Habari

Jumanne, 19 Novemba 2013

Nyumba Salama zapongezwa Pemba.


Today at 8:33 AM
PEMBA .19/11/2013.

Wanaharakati  wanaopinga matendo  ya  ukatili wa kijinsia na udhalilishaji wa wanawake na watoto  Kisiwani Pemba ,wamepongeza uwamuzi wa Serikali wa kuanzisha nyumba salama ambayo itakuwa inawahifadhi wahanga wa matendo ili kusaidia kupatikana kwa uwamuzi katika vyombo vya sheria .

 Wamesema kuwa kuanzishwa kwa nyumba hiyo kutaisaidia kupatikana na ufumbuzi wa kesi za ukatili wa kijinsia na udhalilishaji wa wanawake na watoto zinazori[pitiwa mahakamani.
 
Wakizungumza kwenye kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Kilimo Weni , Wilaya ya Wete , wamesema kuwa pamoja na kuanzishwa kwa nyumba hiyo , lakini ni budi kwa Serikali kuwaelimisha wananchi juu ya uwepo wa nyumba hiyo pamoja na majukumu yake .
 
Sheha wa Shehia ya Mjini Ole , Bw Khamis Shaban amesema kuwa bado wananchi wanahitaji kupatiwa elimu ili waweze kutambua uwepo wa nyumba hiyo huku pia akisisitiza kwamba watendaji wa nyumba hiyo wanapaswa kuwa waaminifu .
 
Naye Mohammed Ali Hamad kutoka Jeshi la Polisi Micheweni , amesema kuwa ni budi jamii kuwapa mafunzo mema watoto wao wakati wakiwa na umri mdogo ili kuwakinga kujiingiza kwenye matendo maovu .

Akifafanua kuhusu  nyumba hiyo  Ismail Salum Mgeni kutoka Shirika la Action Aid Pemba amesema kuwa moja ya majukumu ya nyumba hiyo ni kuwahifadhi wahanga wa matendo hayo , ili kuzuia kusiwepo na suluhu kwa pande zinazohusika .
 
Mgeni amesema kuwa nyumba hiyo  ambayo siri , itakuwa ni msaada mkubwa katika kuyapatia ufumbuzi matendo ya ukatili wa kijinsia na udhalilishaji wa wanawake na watoto  yanayotokea katika maeneo mbali mbali ya Kisiwa cha Pemba .
 
mwisho .
 
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni