Habari

Jumanne, 17 Februari 2026

Sheria ya Zanzibar inavyolinda Watu Wenye Ulemavu Dhidi ya Kutukanwa na Kudhalilishwa Katika Jamii

NA ASIA MWALIM
MKATIKA dunia inayokumbwa na majanga ya mara kwa mara—kutoka kwa mafuriko, vimbunga, hadi matetemeko ya ardhi—ni muhimu kuhakikisha kuwa kila mtu anapata ulinzi sawa.Hili linakuwa la dharura zaidi kwa watu wenye ulemavu, ambao mara nyingi huachwa nyuma katika mipango ya dharura na usimamizi wa maafa. Zanzibar, kama sehemu ya Tanzania, imechukua hatua kadhaa kuunda sera ya maafa inayolenga kujenga jamii jumuishi.Lakini je, sera hiyo inazingatia kwa kina mahitaji ya watu wenye ulemavu? Makala hii inachambua kwa undani suala hilo, ikihusisha sauti za watu wenye ulemavu, jamii, jumuiya zao, wataalamu wa maafa, na sera yenyewe.
MUKTADHA WA ZANZIBAR NA CHANGAMOTO ZA MAAFAZanzibar ni visiwa vinavyokumbwa na changamoto za kijiografia na hali ya hewa, ikiwemo mafuriko, vimbunga, na kuongezeka kwa kina cha bahari. Kwa mujibu wa Tume ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar, majanga haya yamekuwa yakiongezeka kwa kasi, na hivyo kuhitaji sera madhubuti za kukabiliana nayo.
WATU WENYE ULEMAVU
Adil Mohammed mwenye ulemavu wa uoni anasema,watu wenye ulemavu wanakabiliwa na changamoto za kipekee ikiwemo kukosa taarifa kwa wakati kuhusu maafa.Anasema changamoto nyengine Miundombinu isiyo rafiki ya barabara kwa watu wenye ulemavu kupelelkea siku za maafa kupata changamoto za usafiri na mara nyengine kulazimika kupata misaada.Anafahamisha kuwa ukosefu wa huduma za dharura zinazozingatia mahitaji yao maalum kipindi cha majanga haujapewa kipaumbele hivyo kuwanyima haki zao.Bi Asha Suleiman, mkazi wa Mwera na mlemavu wa miguu, anasema wakati wa mafuriko mwaka jana, walipewa taarifa kupitia redio. 
“Mimi siwezi kusikia vizuri, na hakuna mtu aliyenifahamisha kwa wakati. Nilijikuta nimezingirwa na maji bila msaada.” alisema.Ushuhuda kama huu unaonesha pengo kati ya sera na uhalisia. Watu wenye ulemavu wanahitaji mifumo ya mawasiliano mbadala—kama vile ujumbe wa maandishi, alama, au hata wahamasishaji wa kijamii.
JUKUMU LA JAMII NA JUMUIYA ZA WATU WENYE ULEMAVUJumuiya kama Zanzibar Association of People with Disabilities (ZAPD) imekuwa mstari wa mbele katika kutetea haki za watu wenye ulemavu. Kwa mujibu wa  ZAPD, inaeleza utaratibu wake wa kutoa mafunzo kwa vikundi vya dharura kuhusu jinsi ya kuwahudumia watu wenye ulemavu, kupendekeza ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu katika kamati za mipango ya maafa na uundaji wa vituo vya dharura vinavyofikika kwa urahisi.“Tumejadiliana na Tume ya Maafa kuhusu kuingiza mahitaji yetu katika mipango ya dharura. Kuna maendeleo, lakini bado kuna kazi kubwa ya kufanya.”Ushirikishwaji wa Watu Wenye Ulemavu Katika MipangoSera ya Maafa Zanzibar inasisitiza ushirikishwaji wa jamii, bado watu hao wanalalamika kuhusu kukosa fursa ya kujumuishwa kikamilifu. Baraka Hassan mwenye ulemavu wa viungo anasema wanahitaji nafasi ya kutoa maoni katika mikutano ya mipango. kuwajumuisha katika kamati za utekelezaji na Walitoa maoni yao wakisema Maafa Hayachagui, Lakini Mipango Inaweza Kutoa Ulinzi Sawa, wakati majanga yanapotokea, ni muhimu watu hao kupata taarifa kwa wakati, huduma sahihi, au miundombinu inayowafaa, ili kuweka usalama wa maisha yao.Jamii, jumuiya za watu wenye ulemavu, wataalamu wa maafa, na serikali wanapaswa kushirikiana kwa dhati. Maafa hayachagui nani wa kumdhuru—lakini sisi tunaweza kuchagua kuwa jumuishi, wenye huruma, na wenye haki.
JUMUIYA YA WATU WENYE ULEMAVU ZANZIBAR (JUWAUZA)Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Salma Haji Saadat anasema,Zanzibar imebarikiwa kuwa na sheria nyingi za watu wenye ulemalu licha ya kuwa utekelezaji wake ni mdogo jambo ambalo linawakosesha fursa watu hao.Utekelezaji wa sheria hauna muamko wa kutosha kwani mambo mengi yanagharama na yanakuwa magumu kutekelezwa kwa sababu yanakuwa na gharama kubwa.
SERA YA MAAFA ZANZIBAR
Kwa mujibu wa Mtendaji wa ofisi inayohusika na maafa Zanzibar, alijitambulisha kwa jina la Fahad anasema Sera ya Maafa Zanzibar (Disaster Risk Reduction Policy) imeundwa kwa lengo la kupunguza hatari za maafa, kuimarisha uwezo wa jamii kukabiliana na majanga, kuhakikisha ushirikishwaji wa makundi yote ya kijamii.Aidha alisema katika nyaraka za sera hiyo, kuna marejeo ya makundi maalum kama vile wanawake, watoto, na watu wenye ulemavu. Hata hivyo, changamoto ni jinsi utekelezaji unavyofanyika kwa vitendo.
SHERIA YA MAAFA YA ZANZIBAR YA MWAKA 2015—ZANZIBAR DISASTER RISK REDUCTION AND MANAGEMENT ACTSheria hii ina sehemu mbalimbali zinazohusu mipango ya kitaifa, kamati za usimamizi kuanzia ngazi ya shehia hadi taifa, na wajibu wa wadau mbalimbali.

Ijumaa, 13 Februari 2026

SERA YA MAAFA ISIWAACHE NYUMA WATU WENYE ULEMAVU NA

 Na,ASIA MWALIM



KATIKA dunia inayokumbwa na majanga ya mara kwa mara—kutoka kwa mafuriko, vimbunga, hadi matetemeko ya ardhi—ni muhimu kuhakikisha kuwa kila mtu anapata ulinzi sawa.Hili linakuwa la dharura zaidi kwa watu wenye ulemavu, ambao mara nyingi huachwa nyuma katika mipango ya dharura na usimamizi wa maafa. Zanzibar, kama sehemu ya Tanzania, imechukua hatua kadhaa kuunda sera ya maafa inayolenga kujenga jamii jumuishi.Lakini je, sera hiyo inazingatia kwa kina mahitaji ya watu wenye ulemavu? Makala hii inachambua kwa undani suala hilo, ikihusisha sauti za watu wenye ulemavu, jamii, jumuiya zao, wataalamu wa maafa, na sera yenyewe.
MUKTADHA WA ZANZIBAR NA CHANGAMOTO ZA MAAFAZanzibar ni visiwa vinavyokumbwa na changamoto za kijiografia na hali ya hewa, ikiwemo mafuriko, vimbunga, na kuongezeka kwa kina cha bahari. Kwa mujibu wa Tume ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar, majanga haya yamekuwa yakiongezeka kwa kasi, na hivyo kuhitaji sera madhubuti za kukabiliana nayo.
WATU WENYE ULEMAVU
Adil Mohammed mwenye ulemavu wa uoni anasema,watu wenye ulemavu wanakabiliwa na changamoto za kipekee ikiwemo kukosa taarifa kwa wakati kuhusu maafa.Anasema changamoto nyengine Miundombinu isiyo rafiki ya barabara kwa watu wenye ulemavu kupelelkea siku za maafa kupata changamoto za usafiri na mara nyengine kulazimika kupata misaada.Anafahamisha kuwa ukosefu wa huduma za dharura zinazozingatia mahitaji yao maalum kipindi cha majanga haujapewa kipaumbele hivyo kuwanyima haki zao.Bi Asha Suleiman, mkazi wa Mwera na mlemavu wa miguu, anasema wakati wa mafuriko mwaka jana, walipewa taarifa kupitia redio. “Mimi siwezi kusikia vizuri, na hakuna mtu aliyenifahamisha kwa wakati. Nilijikuta nimezingirwa na maji bila msaada.” alisema.Ushuhuda kama huu unaonesha pengo kati ya sera na uhalisia. Watu wenye ulemavu wanahitaji mifumo ya mawasiliano mbadala—kama vile ujumbe wa maandishi, alama, au hata wahamasishaji wa kijamii.
JUKUMU LA JAMII NA JUMUIYA ZA WATU WENYE ULEMAVUJumuiya kama Zanzibar Association of People with Disabilities (ZAPD) imekuwa mstari wa mbele katika kutetea haki za watu wenye ulemavu. Kwa mujibu wa ZAPD, inaeleza utaratibu wake wa kutoa mafunzo kwa vikundi vya dharura kuhusu jinsi ya kuwahudumia watu wenye ulemavu, kupendekeza ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu katika kamati za mipango ya maafa na uundaji wa vituo vya dharura vinavyofikika kwa urahisi.“Tumejadiliana na Tume ya Maafa kuhusu kuingiza mahitaji yetu katika mipango ya dharura. Kuna maendeleo, lakini bado kuna kazi kubwa ya kufanya.”Ushirikishwaji wa Watu Wenye Ulemavu Katika MipangoSera ya Maafa Zanzibar inasisitiza ushirikishwaji wa jamii, bado watu hao wanalalamika kuhusu kukosa fursa ya kujumuishwa kikamilifu. Baraka Hassan mwenye ulemavu wa viungo anasema wanahitaji nafasi ya kutoa maoni katika mikutano ya mipango. 
kuwajumuisha katika kamati za utekelezaji na Walitoa maoni yao wakisema Maafa Hayachagui, Lakini Mipango Inaweza Kutoa Ulinzi Sawa, wakati majanga yanapotokea, ni muhimu watu hao kupata taarifa kwa wakati, huduma sahihi, au miundombinu inayowafaa, ili kuweka usalama wa maisha yao.Jamii, jumuiya za watu wenye ulemavu, wataalamu wa maafa, na serikali wanapaswa kushirikiana kwa dhati. Maafa hayachagui nani wa kumdhuru—lakini sisi tunaweza kuchagua kuwa jumuishi, wenye huruma, na wenye haki.
JUMUIYA YA WATU WENYE ULEMAVU ZANZIBAR (JUWAUZA)
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Salma Haji Saadat anasema,Zanzibar imebarikiwa kuwa na sheria nyingi za watu wenye ulemalu licha ya kuwa utekelezaji wake ni mdogo jambo ambalo linawakosesha fursa watu hao.Utekelezaji wa sheria hauna muamko wa kutosha kwani mambo mengi yanagharama na yanakuwa magumu kutekelezwa kwa sababu yanakuwa na gharama kubwa.
SERA YA MAAFA ZANZIBAR
Kwa mujibu wa Mtendaji wa ofisi inayohusika na maafa Zanzibar, alijitambulisha kwa jina la Fahad anasema Sera ya Maafa Zanzibar (Disaster Risk Reduction Policy) imeundwa kwa lengo la kupunguza hatari za maafa, kuimarisha uwezo wa jamii kukabiliana na majanga, kuhakikisha ushirikishwaji wa makundi yote ya kijamii.Aidha alisema katika nyaraka za sera hiyo, kuna marejeo ya makundi maalum kama vile wanawake, watoto, na watu wenye ulemavu. Hata hivyo, changamoto ni jinsi utekelezaji unavyofanyika kwa vitendo.
SHERIA YA MAAFA YA ZANZIBAR YA MWAKA 2015—ZANZIBAR DISASTER RISK REDUCTION AND MANAGEMENT ACTSheria hii ina sehemu mbalimbali zinazohusu mipango ya kitaifa, kamati za usimamizi kuanzia ngazi ya shehia hadi taifa, na wajibu wa wadau mbalimbali.

RADIO DAY NA WANAHARAKATII

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MAADHIMISHO YA SIKU YA REDIO DUNIANI 2026
Siku ya tarehe 13 Febuari 2026, dunia inaungana kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Redio 
siku iliyotangazwa na UNESCO mwaka 2011 na kupitishwa rasmi na Baraza Kuu la Umoja 
wa Mataifa mwaka 2013. Maadhimisho haya ni fursa ya kutafakari mchango wa redio 
katika kuhabarisha, kuelimisha, kuburudisha na kuimarisha misingi ya demokrasia, haki 
za binadamu na maendeleo endelevu.
Kaulimbiu ya mwaka huu, “Redio na Uaminifu” (Radio and Trust), inatukumbusha 
kwamba uaminifu ndio muhimili mkuu wa taaluma ya habari. Redio haiishi kwa nguvu ya 
mawimbi yake, bali kwa imani ya wasikilizaji wake. Bila uaminifu, hakuna ushawishi, bila 
ukweli, hakuna uwajibikaji.
Kwa mujibu wa Tume ya Utangazaji Zanzibar, kuna zaidi ya vituo 30 vya redio 
vinavyofanya kazi hapa nchini. Ukuaji huu ni ishara ya kupanuka kwa sekta ya habari na 
kuimarika kwa wigo wa mawasiliano. Hata hivyo, ukuaji wa idadi ya vituo haupaswi kuwa 
kipimo pekee cha mafanikio. Mafanikio ya kweli yapo katika ubora wa maudhui, uhuru 
wa uhariri, na uwezo wa redio kuwa sauti ya wananchi.
Redio imeendelea kuwa chanzo kikuu cha taarifa kwa wananchi wengi, hususan katika 
maeneo ya vijijini. Katika jamii nyingi zinazoendelea, redio ndio chombo kinachowafikia 
watu wengi zaidi kwa gharama nafuu na kwa lugha inayoeleweka.
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Irina Bokova, aliwahi kusisitiza umuhimu wa 
redio kwa kusema: “Radio is the mass medium that reaches the widest audience 
worldwide. It is a powerful communication tool and a low-cost medium. (“Redio ndicho 
chombo cha habari kinachowafikia watu wengi zaidi duniani. Ni chombo chenye nguvu 
kubwa ya mawasiliano na ni cha gharama nafuu.”)
Kauli hii inathibitisha kuwa redio si chombo cha kawaida, bali ni muhimili wa mawasiliano 
ya umma, hasa kwa makundi yaliyo pembezoni mwa maendeleo.
Hata hivyo, nguvu ya redio lazima iambatane na uhuru wake. Katibu Mkuu wa zamani 
wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, aliwahi kusema:”No one should underestimate the 
importance of a free media in a democracy.”(“Hakuna anayepaswa kubeza umuhimu wa 
vyombo vya habari huru katika demokrasia.”)
Maneno haya yanabeba ukweli usiopingika: bila vyombo vya habari huru na 
vinavyoaminika, misingi ya demokrasia hudhoofika.
Kwa muktadha wa Zanzibar, bado kuna changamoto za kisheria na kisera zinazoathiri 
tasnia ya habari. Miongoni mwa changamoto hizo ni matumizi ya sheria zilizopitwa na 
wakati kama Sheria ya Tume ya Utangazaji Zanzibar ya mwaka 1997 (iliyorekebishwa 
2010) na Sheria ya Usajili wa Wakala wa Habari, Magazeti na Vitabu Na. 5 ya mwaka 
1988. Aidha, bado kuna mapungufu katika ulinzi wa kisheria kwa waandishi wa habari na 
katika utekelezaji wa haki ya kupata taarifa za umma.
Sambamba na hilo, Ibara ya 19 ya Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu (UDHR) ya 
mwaka 1948 inaeleza kuwa “Kila mtu ana haki ya kuwa na maoni na kujieleza; haki hii 
inajumuisha uhuru wa kutafuta, kupokea na kusambaza taarifa kupitia chombo chochote 
cha habari… ”Hivyo basi, kulinda redio ni kulinda haki ya msingi ya binadamu.
Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Redio 2026, sisi wadau wa tasnia ya habari 
Zanzibar tunatoa wito kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuharakisha mchakato wa 
kupitisha Sheria Mpya ya Huduma za Habari inayozingatia viwango vya kitaifa, kikanda 
na kimataifa vya haki za binadamu.
Kuanzishwa kwa chombo huru cha usimamizi wa vyombo vya habari kinachojitegemea 
pamoja na kuhakikisha ulinzi wa kisheria na kiusalama kwa waandishi wa habari.
Kuimarisha utekelezaji wa haki ya wananchi kupata taarifa za umma na Vituo vya redio 
kuwekeza zaidi katika uandishi wa uchambuzi na ufuatiliaji wa masuala ya wananchi 
badala ya kujikita katika taarifa za matukio pekee.
Maadhimisho haya yasiishie kuwa tukio la sherehe. Yawe mwanzo wa hatua za mageuzi 
ya kweli katika sekta ya habari. Kwa sababu kama alivyowahi kusema mwanahabari 
mashuhuri Walter Cronkite:
“Freedom of the press is not just important to democracy, it is democracy.”
(“Uhuru wa vyombo vya habari si jambo muhimu tu kwa demokrasia - ndio demokrasia 
yenyewe.”)
Wadau wa habari tunasisitiza kuwa Redio inapolindwa na kupewa uhuru wake kamili, 
wananchi hupata sauti, wananchi wanapopata sauti, demokrasia huimarika, na 
demokrasia inapoimarika, taifa hustawi. Kulinda redio ni kulinda mustakabali wa Zanzibar.
IMETOLEWA NA:
Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC), 
Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA-ZNZ) 
Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar (WAHAMAZA) 
Baraza la Habari Tanzania, Zanzibar (MCT, ZNZ)
Jukwaa la Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania, Zanzibar (THRDC, ZNZ).

Alhamisi, 12 Februari 2026

USHIRIKI NA USHIRIKISHWAJI WA WATU WENYE ULEMAVU KATIKA SHUGHULI ZA KIJAMII.



NA ASIA MWALIM
KATIKA jamii yoyote yenye misingi ya usawa na haki, ushiriki na ushirikishwaji wa watu wote ikiwemo watu wenye ulemavu kwenye masuala ya kijamii bila ubaguzi ni nguzo muhimu ya maendeleo endelevu.Kwa bahati mbaya hapa kwetu kushiriki na kushirikishwa watu wenye ulemavu kwenye masuala ya kijamii halijapewa kipaumbele na mara nyingi familia huwatolea maamuzi.Hata hivyo, historia inaonesha kuwa kundi hili limekuwa likikumbwa na changamoto za kijamii ikiwemo kukosa urithi wa mali, kushindwa kushiriki sherehe za harusi, vikao vya familia, misiba, michezo na mikutano.Watu wenye ulemavu ni sehemu ya jamii yenye uwezo, ndoto, na mchango mkubwa katika nyanja mbalimbali za maisha lakini wengi wao wamekua wakilalamika kukuosa fursa hiyo.TAKWIMU ZA WATU WENYE ULEMAVUKwa mujibu wa ripoti ya Mtakwimu Mkuu wa serikali kupitia, sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2022, watu wenye ulemavu kuanzia miaka 7 na kuendelea, ni asilimia 11.4 ya watu wote waliohesabiwa Zanzibar.Ripoti ya Takwimu inaonesha, kiwango cha hali ya watu wenye ulemavu kimeongezeka kwa asilimia 3.9 kati ya sensa ya mwaka 2012 na sensa ya mwaka 2022 kwa kipindi cha miaka 10.Pia mkoa wa kaskazini Pemba una kiwango kikubwa cha watu wenye ulemavu kwa asilimia 13.3 na mkoa wa kaskazini Unguja una kiwango kidogo cha asilimia 10.3 ya watu wenye ulemavu.Matokeo ya sensa yanaonesha kiwango cha hali ya ulemavu kipo juu zaidi kwa wanawake ikilinganishwa na wanaume katika Mikoa mingi ya Zanzibar.Wanaume wenye ulemavu Zanzibar ni asilimia 10.3 na wanawake ni asilimia 12.3 ikiongozwa na Mkoa wa Kaskazini Pemba wenye idadi kubwa ya wanawake wenye ulemavu kwa asilimia 14.1 ikilinganishwa na wanaume wenye ulemavu asilimia 12.2.Mkoa wa Kaskazini Unguja wanaume ni asilimia 9.5 na wanawake ni asilimia 11.2.Mkoa wa Kusini Unguja unaonesha kuwa, wanaume asilimia 10.7 wanawake asilimia 12.4, Mkoa wa Mjini Magharibi wanaume asilimia 9.6 na wanawake asilimia 12.0, na Mkoa wa Kusini Pemba wanaume 11.3 asilimia na wanawake asilimia 12.8.HALI YA WATU WENYE ULEMAVU ZANZIBARFakihat Omar Abubakar (24) kijana wa kike mwenye ulemavu wa viungo anasema ameshuhudia, familia nyingi haziwashirikishi watu wenye ulemavu kwenye shughuli za kijamii hata zile zinazowahusu.Anasema bado familia zimebeba mitazamo hasi juu ya watu wenye ulemavu kuwashirikisha ipasavyo kwenye masuala ya kijamii ikiwemo sherehe zinazojumuisha watu wengi, misiba, vikao, mikutano n.k.“Ni kweli hata mimi nilihudhuria sherehe ya harusi ya kifamilia, lakini watu wengi walistaajabu kuniona, wakisema maneno ya kunidhihaki kwa sauti ya chini nilijisikia vibaya na sikuwa na la kufanya” alisema.“utawasikia wanasema, Eti ilikuaje huyu kumleta hapa harusini si wangemuacha atulie awalindie nyumba” alieleza baadhi ya maneno ya kejeli aliyotupiwa.Kuonekana mtu mwenye ulemavu kwenye mikusanyiko linachukuliwa tofauti kwenye jamii wengi wamezoea kuwaficha na kutowashirikisha harakati za kijamii kama sherehe za harusi.Fakihat anasema kuna changamoto nyingi zinapaswa kutatuliwa ikiwemo kukosa wakalimani wa lugha katika hospitali hasa kwenye huduma za uzazi ambako watu wenye ulemavu wa uziwi wanasumbuka wakati wakujifungua.“Jambo la kukosa mkalimani katika vituo vya afya linapaswa kuchukuliwa hatua za haraka ili kundi la watu wenye ulemeavu kueleza yanayowasibu” alisema.Hidaya Suleiman Rashid, (45) mwanamke mwenye ulemavu wa viungo anasema watu wenye ulemavu wanapaswa kuheshimiwa, kusikilizwa, na kupewa nafasi ya kuchangia.“Ikiwa familia haziwashirikishi kwenye vikao watapata fursa ya kuchangia na kutoa mawazo yao?” aliuliza.Kwenye suala la heshima kumeharibika zaidi wanaonekana hawana ulewa wa kutoa maamuzi yanayofaa kwa sababu zisizo na msingi.Changamoto nyengine ni watu wenye ulemavu kutelekezwa, pia kukoseshwa huduma za msingi na kutopewa urithi.JAMII YA ZANZIBARNasra Khatibu Suleiman anasema, kutoshirikishwa watu wenye ulemavu kwenye masuala ya kijamii ni pengo kati ya watu wenye ulemavu na jamii na kuzuia maendeleo ya pamoja.Anasisitiza jamii kutilia mkazo suala la watu wenye ulemavu mambo yanayowahusu, ili kushiriki shughuli za kijamii ikiwemo elimu, ajira, siasa na michezo. Anaiomba serikali kuhakikisha mazingira, sera, na huduma zinakuwa rafiki kwa watu wenye ulemavu ili kushiriki kikamilifu harakati za kijamii bila vikwazo.Rajabu Mohammed Abdallah na Mwanaisha Miraji wanasema Jamii ina nafasi ya kuhakikisha watu wenye ulemavu hawakumbwi na unyanyapaa. BARAZA LA TAIFA LA WATU WENYE ULEMAVUKatibu wa Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu Zanzibar, Ussy Khamis Debe anasema wanafuatilia utekelezaji wa mikakati ya ushiriki na ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu, ikiwemo kuwezesha uundwaji wa sera rafiki.Baraza limekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanashiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii, hasa kupitia ushawishi wa kisera na utekelezaji.JUMUIYA YA WATU WENYE ULEMAVU ZANZIBAR (JUWAUZA)Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Salma Saadat anasema Jumuiya hiyo ina utaratibu wa kuandaa warsha na makongamano ya kuhamasisha ushiriki na ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu,kuendesha kampeni za kupinga unyanyapaa na ubaguzi.SHERIA YA WATU WENYE ULEMAVU ZANZIBARKatika sheria ya watu wenye ulemavu Zanzibar inaeleza kuzuia ubaguzi dhidi ya watu wenye ulemavu, kuhakikisha upatikanaji wa huduma za afya, elimu, na ajira, kuweka masharti ya miundombinu rafiki kwa watu wenye ulemavu, kutoa adhabu kwa taasisi au watu wanaokiuka haki za watu wenye ulemavu.HitimishoUshiriki na ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu katika shughuli za kijamii si suala la hisani, bali ni haki ya msingi ya binadamu Zanzibar ina fursa ya kuwa mfano wa jamii jumuishi barani Afrika.Jamii inapaswa kuendelea kubadilika, kuondoa vikwazo, na kuhimiza usawa ili kujenga Zanzibar jumuishi, yenye mshikamano, na inayothamini kila mwanajamii bila kujali hali yake ya kimwili au kiakili.

Jumatatu, 9 Februari 2026

HADI KUFIKA MIAKA 62 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR ELIMU NI HAKI SIO UPENDELEO

Na ,Amina Ahmed Moh'd
 
Kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964, elimu ya maandalizi Unguja na Pemba haikuwa rasmi wala jumuishi. Ilitolewa kwa upendeleo wa kijamii na kikabila, na iliwafikia wachache wa tabaka la juu  maeneo ya mijini pekee.
 Watoto wa maskini, wakulima na wavuvi walikosa fursa
 Hakukuwa na skuli za serikali za maandalizi
 Vijijini, watoto walitegemea  (Madrasa)   elimu ya dini pekee
Hakukuwa na utaratibu wa lishe, walimu walikuwa wachache na wengi wageni wasio kuwa wazawa 
 Mfumo wa elimu ya maandalizi  ulikuwa wa kikoloni na kisultani, elimu ikiwa si haki ya kila ZANZIBAR 
LAKINI  BAADA YA MAPINDUZI YA 1964 – MIAKA 62 BAADAYE (2026)
Mapinduzi yameleta mageuzi makubwa katika elimu ambapo 
 Elimu ndani ya miaka 62 ya Mapinduzi  kupitia serikali ya awamu ya nane  iliyo chini ya Dk Hussein Ali Mwinyi  imekuwa ni haki ya kila mtoto bila ubaguzi wa kidini, itikadi za siasa ,uchumi ,maumbile wala hali za maisha kama ilivyokuwa kabla ya Mapinduzi  yam waka 64 .
Huku Zaidi ya skuli  262 za maandalizi Unguja na Pemba ndani  ya miaka 62 ya Mapinduzi  
 Skuli 97 zimekarabatiwa, 36 mpya zinajengwa maeneo mbali mbali .
 Walimu wapya 889 wameajiriwa ndani ya miaka 62 mwaka  (2025/26)
  Wanafunzi wapatao  105,101 (82.5%) wameandikishwa  jambo ambalo awali kabala miaka 62 ya Mapinduzi halikuwepo 
  Wanafunzi 63,099 (50%) wanapata lishe  maskulini  kupitia ruzuku maalum ya serikali  
 ZANZIBAR  YA LEO  katika elimu ina mfumo jumuishi wa elimu, miundombinu bora, walimu wenye sifa na huduma za kijamii maskulini  ,lishe  na mazingira yaliorafiki  kwa wote 
________________________________________

Miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar  kupitia serikali ya awamu ya nane inayoongozwa na Dk Hussein Ali Mwinyi ni ushahidi kuwa: Elimu si upendeleo  bali  Elimu ni haki kwa watu wa aina zote kuanzia madarasa ya awali.
Mapinduzi yameifanya haki hii kufika kwa kila mtoto wa Zanzibar popote alipo  mjini na Vijijini 


  Maono ya kiongozi bora huonekana pale elimu inapokuwa haki ya kila mmoja  huku Taifa imara hujengwa na viongozi wanaothamini elimu bila ubaguzi kwani Uongozi bora huacha alama kupitia elimu jumuishi na yenye usawa kuanzia ngazi ya awali hadi vyuo vikuu .
  


 JEE WAJUWA Kabla ya Mapinduzi (1964)
• Elimu ya maandalizi haikuwa rasmi wala jumuishi.
• Iliwafikia wachache wa tabaka la juu mijini pekee.
• Watoto wa maskini, wakulima na wavuvi walikosa fursa.
• Hakukuwa na skuli za serikali za maandalizi.
• Vijijini, watoto walipata elimu ya dini kupitia madrasa pekee.
• Walimu wachache, wengi wakiwa wageni wasio wazawa.
• Mfumo ulikuwa wa kikoloni na kisultani, elimu si haki ya kila mtoto.
Baada ya Mapinduzi (1964–2026)
• Elimu imekuwa haki ya kila mtoto bila ubaguzi wa dini, siasa, au hali ya maisha.
• Skuli za maandalizi 262 zimeanzishwa Unguja na Pemba.
• Skuli 97 zimekarabatiwa na 36 mpya zinajengwa.
• Walimu wapya 889 wameajiriwa.
• Wanafunzi 105,101 (82.5%) wameandikishwa.
• Wanafunzi 63,099 (50%) hupata lishe shuleni kupitia ruzuku ya serikali.
• Mfumo wa elimu sasa ni jumuishi, wenye miundombinu bora, walimu wenye sifa, na mazingira rafiki.
Hitimisho
Mapinduzi ya Zanzibar yamebadilisha elimu kutoka upendeleo wa kikoloni hadi haki ya kila mtoto. Leo, elimu jumuishi na yenye usawa imejengwa kuanzia madarasa ya awali hadi vyuo vikuu, ikionesha maono ya uongozi bora unaothamini elimu kwa wote.

FREELANCER  
    AMINA AHMED MOH`D – ( BIYAYA)
    0776 -859 184
    minnah1202@gmail.com