Mnara Miaka 50 ya Mapinduzi Kujengwa. Kugharimu Bilioni Moja, Kumalizikla Januari.ZSSF Yapewa Kandarasi ya Usimamizi. Kutumika Kibiashara, Kuvutia Watalii Zanzibar.
Huu ndio Mnara unaotarajiwa kujengwa katika Viwanja vya Michenzani kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi unatarajiwa kuanza ujenzi wake kuanzia sasa na kuwa Kivutio cha Watalii wanaokuja kutembelea Zanzibar kama ilivyo sehemu nyengine za Dunia kuwekwa sehemu ya kumbukumbu ya matukio muhimu.
NA MWANDISHI WETU, ZANZINEWS
Serekali ya Mapinduzi Zanzibar SMZ inakusudia kujenga mnara maalum utakaotoa kielelezo cha kumbukumbu ya miaka 50 tangu yafanyike Mapinduzi Matukufu ya mwaka 1964.
Januari 12 mwakani Zanzibar itaadhimisha kutimia miaka 50 tangu kufanyika kwa mapinduzi ya mwaka 1964 ambayo yaliuondosha utawala wa Sultani .
Akizungumza na waandishi wa habari huko Ofisini kwake Vuga Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed, ujenzi wa mnara huo utaambatana na ujenzi wa kituo cha ukuzaji uchumi ambacho kitakuwa na uwezo wa kutoa ajira ya watu 80.
Waziri Aboud alisema mnara huo unatarajiwa kujengwa katika eneo la Muembekisonge karibu na na jingo la maendeleo la michezani jumba namba 2, ambapo hivi sasa limekuwa limekuwa likitumiwa kwa ajili ya mapumziko.
Alisema mnara huo unajengwa katika eneo hilo kwani ni kitivo na chemchem ya maandalizi yaliyofanikisha kufanywa kwa mapinduzi hayo.
Waziri huyo, amesema ujenzi huo wa kumbukumbu hiyo, utaenda sambamba na kuligeuza eneo hilo kuwa la kiuchumi, kutokana na mnara huo utaambatana na ujenzi wa maduka ya kisasa pamoja na shughuli za kukuza utalii Zanzibar na kumbukumbu ya Mpapinduzi ya Zanzibar.
Alisema Serekali ya Mpinduzi Zanzibar inatarajia kutumia zaidi ya shilingi bilioni moja, ambazo zitatokana na viazio mbalimbali ukiwemo mchango wa Serekali na Taasisi binafsi na kusimamiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF.
Alisema ndani ya ujenzi wa mnara huo, unatarajiwa kuwa na maeneo ya kuweka kumbukumbu ya shughuli za Mapinduzi zikiwemo zana zilizotumika wakati wa Mapinduzi ya Zanzibar jambo ambalo litavutia watalii wanaotembelea Zanzibar.
Aidha alisema eneo jengine ndani ya mnara huo, linakusudiwa kuwekwa mikahawa na ukumbi mkubwa wa kufanyia shughuli mbalimbali,jambo ambalo linaweza kusaidia kukuza Utalii wa Zanzibar.
Akiendelea Waziri Aboud alisema ujenzi huoutaenda sambamba na kulifanyia mabadiliko eneo hilo kwa kuruhusu kuwepo kwa bustani mpya ya mapumziko pamoja na eneo la uegeshaji wa magari.
Mhe. Aboud alisema mabadiliko hayo yatahusisha ujenzi wa jingo jipya la kituo kikuu cha biashara kwa kejenga maduka makubwa (super market),ambayo itaweza kupunguza na kutoa ajira kwa watu zaidi ya 80, ikiwa ni hatua itakayosaidia kupunguza mrudikano katika eneo la darajani.
Alisema Serekali imeamua kuweka mnara huo, ikiwa ni sawa na mfumo wa baadhi ya mataifa duniani, ambayo yamekuwa na vielelezo vya aina hiyo, ikiwemo Paris, Ufaransa na Shangai China.
Kutokana na kuwepo kwa dhamira hiyo, Waziri Aboud aliwatakaka wananchi kuiunga mkono serekali katika ufanikishaji wa ujenzi wa Mnara huo, pale kazi zitakapoaza kwa kutofanya bughu mahali hapo.
Alisema serekali inachokifanya ni kuona eneo hilo linaimarishwa zaidi kuwa la kisasa na lenye kuiwezesha Zanzibar kukuza Uchumi na Utalii wa nchi kwa vile inatarajiwa kuwa ni kivutio kikubwa kwa mataifa mbalimbali duniani.kujua historia ya nchi hii.
Waziri Aboud alieleza wanatarajia kuona kazi hiyo inakamilika katikamwezi wa Januari, lakini inawezekana kuwa endelevu baada yakipindi hicho kupita kutokana na ramani ya shughuli hizo kuhusisha mambo mengi na itakachoaza nacho ni kuweka jiwe la msingi.
Kutokana na mipango hiyo ya Serekali Waziri Aboud, pia aliwaombawananchi kushiriki katika shughuli mbalimbali za sherehe hizo zikiwemo za kujitayarisha kushiriki katika maonesho ya aina yake yatakayofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Taifa SUZA kampasi ya Beit –el raas.
Amesema katika maonesho hayo serekali inatarajia kuonesha shughuli mbalimbali za Taasisi za Serekali ya mapinduzi Zanzibar kwa kuonesha mafanikio yaliopatikana katika kipindi cha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
MWISHO.
imewekwa kwa msaada wa ZANZINEWS
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni