Muungano unaoongozwa na chama cha udugu wa Kiiislamu hapo jana umeitisha mazungumzo ya kumaliza mgogoro wa kisiasa ulioikumba Misri tangu jeshi la nchi hiyo lilipomuondoa madarakani Rais Mohammed Mursi mnamo July 3 mwaka huu.
Awali Muungano huo wa kitaifa ulipanga maandamano tangu Mursi alipooondolewa madarakani na kuapa kuendelea na maandamano hayo hadi pale rais huyo atakaporejeshwa madarani.
Hata hivyo serikali ilianzisha msako mkubwa wa wale wanaofuata itikadi kali za kidini na kuvunja nguvu ya muungano huo kupanga maandamano makubwa zaidi.
Takriban watu 1000 wameuwawa Misri tangu kuondolewa kwa Mohammed Mursi.
Jeshi la nchi hiyo limesema limejibu matakwa ya wananchi kwa kumuondoa madarakani rais aliyekuwa amechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia.
Kwa sasa Mursi anakabiliwa na makosa ya kuchochea mauaji ya waandamanaji wanaopinga serikali hiyo ya vyama vya kiislamu wakati alipokuwa madarakani. Kesi yake itasikilizwa January 8 mwakani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni