zanzibar, hususani kisiwani Pemba.
Inatambulika kuwa kuna miongozo mbali mbali ya kidini juu ya usawa wa kijinsia na nafasi ya kila jinsia ukiondosha ule utofauti wa kimaumbile, na miongozo itokanayo na mafundisho kama mirathi kwa uislamu hata dini nyengine,
Hapa nchini Tanzania tumeshughudia nguvu hizo za kiimani zikitomika katika kutafuta njia bora ya kuliweka jambo mahala pake, ikikumbukwa kuwa dini ni zenye wafuasi na waumini ambao wanazifuata na miongozo yake.
Masalan ni pale panapotokea suala la ugonjwa kwenye jamii dini hutumiwa hata na mamlaka kuweza kuhamasisha jamii juu ya kutoa uelewa wa kujikinga na kukinga wengine na magojwa ili yasiweze kutambaa zaidi.
Lakini inaonekana bado mchango wa dini haujakuwa mkubwa sana katika kuona usawa wa kijinsia unaimarika kwa kiasikile kilichotarajiwa.
Taasisi za Pemba Community Forest, Internation Community Forest na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Zanzibar Tamwa kupitia Mradi wa Wanawake na Uongozi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kuunga mkono wanawake katika kilimo msitu.
Kwa upande wa dini kiislamu mwanamke ana hadhi na cheo kikubwa kilicho taadhimu ambapo mwanamke wa Kiislamu ni mwalimu wa kwanza katika kujenga jamii.
Siri ya umuhimu wa mwanamke imetanda katika kazi yake nzito na mamlaka yaliyokwa juu yake, shida shida ambazo anabeba mabegani mwake, mamlaka na dhiki ambazo hata mwanamme hawezi kuzibeba nan do maana tukaambiwa tuwapende na kuwaheshimu sana mama zote.
“Tumemuusia insanikwa wazazi wake wawili, mama yake amebeba mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu na kumwachisha ziwa katika miaka katika miaka miwiliya kwamba unishukuru mimi, na wazazi wake, kwangu ndio pahali pa kuishia’ (Lukman: 14)
Tukiangalia Biblia, Mwanzi 1:27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, Kwa mafano wa Mungu alimwumba mwanamke na mwanamke aliwaumba,sikiliza pahali popote pale mwanamke ni mtu mwenye nguvu na ushawishi mkubwa katika kufanya jambo kuliko hata mwanamme, Ikiwa ushawishi huu utatumiwa kwa mpango wa Mungu basi kusudi litatekelezwa.
Miongozo ya dini imeweka wazi kuwa mwanamke anayo nafasi kubwa katika jamii kufanya mambo mengi na yaliyo makubwa, lakini inaoneka wazi kuwa bado miongozo ya dini haitapewa nafasi yake kisawa sawa kwa mwanamke.
Ufafanuzi kwa mtindo wa kihabari
Miongozo ya dini, Imeeleza wazi kuwa mwanamke ni mshiriki muhimu katika ujenzi wa familia na jamii. Ana haki ya kushiriki katika elimu, biashara, na hata uongozi wa kijamii.
Changamoto ya utekelezaji, Pamoja na maandiko na mafundisho ya dini kuhimiza usawa, bado kuna tafsiri finyu na mitazamo ya kijamii inayomnyima mwanamke nafasi ya kuonyesha uwezo wake.
Matokeo ya kijamii,Mwanamke anapopewa nafasi yake ipasavyo, jamii hunufaika kwa kupata nguvu kazi yenye ufanisi, mawazo mapya na uongozi wa kiadilifu. Kinyume chake, kumnyima nafasi ni kuikosesha jamii mchango muhimu.
Wito wa mabadiliko, Wataalamu wa dini na viongozi wa kijamii wanahimizwa kusoma upya miongozo ya dini kwa mtazamo wa kina na wa kisasa, ili kuhakikisha mwanamke anapata nafasi yake sawasawa kama ilivyoelekezwa.
WANAWAKE WASEMAJE.
Miongozo ya dini tunashindwa kuielewa ndio mana tunakosa haki zetu,natamanai wadau waendelee kuelimisha jamii hususan ni kisiwani Pemba ,huku vijijini ndio uozo umezidi haki nyingi tunazikosa.Alisema Fatma Hamad ali mkaazi wa Kambini kichokochwe ambae pia ni mkulima wa kilimo mseto
Hitimisho
suala hili ni habari yenye uzito wa kijamii, dini imetoa mwongozo wa wazi, lakini utekelezaji wake bado unakwamishwa na mitazamo ya kijamii. Mwanamke anapewa nafasi kubwa kwa maandiko, lakini kwa vitendo nafasi hiyo mara nyingi hubaki kufungwa na mila na tafsiri zisizo sahihi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni