NA CORRESPONDENT
11th October 2013
B-pepe
Chapa
Tukio hilo limemgharimu mtunza stoo wa hospitali hiyo, Mary Mayombe, kuondolewa katika nafasi yake kutokana na mgongano kati yake na bosi baada ya kumkwamisha kuchukua kiasi hicho cha mafuta.
Afisa Ugavi wa Wilaya ya Manyoni, Genesius Rugemalila, amekiri kupokea mgogoro huo na kufanya mabadiliko ya kumhamisha Mayombe kwa usalama wake.
Mayombe katika mahojiano na gazeti hili amekiri kuondolewa katika kazi yake ya kutunza stoo baada ya kuzuia lita 2000 ambazo zilikuwa zitoke kinyume na utaratibu.
Baadhi ya wafanyakazi katika hospitali hiyo walisema Kaimu Mganga Mkuu, Dk. Rahim Hangai ambaye amekuwapo hospitalini hapo miezi minane iliyopita, amekuwa na kashfa nyingi, hivyo wamemuomba Mkurugenzi wa wilaya ya Manyoni kumhamisha kutokana na kuonyesha udhaifu katika kazi yake.
Wakiorodhesha msururu wa tuhuma, walisema Dk. Hangai hakai ofisini muda mwingi badala yake amekuwa mtu wa kujirusha mjini Dodoma kwa safari zake binafsi hali ambayo imesababisha wafanyakazi kuchelewa kazini kutokana na uzembe wake.
Tuhuma nyingine zinazomkabili ni kutoa tenda ya kuweka umeme wa jua wenye thamani ya Sh. 18,000,000.00 bila kufuata taratibu na mtu aliyepewa tenda hiyo si mzabuni wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.
Wamedai kuwa Dk. Hangai amekuwa akiwanyanyasa na kuwatisha watumishi wanapodai stahiki zao kwa kuwahamisha kiholela bila malipo kwa kuwaondoa kwenye madaraka waganga wafawidhi wa vituo vya Kintinku na Ntumbi.
Alipotafutwa kujibu tuhuma hizo, Dk. Hangai alisema tuhuma zote ni majungu.
Kuhusu kujirusha Dodoma, alisema hayo ni mambo binafsi hayahusiani na kazi.
Akizungumzia tuhuma za mafuta, alisema kuna taratibu zake za kuchukua hivyo isingewezekana kuchukua kiasi hicho kikubwa cha mafuta.
Kuhusu suala la zabuni ya umeme, alisema tenda yoyote inayoanzia milioni tatu, lazima itangazwe gazetini lakini hakufafanua lini ilitangazwa.
CHANZO: NIPASHE
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni