China imebainisha kusikitishwa kwake kufuatia kushindwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuahirisha kesi ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC dhidi ya viongozi wa Kenya.
Balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Liu Jieyi amesema hatua ya kuahirisha kesi dhidi ya viongozi wa Kenya ambayo pia inaungwa mkono na nchi za Afrika ililenga kudumisha amani na utulivu wa barani Afrika.
Kwenye upigaji kura, nchi saba wajumbe wa baraza hilo zikiwemo Russia na China zilipiga kura ya kuunga mkono mswada huo huku nchi nane wajumbe zikiwemo Uingereza, Ufaransa na Marekani zikipinga mswada huo.
Bw Liu alipongeza Kenya kwa kusimama kwenye mstari wa mbele katika vita dhidi ya ugaidi na mchango wake katika kudumisha amani na usalama katika kanda ya Afrika mashariki.
Umoja wa Afrika ulikuwa unataka kesi za Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na naibu wake William Ruto katika ICC ziahirishwe.
Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Bi. Amina Mohammad amekosoa uamuzi uliotolewa na Baraza la Uslama kuhusu ombi la Umoja wa Afrika. Amesema muundo wa hivi sa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni