Habari

Jumamosi, 12 Oktoba 2013

Uzinduzi wa Mradi wa Ujenzi wa Hifadhi ya Eneo la Historia katika Kanisa la Mkunazini Zanzibar.

Saturday, October 12, 2013


Balozi wa Umoja wa Ulaya Nchini Tanzania Balozi Filiberto Ceriani Sebregondi, akikata utepe kuashiria Kuzindua  Mradi wa Kuhifadhi Eneo la Historia la Kanisa la Mkunazini Zanzibar, ambalo linabeba historia ya Utumwa Zanzibar kwa kuwa ndipo lilipokuwasokon la kuu la watumwa, akishuhudia uzinduzi huo ni Waziri wa Habari,Michezo, Utamaduni na Utalii Zanzibar Said Ali Mbarouk.uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya Kanisa la Mkunazini.

 Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk,na Balozi wa Jumuiya ya Ulaya Nchini Tanzania Balozi Filiberto Ceriani Sebregondi, wakiondosha kipazia kuashiria kwa uzinduzi wa mradi huo ya ujenzi eneo hilo la historia katika Visiwa vya Zanzibar, kwa Watalii wanaotembelea Zanzibar hufika katika eneo hilo kuangalia historia ya Sokola Watumwa.

   

Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Micheo Mhe. Said Ali Mbarouk, akihutubia katika sherehe za Uzinduzi wa Mradi wa Kuhifadhi eneo la Historia ya Soko la Watumwa katika eneo la Kanisa la Mkunazini Zanzibar.

Balozi wa Umoja wa Ulaya Nchini Tanzania Filiberto  Ceriani, akihutubia baada ya uzinduzi wa mradi huo wa ujenzi wa hifadhi ya sehemu ya historia ya Soko la Watumwa Zanzibar katika eneo la Kanisa la Mkunazini Zanzibar.


Msimamizi wa Mradi huo Stephen Battle, akitowa maelezo ya mradi huo wakati wa uzinduzi wake uliofanywa na Balozi wa Umoja wa Ulaya Tanzania Balozi FilibertoCeriani, amezinduwa mradi huo katika viwanja vya Kanisa la Mkunazini Zanzibar.



Katibu wa Kanisa la Mkunazini Nuhu Justine Sallaya, akitowa maelezo wakati wa sherehe hizo za uzinduzi wa Mradi wa kukarabati eneo hilo la historia ya Zanzibar kupitia Mradi wa Jumuiya ya Ulaya EU.







CHANZO ZANZINEWS

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni