Habari

Jumatano, 23 Oktoba 2013

KUNAHITAJIKA MAPINDUZI YA FIKRA ZANZIBAR, KABLA YA MAMLAKA

Kama kuna jambo linaloimaliza Zanzibar katika ustawi wa kila kitu kwa sasa basi ni fikra mgando, hayo mengine yanafuatia ndivyo ninavyoweza kusema.

hayumkiniki kwamba licha ya kulalamika kwetu kwamba Zanzibar imekosa mamlaka ( Naam) lakini kiasi cha kushindwa hata kusimamia mambo ambayo angalau tuna maamuzi nayo basi nayo tushindwe.
Kwamba hata uzembe kule mahospitalini kwetu, wizi, na ubadhirifu wa kila aina katika maofisi ya serikali na katika jamii zetu nayo yasubiri mamlaka kamili. Hapa tumefeli tu hata hayo mamlaka yakija ni kazi bure.
Hakuna uadilifu, si serikalini si katika taasisi huru, si katika mamlaka za kidini wala katika maisha ya wanajamii mambo yote ni hohehahe tu. Mimi nadhani sisi Zanzibar tuna kazi pevu sana kwa mambo yalivyo leo na tusitegemee miujiza ya hio MAMLAKA hatujajiandaa sasa tutawezaje kufanikiwa hapo mbele?
Hebu fikiria Ni kiongozi gani mathalani yuko tayari kumuwajibisha mtendaji kwa makosa yanayofanywa. kwanza hao viongozi wamekosa vigezo vya kuwaadabisha wengine na mambo haya ndio yameipeleka Zanzibar hapa ilipo, kila kitu hapa kwetu kimeharibika na kilichobaki ni nyimbo za KUSIFU MAPINDUZI, tumetoka kwenye lengo halisi la mapinduzi na sasa tunaweweseka kwa kuimba na kibwagizo chake ni maarufu hapa Zanzibar . DAIMA ,DAIMA DAIMA TU. mbona udaima wa mapinduzi kadiri siku zinavozidi na kadiri tunavyozidi kuyasifu ndivyo ZANZIBAR inavyozidi kuelemewa na mambo na sio kutatuka? Nini kimezuiya sheria zilizotungwa kwa mbwembwe na vibwagizo vya ilani na misamiati lukuki kutekelezwa?
kwani hazipo sheria za manunuzi hapa Zanzibar? mbona hazifuatwi, sheria na kanuni za uajiri mbona kuna kupendeleana? Sheria za leseni mbona kuna kughushi? Mahkama hazipo kweli? mbona haki hazipatikani? ilimradi ZANZIBAR YETU IMEKWISHA.
Labda tungesema Zanzibar HAKUNA WASOMI mbona wapo tele. na pengine tungesema TUMEKOSA VIONGOZI ( inawezekana) lakini mbona wamejazana tele maofisini na vikao haviishi lakini hakuna mabadiliko kwa nini? Licha ya yote yawayo lakini ni FIKRA MGANDO TU. NADHANI TUNAHITAJI MAPINDUZI YA FIKRA MPYA ILI MAMLAKA YAKIJA TUJIIMARISHE NA SIO KUANZA UPYA WAKATI HUO.
Inashangaza zamani ilikuwa maofisini wamejaa wazee waliokulia kimapinduzi na elimu haikupewa nafasi lakini leo kumejaa vijana tena wasomi lakini tunashindwa kuisaidia jamii yetu katika nchi ndogo kama Zanzibar, ubinafsi umejaa kila kona
Utendaji wa mazowea kila kukicha na hata waje watu wenye mwelekeo wa mabadiliko BASI HUANDAMWA sisi TUNA NINI HAPA ZANZIBAR JAMANI?
ILI kufupisha mada niseme kwa ujumla wake Zanzibar tuna bahati mbaya ya MAKUSUDI yetu SISI WENYEWE KWANZA ya FIKRA MGANDO ambayo IMEENDELEZWA, IMELINDWA,IMERITHIWA na KUTHAMINIWA kiasi cha kujenga UTAMADUNI MBOVU wa kiutendaji na kwa ninavyoona panahitajika WINJI ili kuliondowa zigo hili
Tufikirie kuanza kuandaa MITAALA MIPYA YA ELIMU, KUANDAA MAFUNZO MAPYA YA UZALENDO, TUWE NA MFUMO WA MAADILI YA TAIFA LA ZANZIBAR yenye kwenda sambamba na desturi zetu, TUWE NA VIPAUMBELE VYETU na TUNU ZETU Ili ZANZIBAR YENYE MAMLAKA KAMILI IKIJA TUJIIMARISHE.
Tunahitaji MAPINDUZI YA FIKRA ZANZIBAR, MAZOWEA YAMETUMALIZA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni