Habari

Jumanne, 26 Novemba 2013

Wanasiasa Zanzibar watuhumiwa kuingilia mahakama

Ni utafiti uliofanywa na mhadhiri mmoja
Zanzibar. Baadhi ya viongozi katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar wanatuhumiwa kuingilia utendaji kazi wa mahakama kinyume na misingi ya utawala bora visiwani humu.


Hatua hiyo inapingana na dhamira ya Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein ambaye ofisi yake inawekwa mbali na kama shutuma hizo tangu aingie madarakani mwaka 2010 na kuunda Serikali inayovishirikisha vyama vya CCM na CUF.
Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Tunguu Zanzibar Ali Ahmed Uki, amebainisha mambo mengi katika taarifa ya utafiti wake kuhusu miaka 50 ya mahakama tangu kufanyika kwa Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964.
Uki anasema kuwa katika taarifa hiyo utafiti umeonyesha kuwa baadhi ya viongozi wa kisasa, wamekuwa wakiingilia utendaji kazi wa Mahakama ya Zanzibar kinyume na sheria na msingi ya utawala bora.
“Tuhuma za ushawishi wa wanasiasa kuingillia utendaji kazi za mahakama zimejitokeza katika utafiti wa miaka 50 ya Mahakama Zanzibar tangu kufanyika kwa Mapinduzi ya Januari 12 mwaka 1964.” alisema Uki
Maelezo hayo ameyawasilisha katika kongamano lililowashirikisha wanasheria na kufunguliwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu.
Mwanasheria Uki alisema harufu ya rushwa inaonekana kuchukua nafasi kubwa mahakamani na kusababisha wananchi wanyonge kupoteza haki.
Alisema hata hivyo malalamiko kuhusu rushwa yamekuwa yakisikika baada ya mahakama kutoa uamuzi wake.
Alisema katika miaka 50 ya Mapinduzi mahakimu wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira magumu.
Mwananchi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni