Habari

Ijumaa, 22 Novemba 2013

Kova amtaja anayeshikilia laptop ya Mvungi

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Sulaiman Kova, amemtaja mkazi mmoja wa Jiji la Dar es Salaam kwamba ndiye anayeishikilia komputa mpakato (laptop) ya marehemu Dk. Sengondo Mvungi.



Mtu huyo (jina tunalihifadhi), mkazi wa  Vingunguti, anadaiwa kuwa ndiye anahodhi ya marehemu aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Kova alisema jana kuwa jeshi hilo limechukua hatua hizo baada ya kufanya uchunguzi wa kina katika upelelezi imegundulika kwamba kompyuta ya marehemu inamilikiwa isivyo halali na mtuhumiwa huyo.

Alisema mtu huyo ameingia katika sifa ya watu wanaotafutwa bila kificho wanted person(S) (Sheria hii pia inatumika Kimataifa na kuwa picha ya mtuhumiwa huyo itaonyeshwa katika vyombo vya habari ili mtu yeyote atakayemwona na kumtambua ajulishe Jeshi la Polisi kwa madhumini ya kumkamata na kupata laptop hiyo.

Aliongeza kuwa, kuna dalili kuwa mtuhumiwa huyo amegundua kwamba anatafutwa  hivyo anakwepa kukamatwa na anajificha maeneo tofauti tofauti ya jiji ikiwa ni pamoja na kusafiri sehemu mbalimbali nchini kukwepa mkono wa sheria.

Alisema Jeshi la Polisi Kanda Maalum linaendea kufanya jitihada kubwa kwa lengo la kuipata “laptop” hiyo pamoja na simu moja ya marehemu.

Aliwaomba raia wema wasisite kutoa taarifa zitakazosaidia kumkamata mtuhumiwa huyo.

Watuhumiwa kumi walishakamatwa kuhusiana na tukio hilo.
CHANZO: NIPASHE

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni