Mkuu wa Kituo cha Kiislamu na Imam wa sala ya Ijumaa katika mji wa Manchester nchini Uingereza amesema kuwa, kati ya wajumbe 15 wa baraza la mji wa Manchester, wanane miongoni mwao ni Waislamu. Sheikh Ali Akbar Badi'i ameongeza kuwa, wajumbe hao wanajiandaa ili baadaye wajitumbukize kwenye kinyang'anyiro cha kuwania nafasi za ubunge nchini humo.
Akizungumza kwenye kongamano lenye mada 'Kukaribia Magharibi kwenye Uislamu' lililofanyika hapa nchini, Sheikh Ali Akbar Badi'i ameongeza kuwa uchaguzi wa bunge nchini Uingereza unaathiriwa na kura za Waislamu na dini tukufu ya Kiislamu ina taathira kubwa katika sekta ya uchumi nchini Uingereza na katika nchi nyingine za Magharibi.
Sheikh Badi'i ameelezea kuundwa jamii ya Kiislamu huko Ulaya na kushirikishwa kizazi cha pili katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni kusisitiza kuwa, Wamagharibi wenyewe wanatabiri kwamba, kufikia miaka 25 ijayo nusu ya jamii ya Wamagharibi itaundwa na wafuasi wa dini tukufu ya Kiislamu.

Na Mussa Said Abdur Rahman
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni