Habari

Jumamosi, 26 Oktoba 2013

Mkoa wa Kusini Pemba awahimiza vijana kwenda kujiandikisha katika daftari na wapiga kura.

                                                       
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Juma Kassim Tindwa amewataka wananchi wa Mkoa huo kuendeleza amani na utulivu iliopo wakati wa uandikishaji wapiga kura wapya unaonza leo katika mkoa huo.

Amewaomba wananchi kujiepusha na vitendo vyovyote vitakavyoweza kuashiria vurugu na uvunjifu wa amani na utulivu katika kipindi chote ambacho daftari litakuwa katika mkoa huo.
Akizungumza na waandishi wa habari huko ofisini kwake Chake Chake. 

M.h Tindwa amesema Serikali ya Mkoa wa Kusini Pemba haitaacha kuchukua hatua kwa mtu au kikundi chochote kitakachojaribu kutaka kuvunja amani na utulivu uliopo.

Hata hivyo amesema  watendaji wa tume ya uchaguzi watatimiza wajibu wao wa kumwandikisha kila  wenye haki ya kuandikishwa kuwa mpiga kura kutokana na sfa zinazohitajika.

Kwa upande mwendine Mkuu wa Mkoa huyo amewahimiza vijana wote waliotimiza umri wa miaka 18 na wenye sifa ya kuandikishwa kufika katika vituo hivyo waweze kuandikishwa kuwa wapiga kura.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni