Na,Is haka Mohamed Rubea .
KATIKA jamii nyingi Tanzania , dini imekuwa na nafasi kubwa katika kuunda maadili, mila na desturi.
Huku mafundisho ya kidini mara nyingi yakiendelea kutumika kama mwongozo wa maisha ya kila siku, na huathiri namna watu wanavyohusiana, kushirikiana na kugawana rasilimali.
Hata hivyo, changamoto kubwa imekuwa jinsi mafundisho haya yanavyoweza kuendana na dhana ya kisasa ya usawa wa kijinsia, hasa katika mila na desturi za kijamii, pamoja na udhibiti wa rasilimali.
Mafundisho ya Kidini ndio hutoa miongozo na Maadili ya Jamii ,Dini nyingi, ikiwemo Uislamu, , hufundisha kuhusu haki, heshima na mshikamano wa kijamii,Mafundisho haya mara nyingi yanasisitiza umuhimu wa upendo, mshikamano na usawa mbele ya Mungu.
Hata hivyo, tafsiri za mafundisho ya kidini hutofautiana kulingana na jamii na wakati, na mara nyingine hutumika kuhalalisha mfumo wa kijamii unaoweka jinsia moja juu ya nyingine.
Mafundisho hayo y a dini na husaidia usawa wa kijinsia katika mila na desturi za kijamii, pamoja na udhibiti wa rasilimali.”
Usawa wa Kijinsia katika Mila na Desturi,Mila na desturi za kijamii mara nyingi huakisi historia na utamaduni wa jamii husika.
Katika baadhi ya jamii, wanawake wamekuwa wakipewa nafasi ndogo katika maamuzi ya kifamilia na kijamii.
Hali hii imekuwa ikipingwa na harakati za kijamii na kisiasa zinazosisitiza usawa wa kijinsia, ambapo wanawake na wanaume wanapaswa kushiriki kwa usawa katika maamuzi na fursa za maisha.
Amina Ahmed Mohd ni Kaimu mratibu Chama cha waandishi wa habari wanawake TANZANIA ,TAMWA ZANZIBAR,ambayo ni miongoni mwa taasisi isyoya kiserikali inayoendelea kutetea na kusimamia haki za wanawake ili kufikia usawa wa kijinsia yey anasema kuwa ‘’ mila desturi na tamaduni zilizojengeka katika baadhi ya maeneo ndani ya jamii ,yamekuwa sababu ya kurudisha nyuma harakati hizo za kufikia usawa wa kijinsia hususan katika maswala ya umiliki wa rasilimali ikiwemo ardhi
‘’ Bado kuna changamoto kubwa Katika jamii kuhusu maswala ya umiliki wa rasilimali na usawa wa kijinsia ,ikiwemo ardhi kwa wanawake kwa usawa , huku wengine wakiona suala hilo ni kwamujibu wa dini jambo ambalo dini limeweka miongozo na maelekzo ya kufuata iwapo ’’
‘’Katika hili sisi kama taasisi tunaendelea kutoa elimu kupitia vyombo vya habari ili jamii izidi kuelimika na kuweza kuufikia usawa wa kijinsia katika kumiliki rasilimali’’alimaliza
MIONGOZO YA DINI
Mafundisho ya kidini, yanapotafsiriwa kwa mtazamo wa haki na usawa, yanaweza kuwa chachu ya kuondoa Kutokuwepo kwa usawa wa kijinsia na kuimarisha mshikamano wa kijami,kwa mitazamo
Katika Qur’an, Mwenyezi Mungu anasema katika Sura An-Nisai (4:32) Mwenyezimungu anasema,“Wanaume watapata sehemu ya walichokichuma, na wanawake watapata sehemu ya walichokichuma”.
Aya hii inaweka msingi wa kisheria wa kidini kwamba kila mtu ana haki ya kumiliki mali bila ubaguzi wa kijinsia .
Huku miongozo hiyo hiyo ya dini kwa upande wa dini ya kikiristo katika Biblia (Mithali 31:16), mwanamke jasiri anatajwa kuwa “hununua shamba kwa matunda ya kazi yake,” ikionesha wazi kuwa umiliki wa ardhi ni haki halali ya wanawake wa dini ya Kikristo.
WANAWAKE
Bikombo Faki Khamis ,ni mama wa watoto 8 Mkaazi wa Kiuyu minungwini wilaya ya wete Mkoa wa kaskazini Pemba ,mkulima alibadili mfumo na utaratibu wake wa kulima kilimo cha mazoea na kuanza kulima kilimo kinachoendana na hali ya hewa na kinachohimili mabadiliko ya tabia ya nchi ,akiwa moja kati ya wanufaika wa mradi wa ZANZ ADAPT unaotekelezwa na Jumuia ya uhufadhi wa misitu Pemba CFP,jumuia ya uhifadhi wa mistu kimataifa CFI ,NA chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania Zanzibar TAMWA KWA UFADHILI WA CANADA GLOBAL AFFAIR katika suala hili la usawa wa kijinsia katika suala hili la usawa wa kijinsia na udhibiti wa rasilimali anaeleza kuwa
‘’ Mwazoni nilipoanza kulima kilimo hichi ambacho ni mchanganyiko ,mume wangu aliniambia sina kazi kiufupi alinibeza ,lakini kwa sasa nashukuru ananisaidia tunafanya kazi hii kwa pamoja pale ambapo nakwama katika kilimo ananisaidia ’’.
Natumia kilimo hicho katika ardhi yao ya familia lakini yeye anaisimamia kuhakikisha Napata haki yangu juu ya nguvu zangu zote ninazoendlea kutumia, alinifyekea yey pori na mengine mengi anakubali nimshirikishe kila hatua kwangu ni mafanikio kwa vile awali alikuwa hana utayari’’
Katika jamii pia mashirikiano Napata ,na mumewangu ananiunga mkono Zaidi ,niligombea udiwani wa wadi yangu ,ingawa sikubahatika kuingia katika mchakato lakini alionesha mashirikiano makubwa na kunisapoti,Kwenye biashara pia tunasaidiana’’ alimaliza Bikombo
Fatma Shaaban ni mnufaika mwengine mradi wa Zanz ADAPT anasema kuwa Udhibiti wa Rasilimali, Rasilimali ni pamoja na ardhi, mali, elimu na hata nafasi za uongozi,kwakwe umekuwa na msaada mkubwa kutoka kwa mume wake ambae amekuwa mshauri, msaidizi na msimamizi wa maendeleo yake katika kilimo anachoendelea kulima huku akiamini kuwa rasilimali zinazozalishwa katika shamba hilo ni faida yake na watoto wake hapo baadae.
Katika jamii nyingi, udhibiti wa rasilimali umekuwa ukiegemea zaidi kwa wanaume, huku wanawake wakiachwa nyuma.
Hali hii imekuwa ikisababisha pengo kubwa la kiuchumi na kijamii kati ya wanaume na wanawake.
Mafundisho ya kidini yanaposisitiza haki na usawa, yanaweza kutumika kama msingi wa kugawanya rasilimali kwa njia ya haki, bila kujali jinsia kama hapa MR Robert Migue Kiongozi wa dini ya kikiristo lakini pia mwanaharakati maswala ya wanawake kutoka vitongoji anavyosema
‘’Usawa wa kijinsia katika umiliki wa rasilimali ni suala ambalo limewekewa mipaka yake kisheria ni vyema ikafuatwa ili kuona hatuwaachi nyuma wanawake ‘’
Wapo baadhi ya viongozi wamekuwa wakipotosha bila kufafanua ipasavyo wakiona kuwa wanaona usawa wa kijinsia kama tishio kwa mila na desturi za jadi wakiacha kutoa miongozo ya dini na maelekezo yake yanavyosema .
WANAJAMII .
Uelewa mdogo wa jamii kuhusu tafsiri pana ya mafundisho ya kidini inayosisitiza haki na usawa,Bado baadhi ya watu katika jamii wanashindwa kutofautisha dini ,mila na desturi katika maswala haya ,tunaomba elimu izidi kutolewa ili mwisho wa siklu rasilimali za wanawake ziweze kumilikiwa na wao wenyewe alisema Riziki Khamis hamad kaazi wa Kiuyu .
Mfumo wa kisheria na kiutawala ambao mara nyingine haujengi mazingira ya usawa wa kijinsia katika udhibiti wa rasilimali,unapelekea kuwaona wanawake hususan ni huku vijijini waonekane kama hwastahiki kuwa na haki katika rasilimali ndio mana waliowengi wamezisabilia’’alisema Khamis Abass Khamis mkaazi wa minungwini.
MAONI
Katika baadhi ya nchi za Kiafrika, mafundisho ya kidini yametumika kuhamasisha elimu kwa wasichana, jambo ambalo limeongeza usawa wa kijinsia katika sekta ya elimu.
Mashirika ya kidini yamekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha wanawake kushiriki katika uongozi wa kijamii na kisiasa.
Jumuiya za kidini pia zimekuwa zikihamasisha mshikamano wa kijamii kwa kusisitiza kwamba rasilimali ni zawadi yakila mtu na zinapaswa kugawanywa kwa usawa.
Wadau maswala ya wanawake na usawa wa kijinsia wanaendelea kusiadia kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa usawa katika umiliki wa rasilimali na usawa wa kijinsia ndio njia pekee itakayosaidia kumkomboa mwanamke na aweze kuwa huru bila utegemezi.
Hitimisho Mafundisho ya kidini, yanapochukuliwa kwa mtazamo wa haki na usawa, yanaweza kuwa chachu ya mabadiliko makubwa katika jamii.
Kusaidia usawa wa kijinsia katika mila na desturi za kijamii, pamoja na udhibiti wa rasilimali, si tu suala la kisiasa au kijamii bali pia ni suala la kiimani. Jamii inayojengwa juu ya misingi ya usawa na haki ni jamii yenye mshikamano, maendeleo na amani.
MWISHO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni