NA BEATRICE SHAYO
11th October 2013
B-pepe
Chapa
Alisema hayo jana jijini Dar es Salaam alipozindua mpango wa usomaji vitabu wenye lengo la kuhamasisha watu kujisomea.
Zaidi ya asilimia 65 ya wanafunzi walifeli mtihani wa kidato cha nne mwaka jana, matokeo ambayo yaliilazimu serikali kuunda tume ili kubaini chanzo cha hali hiyo.
Wanafunzi 126,851 walifanikiwa kufaulu mtihani kati ya wanafunzi 397,132 ambao walifanya mtihani huo.
Hata hivyo, Mkapa aliwalaumu wazazi kwa kutojihusisha na tabia ya usomaji wa vitabu hali ambayo husababishia watoto wao kuwaiga na kuacha kujisomea vitabu.
Alisema kusoma vitabu ni moja kati ya vitu vilivyomfanya aweze kufanikiwa maishani kutokana na tabia yake ya kupenda kujisomea vitabu… "Mpaka sasa ninayo maktaba ya vitabu nyumbani kwangu ambavyo vinajumuisha mambo mbalimbali katika ulimwengu huu," alisema.
Mkapa alizitaja faida zitokanazo na usomaji vitabu kuwa inamjengea msomaji uelewa mpana wa kufafanua jambo pamoja na kumpatia fursa mbalimbali za maendeleo.
Hata hivyo, Mkapa aliwataka Watanzania kujijengea tabia ya kujisomea vitabu kwani ni njia mojawapo ya kuzifikia fursa za maendeleo.
"Si dalili nzuri kwa nchi inayoendelea kama ya kwetu watu kutopenda kujisomea vitabu kwani usomaji vitabu ni njia mojawapo ya maendeleo,” alisema Mkapa.
Kwa upande wa mwazilishi wa mpango wa usomaji vitabu, January Makamba, alisema tunatakiwa kuwa na idadi kubwa ya watoto wanaopenda kusoma vitabu kama wanavyopenda kuangalia televisheni.
Alisema idadi hiyo itapatikana kama wazazi wakiwajengea msingi wa usomaji watoto wao tangu wakiwa wadogo.
CHANZO: NIPASHE
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni