Habari

Jumamosi, 23 Novemba 2013

Shein anatambua tulikotoka na tuendako

Ni Uungwana kumpa mtu haki yake. Katika toleo hili tuna maka-la yenye kumpa haki yake Rais Ali Mo-hamed Shein kwa msimamo wake wa kuitetea Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) na kumkinga Makamu wake wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamadi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF).


Si siri kwamba kuna baadhi ya Wa-zanzibari ambao kila siku, usiku na mchana, wanakula njama za kuihu- jumu SUK. Wanaitwa wahafidhina kwa sababu hawana siasa za kileo, za kimaendeleo. Hawataki Serikali hiyo ifanikiwe.
Kwa hakika, hawataki Se-rikali hiyo iendelee kuishi. Wanataka ife, leo kesho.Wanaiombea Serikali hiyo mauti kwa sababu wanaelewa vilivyo nini kina-choweza kutokea Serikali hiyo ikifa au hata ikisambaratika tu.
Wanachotaka wahafidhina hao, am-bao ni wachache sana katika jamii yetu, ni kuirejesha Zanzibar kule ili-kotoka na tusikotaka kurudi. Wa-nachotaka wao ni kuiona Zanzibar ina machafuko, michirizi ya damu na uhasama utaovifanya visiwa vyetu visikalike.
 Hali hiyo ndiyo wanayoililia, ndiyo wanayoitilia ubani irudi, tena kwa haraka sana.Hawataki kuiona Zanzibar yenye utu-livu na amani — hali ambazo ni mu-himu kwa maendeleo. 
Hakuna taifa linaloweza kuendelea ikiwa halina utengamano, utulivu na hali ya amani.Wahafidhina hao wachache, ambao hatuchoki kuwaombea dua Mungu awahidi, wana silaha kadhaa wana-zozitumia ili kulifanikisha lengo lao.
Silaha yao kubwa ni fitna. Kwanza wanataka kuwafitinisha wabia katika SUK. Na wanaanza hukohuko juu kuwagonganisha vichwa wakubwa wa Serikali hiyo. Mishale yao ya fitna wamekuwa wakiilenga kwa Maalim Seif.
 Wanavyo ona wao ni kwamba ni wao waliomweka Maalim Seif katika kiti cha umakamu wa Rais.Wanachosahau au wasichokijua ni kwamba hii si Serikali iliyo mali yao. Ni Serikali ya Wazanzibari wote. Wala hii si Serikali inayoundwa na chama kimoja. Ni Serikali iliyoundwa na vyama vyote viwili vikuu vilivyochuana katika uchaguzi mkuu uliopita. 
Hivyo ndivyo Katiba ya Zanzibar isemavyo baada ya kura ya maoni ya 2010 iliyoidhinisha kwa asilimia kubwa uundwaji wa Serikali aina hiyo.Mchezo walioupanga ni kumpaka matope Maalim Seif na kumfitinisha na Rais wake.
Matamshi ya Rais Shein alipozungumza na waandishi wa habari hivi majuzi yalikuwa na lengo la kuukata huo mzizi wa fitna. Kwa hilo hatuna budi ila kumpa heko Rais Shein. Tunampa heko huku tukimsihi aendelee kuwa na ujasiri wa kuushika uzi huohuo.
Wanaitumia pia fitna kujaribu kutufitinisha sisi Wazanzibari wa kawaida na kujaribu kutugawa baina ya Wapemba na Waunguja. Watafurahi wakituona tunapofuana macho na kuchinjana.
Silaha nyingine inayotumiwa na hao wanaojikakamua kutuletea balaa ni kuzipanda na kuzipalilia mbegu za chuki.
 Hawakuanza jana. Walianza na chuki za kikabila. Sasa wamekamia kupalilia chuki kati ya Pemba na Unguja ikiwa ni sehemu ya mkakati wao niliokwishautaja wa kutugawa.
Bahati nzuri hakuna Mzanzibari mwenye akili yake timamu anayewasikiliza na kuwatia maanani wanapozungumzia juu ya kuzitenganisha Pemba na Unguja. 
Wengi wa Wazanzibari wanawaona hawa wahafidhina kuwa ni muflis wa kisiasa. Hawana lao jambo. Na wenyewe wanajijuwa na ndio maana wanatapatapa.
Silaha yao ya tatu ni kutumia vitisho. Wanajaribu kumtisha kila mtu wakisahau kwamba enzi za kutishana zimekwisha zamani Zanzibar. 
Hii tuliyo nayo ni enzi ya siasa mpya na mwelekeo mpya.Hatusemi kwamba siasa zetu ni safi safina wala hatusemi kwamba Serikali tuliyo nayo imekamilika. Lakini tunachosema na kukitambua ni kwamba Wazanzibari kwa wingi wetu tumeamua kuwa wamoja, kuziacha siasa za kutugawa na za kuturudisha nyuma. 
Tunachotaka ni maendeleo na ufanisi wetu sote bila ya kujali, kabila, dini, itikadi za kisiasa au kisiwa gani au kijiji gani tumetoka.Inavyoonyesha ni kwamba Rais Shein naye pia anayatambua haya na ndio maana aliyasema aliyoyasema alipokutana majuzi na waandishi wa habari
Chanzo Zanzibar Daima

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni