Habari

Jumamosi, 12 Oktoba 2013

HAUSIGELI AMNYONGA MTOTO WA BOSI NA KUITUPA MAITI YAKE KWENYE DIMBWI LA MAJI MACHAFU HUKO KIBAHA.....WAZAZI WA MTOTO WAZIMIA...!!

NI ukatili uliopitiliza! Hausigeli aliyejulikana kwa jina moja la Ester (14) yupo matatani kwa madai ya kumuua mtoto Arafat Allan (3) kwa kumnyonga shingo na kumpiga na kitu kizito kichwani kisha kuutumbukiza mwili wake kwenye dimbwi la maji machafu, Risasi Jumamosi limekamata tukio zima.
Tukio hilo lilijiri Jumapili iliyopita Mailimoja, Kibaha mkoani Pwani ambako marehemu alikuwa akiishi na wazazi wake.
Akizungumza kwa uchungu, mama mzazi wa mtoto huyo, Zakia Peter ambaye amelazwa katika Zahanati ya Kellen kutokana na mshtuko wa kifo cha mwanaye, alisema siku ya tukio, hausigeli huyo aliyekuwa na siku mbili tangu aanze kazi aling’ang’ania kutumwa sokoni saa mbili asubuhi ambapo alimkubalia na kumuagiza mboga.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni