Shaibu Hassan Kaduara akizungumza na waandishi wa habari,huko katika chuo cha uandishi wa habari cha TSJ,Chake Chake Pemba.
NA Is-haka Mohammed,PEMBA.
Familia ya Bw. Hassan Kaduara ya Kisiwani Pemba imesema itakwenda
kufungua kesi mahakamani endapo serikali haitampeleka yeye mahakamani kutokana kumzungumza
ndani ya baraza la wawakilishi ilihali yeye akiwa sio mjumbe wa baraza hilo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari huko Chake Chake Shaibu Hassan
Kaduara amesema kauli iliyotolewa katika
ukumbi wa baraza la wawakilishi na Waziri wa Katiba na Sheria Abuubakar Khamis
Bakari ya kuwa aliibia serikali shilingi milioni mbili na kujiuzia gari la
shirika la Umeme kwa bei aliyotaka mwenyewe bila ya kufuata taratibu.
Alisema lengo la Kuiomba serikali kumpeleka mahakamani ni kutaka
kuonesha ukweli kwa jamii kwa vile
mahakamaniukweli utajulikana na
anayepashwa kuchukuliwa hatua zinazofaa atabainika huko badala ya kusema katika
baraza la wawakilishi kwa kujifurahisha wenyewe.
Kaduara ambaye alikuwa mtumishi wa Shirika la Umeme ZECO
Pemba kabla ya kuhamishiwa Wizara ya Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati kwa
kudaiwa kutoa siri za ufisadi katika shirika hilo Pemba,alisema ifikapo wiki
mbili kama serikali haijamfikisha yeye mahakamani atakwenda kufungua kesi
kuishitaki serikali kwa kutumia chombo cha umma kumzulia uongo
mbele ya jamii.
Alisema kauli iliyotolewa na waziri wa Sheria la Katibu wa Zanzibar
Abuu bakar Khamis Bakar haikuwa na
ukweli wowote zaidi ya kumzalilisha yeye na famlia yake,ambayo amedai kuwa ina
heshima kubwa kwa serikali na jamiii.
“Gari mimi nilinunua kwenye mnada wa hadhara wa serikali na
kushindana na watu wengine mbali wakiwemo wafanyakazi wenzangu wa zeco,nah ii hapa nisiti ya mpiga mnada wa
serikali hii hapa ni namba 05 ya tarehe 18-12-2011,yenye maelezo ya kununua
gari aina ya defender”Alionyesha risiti hiyo Kaduara.
Aidha Kaduara pia aliotoa risiti ya shirika la umeme mbele ya
waandishi wa habari akishuhudisha kuwa gari hilo aliuziwa kihalali na shikala
la Umeme Pemba kupitia mnada ambapo risiti ya shirika ililikuwa na namba 22025
ambayo ilitolewa tarehe 25/12/2011 na Habibu Moh’d Ali.
Aidha alipinga vikali kauli ya kuwa yeye wakati huo alikuwa afisa
utawala wa ZECO Pemba hazina ukweli,kwa vile aliyekuwa afisa utawala kipindi
hicho ni Hafidh Tahir Silima,ambaye alipewa nafasi hiyo tarehe 19/10/2011.
“Barua hii ndiyo inayothibitisha kuwa mimi katika kipindi hicho
sikuwa afisa utawala kwa barua hii yenye namba ZECO/PF/H.78.19/10/2011,
iliyoandikwa meneja wa ZECO Pemba Salum Massoud kwa niaba ya Meneja Mkuu wa
ZECO Zanzibar”alifafanua Kaduara.
Aidha Kaduara alisema kuwa lengo la kufika la kuzungumza na
waandishi wa habari ni kutaka kuonyesha ubinafsi uliopo kwa baadhi ya viongozi
wa Umma wa kuwalinda jamaa zao na kuwakandamiza wengine.
“Huyu ndugu Hafidhi Twahir Silima ambaye ndiye aliyekuwa afisa
utawala kipindi hicho kila mtu anajua ana mahusiano gani na M.h Abuubakar,huyu ni mkwe wake M.h
Abuubakar amemuodhesha mwanawe mzazi,hivyo kutokana na kutaka kumlinda mkwewe
aliona kuwadhalilisha webgine”
Akizungumzia suala la kuitwa mwizi na M.h Abuubakar ya kuliibia
shirika milioni mbili 2 katika Chombo cha Umma,alisema ni kutaka kumlinda
mkwewe ambaye ndiye alkiyekuwa afisa uhusiano kipindi hicho na kuidhalilisha
familia yake.
Alisema kutokana na tuhuma hizo zilizotolewa ndani ya baraza na
Waziri wa katiba na sheria limemsononesha na kuitaka kumpeleka mahakamani,ili
Abuubakar akatoe ushahidi mahakamani.
“Na mimi kwa hili naiomba serikali inipeleke mahakamani na nipo
tayari kuchukuliwa hatua zozote zile ikiwemo kufukuzwa kazi endapo nitabainika
na kosa,na serikali ikishindwa kunipekeleka mahakamani baada ya wiki mbili
nitakwenda mimi kufungua kesi ya kudhalilishwa na serikali ndani ya chombo cha
Umma”alisisitiza Kaduara.
Aidha kaduara alisema kuwa baadhi ya viongozi wamekuwa
wakimwandama kwa ajili ya kuwalinda jamaa zao na kumzamisha yeye kutokana na
kutoa mashirikiano kwa kamati ya baraza la wawakilishi ya kuchunguza ubadhirifu
katika shirika la Umeme Zanzibar ZECO ilipofika katika shirika hilo.
Alisema kuwa yeye kama mfanyakazi wa ZECO na raia mwema wa
Tanzania alitakiwa kutoa ushirikiano kwa kamati ya PSI na kusema kuwa alianza kubaini
ubadhirifu kutoka katika magazeti ya Nipe Habari ambayo aliwaonyesha waandishi
wa habari katika mkutano huo.
Alisema kutajwa yeye katika baraza la wawakilishi na baadhi ya
viongozi na ubaya wa wanasiasa wanaojali maslahi yao binafsi badala ya kuwajali
wananchi, ndipo walipoona kuchukua fursa hiyo kuwadhalilisha wengine.
Hata hivyo alipoulizwa kuhusu kuhamishwa kwake kutoka ZECO
kupelekwa Wizara ya Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati kunatokana na ushikiano
alioutoa kwa kamati ya PSI pamoja na kutoa taarifa mbele ya rais mwaka mwanzoni
mwa mwaka huu,Kaduara amesema kuwa hawezi kujua.
“Mimi kwa vile ni mtumishi wa serikali siwezi kuzungumzia kuhusu suala
la ZECO kiundani kwa sasa kwa vile yeye ni mtumishi wa umma kwa vile hizo ni
sheria za kazi kuhamishiwa kutoka seheme moja kwenda nyengine,leo zaidi
nazungumzia suala la kifamilia”
Shaibu Hassan Kaduara aliwahi kutoa taarifa za ubadhirifu wa
shirika la Umeme Pemba mbele ya Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein alipokuwa
akipokea taarifa ya Mkoa wa Kusini Pemba katika viwanja vya Tenis Chake Chake
mwanzoni mwa mwaka huu.
“Mh. Rais katika
shirika la umeme kuna ubadhirifu mkubwa hivi na tayari tumeshapeleka kwa
uongozi wa juu lakini hakuna hatua zilizochukuliwa,hivyo naomba nichukue nafasi
hii kuyaeleza,kwanza ni ajira zisizodhingatia sifa katika shirika la umeme
Pemba”
Mwisho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni