WILAYA YA MKOANI. Tatizo la kutokuwepo kwa nyumba za walimu katika kisiwa cha Shamiani Mwambe Wilaya ya Mkoani kumepelekea kuwepo kwa utoro wa wanafunzi katika Skuli ya Kisiwa hicho.
Wakizungumza
na Waandishi wa Habari Wananchi wa Kisiwa hicho wamesema kuwa wawalimu ambao
wanatoka ng`ambo ya kisiwa hicho wamekuwa wakichelewa na wakati mwengine
kuondoka mapema jambo ambalo huwapa mwanya watoto kutoroka skuli.
Hata hivyo
baadhi ya wananchi wamewaelekezea lawama baadhi ya wananchi kwa kutowasimamia
watoto wao kwa kuwahimiza kwenda skuli ndiko kunakochangia kuongezeka kwa utoro
wa wanafnzi hao.
Wamesema
baadhi ya wazee wamekuwa radhi kuwaona watoto wao wakijishughulisha na kazi za
uvuvi, huku wakiwa hawana habari watoto wao wasipokwenda Skuli.
Sheha wa
Shehia ya Shamiani Mwambe Bi Safia
Khamis Ngwali ameelekeza lawama zake kwa wazazi kuwa ndiyo chanzo cha utoro wa
wanafunzi katika skuli hiyona wala siyo walimu kama wanavyodai baadhi ya
wazazi.
Sheha huyo
amesema wazazi wa watoto hao wamekuwa wakiwajali zaidi watoto wao kwa kuwapatia
huduma za chakula na mavazi lakini hawakumbuki umuhimu wa kuwapatia elimu
watoto hao.
Kwa upande
wake Afisa Elimu Wilaya ya Mkoani Mwalimu Seif Mohammed Seif amesema kuwa
tatizo kubwa lipo kwa wazazi wenyewe na wala sio walimu kwani walimu wamekuwa
wakifika skulini hapo na kusomesha.
Hata hivyo
amewataka wananchi wa Kisiwa cha Shamiani kuwa na mwamko wa kuwahimiza watoto
wao kwenda skuli kwa vile hao ndio watakaokuja kuwa waalimu wa baadaye na
kuondokana na utegemezi wa walimu kutoka nje ya kisiwa hicho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni