WANAWAKE wamekuwa nguzo muhimu katika jamii kwa karne nyingi. Kauli kwamba “Wajibu wa wanawake unatambuliwa kuwa muhimu katika kazi za jamii na maendeleo ya kijamii zinaendelea kusikika hata kwa viongozi wa juu wa nchi na inabeba uzito mkubwa, kwani inatambua mchango wa wanawake si tu katika familia bali pia katika nyanja za kijamii, kiuchumi uongozi na kisiasa.
Katika makala hii, tutachambua wajibu wa wanawake kwa kina, tukitoa mifano hai kutoka Tanzania na ulimwengu kwa ujumla, ili kuonyesha namna mchango wao unavyoendeleza jamii na kuchochea maendeleo endelevu.
MIFANO YA KUIGWA NA JAMII.
Tukianza wajibu wa Wanawake kama Msingi wa Familia,Familia ni kitovu cha jamii, na mara nyingi wanawake ndio wanaobeba jukumu la kuhakikisha familia inakuwa na malezi bora.
Malezi ya watoto, Mwanamke ndiye mwalimu wa kwanza wa mtoto, Kupitia malezi yake, mtoto hujifunza maadili, lugha na utamaduni.
Vijiji vya Pemba na Tanzania kwa ujumla, mama hutumia muda mwingi kuwafundisha watoto wake kusoma Qur’an, kuimba nyimbo za kitamaduni, na kuwafundisha stadi za maisha kama kupika na kushona,kulima kulinda mila na tamaduni ,ikiwa kama sehemu ya urithi wa kijamii unaoendelezwa kizazi hadi kizazi.
Mchango wa Wanawake katika Elimu
Elimu ni nguzo ya maendeleo ya kijamii. Wanawake wanapopewa nafasi ya kusoma, jamii nzima hunufaika kwani mara nyingi huonekana kama wategemezi,hivyo wanapoapta furs ya elimu husaidia Kupunguza ujinga,Wanawake waliosoma huweza kufundisha watoto wao na kuhimiza familia nzima kuthamini elimu na mabadiliko hupatikana katika jamii nzima,Kama ambavyo Malala Yousafzai kutoka Pakistan alivyosimama kidete kupigania haki ya wasichana kupata elimu. na Harakati zake zimekuwa mfano wa kimataifa kwamba mwanamke mmoja anaweza kuleta mabadiliko makubwa.
Wanawake katika Uchumi
Wanawake wanashiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi, kuanzia kilimo, biashara ndogo ndogo, hadi uongozi wa jamii na mashirika makubwa.
Katika kilimo Wanawake wengi vijijini ndio wanaolima mashamba ya chakula, ambayo inahakikisha familia na taifa linapata chakula cha kutosha ukilinganisha na wanaume.
MIFANO
Katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha,ndani ya hiiTanzania wanawake wamekuwa mstari wa mbele katika kilimo cha kahawa , huku Biashara ndogo ndogo, zikiongozwa na Wanawake mijini huendesha biashara za sokoni, kuuza matunda, nguo na bidhaa mbalimbali,ambapo bila shaka mwanamke ni zaidi ya injini ya uchumi wa kila siku.
Wanawake katika Afya na Huduma za Jamii , Wanawake pia ni wahudumu wakuu wa afya na ustawi wa jamii.
Wauguzi na wakunga,Wanawake wengi hufanya kazi kama wauguzi na wakunga, wakihakikisha mama na mtoto wanapata huduma bora,mfano hai Katika hospitali za vijijini Tanzania, wakunga wanawake ndio wanaosaidia akina mama kujifungua salama,Bila wao, vifo vya uzazi vingekuwa vingi zaidi.
Upande wa Huduma za kijamii,Wanawake hushiriki katika vikundi vya kijamii kama vikoba, ambavyo husaidia familia kupata mikopo midogo na kujiendeleza kiuchumi.
Wanawake katika Uongozi na Siasa
Wanawake wanaposhiriki katika uongozi, maamuzi yanakuwa jumuishi na yenye kuzingatia mahitaji ya jamii
Ellen Johnson Sirleaf, Rais wa zamani wa Liberia, alionyesha dunia kwamba mwanamke anaweza kuongoza taifa na kuliletea amani baada ya vita.
Wakati Tanzania,Rais Samia Suluhu Hassan nae ni kielelezo cha mchango wa wanawake katika siasa, Uongozi wake umeweka Tanzania katika ramani ya kimataifa na kuonyesha kuwa wanawake wana uwezo wa kusimamia maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Jee Wanawake na Kulinda Utamaduni
Wanawake ni walinzi wa utamaduni na mila katika jamii ,watekelezaji wa mila na warithisha mila hizo kwa kwa upamde wa hapa kisiwani Pemba, wanawake hushiriki katika utengenezaji wa mikeka na vikapu vya mkonge,ngoma za kimila ,ususi,ushoni Hii si tu sanaa bali pia ni chanzo cha kipato na utambulisho wa jamii.
CHANGAMOTO KWA WANAWAKE
Changamoto Wanazokabiliana Nazo
Licha ya mchango wao mkubwa,walionao katika harakati zote zinazohusu maendeleo ndani ya jamii lakini bado w wanawake hukumbana na changamoto nyingi ikiwemo
Ubaguzi wa kijinsia, Wanawake mara nyingi hupunguzwa nafasi katika uongozi na ajira Kama hapa anavyosimulia Hadia Faki Mkaazi wa Kiuyu minungwini ,mwabamke mjasiriamali biashara ndogo ndogo,Mkulima wa kilimo mseto mke na mama wa watoto 8 .
"Najishughulisha na shughuli mbali mbali kilimo na biashara ndogo ndogo za ushoni wa mikoba,makawa, ladu,mafuta ya mwani singo ,lakini pia ni mkulima na mnufaika wa Zanz adapt program na nendelea na kilimo msitu"
Nimegombea lakini sijui imekuaje mpaka nimeshindwa kuingia hata katika hatua za mapema nimekosa fursa ,bado jamii haioni umuhimu wa sisi kutushirikisha hata tukizitafuta fursa "
"Ukosefu wa mitaji, kazi yangu ninayoitegemea kupata kipato ni kilimo na hapa kwetu Wanawake wengi hawana uwezo wa kupata mikopo ya kifedha kwa ajili ya biashara licha ya kuwa mstari wa mbele katika kila jambo la maendeleo lakini zinapokuja fursa kama hizo tunasahauliwa.
SULUHISHO
Elimu kwa wote,Uwezeshaji kiuchumi,Sheria na sera, Serikali kuweka sera zinazolinda haki za wanawake dhidi ya ubaguzi na unyanyasaji.
Kwani wanawake wanapopata fursa wanafanya vizuri mfano ni Programu za kukopa na kuweka vikoba na SACCOS ambazo kwa asilimia kubwa zinaendeshwa na wanawake zimekuwa zikiwasaidia kujiendeleza kiuchumi na kijamii.
Kauli kwamba “Wajibu wa wanawake unatambuliwa kuwa muhimu katika kazi za jamii na maendeleo ya kijamii” si maneno matupu bali ni ukweli unaojidhihirisha kila siku.
Wanawake ni walimu, wakulima, viongozi, wahudumu wa afya, na walinzi wa utamaduni na mazingira Bila mchango wao, jamii isingeweza kusonga mbele. Ni wajibu wa kila mtu kuhakikisha wanawake wanapewa nafasi sawa na wanaume ili kuendeleza jamii na kufanikisha maendeleo endelevu,kama ambavyo mradi wa Zanzibar women leadership climate change and adaptation ZANZ ADAPT unaotekelezwa na Community Forest Pemba CFP ,CFI NA TAMWA ZANZIBAR ulivyokuja kuwakomboa wanawake kutimiza malengo yao ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi kushiriki katika uongozi pamoja na kuwakomboa kiuchumi.
MWISHO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni