Habari

Jumapili, 17 Novemba 2013

100 wauawa katika mapigano ya kikabila Sudan

Watu 100 wameuawa katika mapigano ya kikabila katika eneo la Darfur Magharibi mwa Sudan.
Kwa mujibu wa Radio Omdurman ya nchini Sudan, watu hao wakiwemo askari wa nchi jirani ya Chad wamepoteza maisha katika mapigano baina ya makabila ya Misseriya na Salamat.

Makabila hayo hasimu yamekuwa yakipigana kwa miaka kadhaa sasa. Imearifiwa kuwa mapigano yalishadidi Jumamosi katika eneo la Umm Dukhun karibu na mpaka wa Chad ambapo wapiganaji wa pande zote mbili waliuawa.

Kairbu watu 200 wamepoteza maisha katika mapigano baina ya makundi hayo tokea mwezi Aprili mwaka huu. Umoja wa Mataifa unasema mapigano ya kikabila Darfur yamepelekea watu karibu nusu milioni kuwa wakimbizi mwaka huu. 
Waziri wa Ulinzi Sudan Abdelrahim Mohammad Hussein amesema mapigano ya kikabila Darfur sasa ni tishio zaidi ya hata harakati za waasi. Wakuu wa kikosi cha pamoja cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika na Umoka wa Mataifa Darfur (UNAMID) wameelezea wasi wasi wao kuhusu mapigano baina ya makabila ya ya Misseriya, Taisa na Salamat huko Darfur.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni