Habari

Alhamisi, 14 Novemba 2013

Jumuiya ya wafanyabiashara wenye asili ya Afica watiliana saini na Jumuiya ya wafanyabiashara ya Zanzibar

 Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wenye asili ya Afrika ya Kaskazini ya Pacific Bwana Peter Gishuru na Mwenzake Rais wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na wakulima Zanzibar Abdulla Abass wakitia saini Mkataba wa ushirikiano  wa Taasisi hizo mbili za Kibiashara kwenye Jengo la Wizara ya Biashara Mjini Seattle – Washington.Kati kati yao ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibarf Balozi Seif Ali Iddi akishuhudia kitendo hicho kinachotoa muelekeo wa ushirikiano wa kibiashara kati ya Zanzibar na Marekani.



Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika Picha ya Pamoja na Rais wa Chama cha Wafanyabiashara wenye viwanda na wakulima Zanzibar Abdulla Abass kushoto yake na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wenye asili ya Afrika ya Kaskazini Magharibi ya Pacific Bwana Peter Gishuru mara baada ya kutia saini mkataba wa ushirikiano katgi ya taasisi hizo hizo mbili za Kibiashara.

Picha na Hassan Issa,  Seattle, Washington State, Marekani

Na Othman Khamis Ame, Seattle, Washington State, Marekani
Jumuiya ya Wafanyabiashara wenye asili ya Afrika { African chamber of Commerce } ya Kaskazini Magharibi ya Pacific  imetiliana saini mkataba na Jumuiya ya Wafanya bishara wenye Viwanda na Wakulima ya Zanzibar katika kuanza hatua mpya ya ushirikiano baina ya pande hizo mbili.

Hafla hiyo fupi iliyofanyika katika jengo la Wizara ya Biashara ya Mji wa Seattle – Washington ilishuhudia pia na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Mawaziri na makatibu wakuu wa SMZ aliofuatana nao kqwenye ziara yake ya kiserikali Nchini Marekani.

Kwa upande wa Jumuiya ya wafanyabiashara wenye asili ya afrika saini ilitiwa na  Rais wa Jumuiya hiyo Bwana Peter Gishuru wakati ule wa Chama cha Wafanyabiashara wenye viwanda na Wakulima iliweka na Rais wajke Bwana Abdulla Abass.

Akizungumza mara ya utiaji saini huo Rais wa Chama cha wafanyabiashatra wenye viwanda na wakulima Zanzibar Nd. Abdulla Abass aliishukuru Jumuiya hiyo kwa uamuzi wake wa kuualika ujumbe wa Zanzibar katika Mkutano wao wa 15 ambao umezaa matunda.

Bwana Abass alisema makubaliano hayo ya pande hizo mbili yatasaidi kutoa nafasi kwa wanachama wa taasisi hizo mbili kubadilishana uzoefu katika masuala ya  ya Biashara kupitia maonyesho ya biashara.

Hata hivyo rais huyo wa chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na wakulima Zanzibar alitanabahisha kwamba saini hiyo ya ushirikiano haitahusisha masuala ya Kisiasa na kidini.

Mapema Rais wa Jumuiya Wafanyabiashara wenye asili ya Afrika ya Kaskazini ya Pacific Bwana Petre Gishuru alieleza kwamba ushirikiano huo utatoa fursa kwa pande hizo mbili kuangalia maeneo ya uwekezaji.

Bwana Gishuru alifahamisha kwamba mpango wa kubadilishana uzoefu baina ya wanachama wa pande zote za Taasisi hizo  hasa katika sekta ya biashara wanayowajibika nayo.

Katika kuimarisha ushirikiano wa pande hizo mbili Jumuiya ya wafanyabiashara wenye asili ya Afrika  ilito mualiko kwa Chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na wakukima Zanzibar kushiriki mkutano huo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni