Mtu ambaye
anadaiwa kuwa ni askari wa KMKM amemshambulia mkusanya mapato wa Mamlaka ya
Maji Zanzibar (ZAWA) tawi la Pemba ambaye anafanyakazi katika Shehia ya Bopwe
Wilaya ya Wete.
Akizungumzia
kadhia hiyo Haji Haji Khamis ambaye ndiye aliyefanyiwa shambilio hilo,amesema
ameshambuliwa askari huyo wa KMKM aliyemtaja kwa jina la Hamad Said baada ya
kukata maji karibu na nyumba yake aliyokuwa amejirejeshea bila kufika ofisini
kulipia deni analodaiwa.
Amesema siku
ya tarehe 19 mwezi huu alikata maji katika nyumba ya askari huyo,lakini siku ya
tarehe 21 alipokuwa akipita kutoa bili za malipo ya maji alikuta huduma ya maji
kwa Bw. Hamad imesharejeshwa bila ya kufuatwa kwa taratibu na ndipo alipoamua
kuikata.
Hata hivyo
amesema baada ya kuikata huduma hiyo muda mfupi baadaye alikutaka na Hamad na
ndipo alipoanza kumshambilia kwa nguni za uso na mdomoni na kumpatia maumivu.
Afisa
Uhusiano wa ZAWA Pemba Suleiman Annas Massoud amesema Mamlaka imeipokea taarifa
hiyo kwa masikitiko kwa vile mfanyakazi huyo alikuwa akitekeleza kazi zake kwa
mujibu wa taratibu.
Hata hivyo amesema
Mamlaka hiyo itashirikiana na vyombo vya sheria kuona mtu anachukuliwa hatua za
kisheria kutokana na kitendo hicho cha uvunjifu wa amani
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Shekhani Mohammed Shekhan amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema jeshi la polisi nipo njiani kukamisha ushahili kumfikisha mahakamani mtu huyo.
Ameseama anasikitishwa na kitendo kilichofanywa na askari huyo wa KMKM,kwa kufanya shambulizi hilo huku akijua aliyemshambila alikuwa akifanya kazi yake kihalali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni