Akitoa hukumu hiyo Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Hai, Dennis Mpelembwa alisema mahakama hiyo haina budi kutoa hukumu kali pamoja na mtuhumiwa kukubali kosa alilotenda na kuirahisishia mahakama hukumu hiyo.
Hata hivyo kabla ya hakimu kutoa hukumu hiyo, Mwendesha Mashtaka Mkaguzi msaidizi wa Polisi, Roymax Membe alisoma maelezo ya mshtakiwa kuwa Novemba 5, mwaka huu saa 11 jioni huko Koboko Kusini Sanya Juu wilayani Siha, mshtakiwa alimbaka mtoto wa miaka 3 kwa kumuingilia kimwili na kumsababishia maumivu makali.
Membe alisema, siku hiyo ya tukio mshtakiwa alimrubuni mama aliyeachiwa mtoto huyo, mama Ombeni akidai kuwa ametumwa na mzazi wa mtoto huyo. Mama huyo alimruhusu mtuhumiwa kwenda na mtoto huyo akidhani anampeleka kwa mama yake mzazi.
Hata hivyo mtuhumiwa aliondoka na mtoto huyo na kumpeleka mahali karibu na nyumbani kwao na kumfanyia unyama huo.
Alisema mara baada ya mtuhumiwa kuwaona wapita njia, alitimua mbio ili kujinusuru lakini walimfukuza na kumtia mikononi na kumpeleka katika Kituo cha Polisi cha Sanya Juu.
Mtoto huyo, alipelekwa Hospitali ya Kibong’oto na kupimwa ambapo alipatikana na mbegu za kiume katika sehemu zake za siri na kuharibiwa vibaya kulikolazimu kushonwa nyuzi saba.
Mwendesha mashtaka aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa kutoa haki kwa mtoto huyo ambaye ameteswa kisaikonolojia na maisha yake ya baadaye.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni