Habari

Jumatano, 10 Desemba 2025

MCHANGO WA DINI KWA MAENDELEO YA JAMII

Na Is haka Mohamed Rubea, Pemba.
MCHANGO wa dini katika masuala mbali mbali ni muhimu katika kufanikisha lengo ya jambo lolote lile ambapo limepangwa kufanyika kwa mafanikio na kupelekea mageuzi.

Tumekuwa tukishughudia dini zikitumika kwenye masuala mengi ya kijamii, yale ya kitaifa na wakati mwengine hata suala la mtu binafsi.
Mtanzamaji katika Makala hii tunaangalia mchango wa dini katika kuimarisha usawa wa kijinsia hapa Zanzibar, hususani kisiwani Pemba.
Inatambulika kuwa kuna miongozo mbali mbali ya kidini juu ya usawa wa kijinsia na nafasi ya kila jinsia ukiondosha ule utofauti wa kimaumbile, na miongozo itokanayo na mafundisho kama mirathi kwa uislamu hata dini nyengine,
Hapa nchini Tanzania tumeshughudia nguvu hizo za kiimani zikitomika katika kutafuta njia bora ya kuliweka jambo mahala pake, ikikumbukwa kuwa dini ni zenye wafuasi na waumini ambao wanazifuata na miongozo yake.
Masalan ni pale panapotokea suala la ugonjwa kwenye jamii dini hutumiwa hata na mamlaka kuweza kuhamasisha jamii juu ya kutoa uelewa wa kujikinga na kukinga wengine na magojwa ili yasiweze kutambaa zaidi.
Lakini inaonekana bado mchango wa dini haujakuwa mkubwa sana katika kuona usawa wa kijinsia unaimarika kwa kiasikile kilichotarajiwa.
Taasisi za Pemba Community Forest, Internation Community Forest na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Zanzibar Tamwa kupitia Mradi wa Wanawake na Uongozi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kuunga mkono wanawake katika kilimo msitu.
Kwa upande wa dini kiislamu mwanamke ana hadhi na cheo kikubwa kilicho taadhimu ambapo mwanamke wa Kiislamu ni mwalimu wa kwanza katika kujenga jamii.
Siri ya umuhimu wa mwanamke imetanda katika kazi yake nzito na mamlaka yaliyokwa juu yake, shida shida ambazo anabeba mabegani mwake, mamlaka na dhiki ambazo hata mwanamme hawezi kuzibeba nan do maana tukaambiwa tuwapende na kuwaheshimu sana mama zote.
“Tumemuusia insanikwa wazazi wake wawili, mama yake amebeba mimba yake  kwa udhaifu juu ya udhaifu na kumwachisha ziwa katika miaka katika miaka miwiliya kwamba unishukuru mimi, na wazazi wake, kwangu ndio pahali pa kuishia’ (Lukman: 14)
Tukiangalia Biblia, Mwanzi 1:27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, Kwa mafano wa Mungu alimwumba mwanamke na mwanamke aliwaumba,sikiliza pahali popote pale mwanamke ni mtu mwenye nguvu na ushawishi mkubwa katika kufanya jambo kuliko hata mwanamme, Ikiwa ushawishi huu utatumiwa kwa mpango wa Mungu basi kusudi litatekelezwa.
Miongozo ya dini imeweka wazi kuwa mwanamke anayo nafasi kubwa katika jamii kufanya mambo mengi na yaliyo makubwa, lakini inaoneka wazi kuwa bado miongozo ya dini haitapewa nafasi yake kisawa sawa kwa mwanamke.
Ufafanuzi kwa mtindo wa kihabari
Miongozo ya dini, Imeeleza wazi kuwa mwanamke ni mshiriki muhimu katika ujenzi wa familia na jamii. Ana haki ya kushiriki katika elimu, biashara, na hata uongozi wa kijamii.

Changamoto ya utekelezaji, Pamoja na maandiko na mafundisho ya dini kuhimiza usawa, bado kuna tafsiri finyu na mitazamo ya kijamii inayomnyima mwanamke nafasi ya kuonyesha uwezo wake.
Matokeo ya kijamii,Mwanamke anapopewa nafasi yake ipasavyo, jamii hunufaika kwa kupata nguvu kazi yenye ufanisi, mawazo mapya na uongozi wa kiadilifu. Kinyume chake, kumnyima nafasi ni kuikosesha jamii mchango muhimu.

Wito wa mabadiliko, Wataalamu wa dini na viongozi wa kijamii wanahimizwa kusoma upya miongozo ya dini kwa mtazamo wa kina na wa kisasa, ili kuhakikisha mwanamke anapata nafasi yake sawasawa kama ilivyoelekezwa.
WANAWAKE WASEMAJE.
Miongozo ya dini tunashindwa kuielewa ndio mana tunakosa haki zetu,natamanai wadau waendelee kuelimisha jamii hususan ni kisiwani Pemba ,huku vijijini ndio uozo umezidi haki nyingi tunazikosa.Alisema Fatma Hamad ali mkaazi wa Kambini kichokochwe ambae pia ni mkulima wa kilimo mseto
Hitimisho

suala hili ni habari yenye uzito wa kijamii, dini imetoa mwongozo wa wazi, lakini utekelezaji wake bado unakwamishwa na mitazamo ya kijamii. Mwanamke anapewa nafasi kubwa kwa maandiko, lakini kwa vitendo nafasi hiyo mara nyingi hubaki kufungwa na mila na tafsiri zisizo sahihi.

ZANZ ADAPT ILIVYOBADILISHA MATUMIZI YA MITANDAO NA KUWA FURSA KWA BIKOMBO FAKI

.
Na  Is haka Mohamed Rubea.
    KATIKA kijiji cha Kiuyu Minungwini, Pemba wilaya Wete , ndiko maisha halisi anayoishi anaishi Bikombo Faki Ali, mwanamke jasiri, mkulima wa kilimo mseto, mfanyabiashara mdogo na mwanaharakati wa masuala mbali mbali ya kijamii. 
Safari yake ya maisha imekuwa kielelezo cha mfano wa kuigwa  na  mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi  wanawake na uongozi, ZANZ ADAPT  unaotekelezwa na  Jumuia ya uhifadhi wa misitu Pemba C FP, Jumuia ya uhifadhi wa misitu kimataifa CFI, na TAMWA  ZNZ unaofadhiliwa na Canada Global Affairs, ulivyoweza kubadilisha  maisha katika kilimo , siasa za kijamii na kiuchumi kwa wanawake vijijini. 
Mradi huu, kwa kushirikiana na Community Forests Pemba na Community Forests International, umefungua milango mipya ya fursa kwa wanawake  akiwemo Bikombo, hususan katika matumizi ya mitandao ya kijamii kama WhatsApp na Facebook.
MWANZO WA SAFARI
Bikombo Faki Ali alikulia katika mazingira ya kijijini ambapo kilimo ndicho uti wa mgongo wa familia nyingi Ikiwemo familia yake yenye jumla ya watoto nane  na baba wa familia hiyo. Akiwa mkulima wa kilimo aliebadilisha maisha yake ya kilimo kutoka kilimo cha mazoea alichokuwa akilima hadi kulima kilimo  mseto,mara baada ya kupata fursa ya kushiriki mafunzo yamradi huo wa ZANZ ADAPT  alijikita katika mazao ya chakula miti ya matunda huku nje ya kilimo anaendelea na  biashara ndogo ndogo ili kuendesha maisha ya familia yake.
 Bikombo Alitamani kushiriki katika uongozi wa kijamii na kisiasa, akiamini kwamba sauti ya mwanamke ni muhimu katika maamuzi ya maendeleo ya jamii.
Mnamo septembe Mwaka huu  2025, Bikombo alijaribu kugombea nafasi ya udiwani katika wadi yake ya Kiuyu, kupitia CCM Ingawa hakufanikiwa kushinda,wala kupita katika hatua zake za awali  hatua yake ilibaki kuwa alama ya ujasiri na uthubutu wa mwanamke kijijini kuingia katika ulingo wa siasa. Changamoto alizokutana nazo zilimfundisha kuwa siasa si rahisi, hasa kwa wanawake wanaotoka vijijini, lakini pia zilimpa msukumo wa kutafuta njia mpya za kushirikiana na jamii yake.
MAFUNZO YA TAMWA ZANZIBAR
Mabadiliko makubwa yalikuja baada ya Bikombo kushiriki mafunzo yaliyotolewa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Zanzibar, huko Mkanjuni  Chake chake Kupitia mradi wa Zanz Adapt, alijifunza kuhusu uongozi, usawa wa kijinsia, na namna ya kutumia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari, kama nyenzo ya kuelimisha na kushirikisha jamii,kujifunza kutafuta elimu kutoka kwa wengine jambo ambalo awali halikuwa katika akili yake kutumia mitandao ya kijamii .
 Mafunzo haya yalikuwa na lengo la kuwajengea wanawake uwezo wa kushiriki kikamilifu katika uongozi na kupaza sauti zao katika masuala ya kijamii na kisiasa na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Kwa Bikombo, mafunzo haya yalikuwa kama mwanga mpya, alianza kutumia mitandao ya kijamii  kujifunza ,na kuiga manendeleo ya wakulima na wafanya biashara wanawake walioko nje ya  Tanzania na akiamini kuwa mitandao ya kijamii siyo tu mahali pa mawasiliano ya kijamii, bali ni jukwaa lenye nguvu la kuhamasisha, kuelimisha na kushirikisha jamii katika mijadala ya maendeleo. 
WhatsApp na Facebook, ambazo awali alizitumia kwa mawasiliano ya kifamilia na biashara ndogo ndogo, sasa zikawa nyenzo za harakati na uongozi.

MITANDAO YA KIJAMII KAMA FURSA
Baada ya mafunzo, Bikombo alianza kutumia WhatsApp na Facebook kwa njia mpya, Aliunda vikundi vya WhatsApp vya wakulima na wanawake wajasiriamali wadogo, ambapo walijadiliana kuhusu changamoto za kilimo, masoko ya bidhaa, na mbinu za kuongeza kipato. Kupitia Facebook, alishiriki simulizi za maisha ya wanawake wa Kiuyu, akihamasisha jamii kuhusu umuhimu wa usawa wa kijinsia na nafasi ya mwanamke katika uongozi.
Ambapo  kwa mtandao wa kijamii wa facebook anajulikana kama KIUYU JITENGE.
Mitandao hii ilimsaidia kuunganisha wanawake wenzake na wadau wa maendeleo,Aliweza kufikisha ujumbe wake kwa haraka na kwa uwazi, na kwa mara ya kwanza alihisi kuwa sauti yake inasikika zaidi ya mipaka ya kijiji chake.
 Hii ilikuwa hatua kubwa ya kuondoa vikwazo vya kijamii vilivyokuwa vinawazuia wanawake kushiriki kikamilifu katika mijadala ya maendeleo.

Mwanamke Mkulima, Mfanyabiashara na Mwanaharakati
Mbali na siasa, Bikombo aliendelea na shughuli zake za kilimo mseto. Alilima mazao mbalimbali kwa ajili ya chakula na biashara, akitumia mitandao ya kijamii kutafuta masoko mapya. Kupitia WhatsApp, aliweza kuwasiliana na wateja na wauzaji wa pembejeo, jambo lililomsaidia kupunguza gharama na kuongeza faida.

Aidha, kama mfanyabiashara mdogo, alitumia Facebook kutangaza bidhaa zake, kuanzia mazao ya shambani hadi bidhaa ndogo ndogo alizokuwa akiuza sokoni. Hii ilimsaidia kupanua wigo wa biashara yake na kujenga mtandao wa wateja wapya. Mitandao ya kijamii ikawa daraja la kumtoa kijijini na kumfikisha sokoni kwa urahisi.
CHANGAMOTO NA MAFANIKIO
Safari ya Bikombo haikuwa rahisi. Alikumbana na changamoto za kijamii, ikiwemo mitazamo ya baadhi ya watu waliodhani kwamba mwanamke hawezi kushiriki kikamilifu katika siasa au uongozi. 
Pia, alikabiliana na changamoto za kiuchumi na ukosefu wa rasilimali za kutosha kuendesha kampeni zake za kisiasa. Hata hivyo, kupitia mafunzo na msaada wa mradi wa Zanz Adapt, alijifunza mbinu za kushinda changamoto hizi.

Mafanikio yake yalionekana katika namna alivyoweza kuhamasisha wanawake wenzake kushiriki katika mijadala ya kijamii na kisiasa. Ingawa hakushinda nafasi ya udiwani, alibaki kuwa kiongozi wa kijamii, akihamasisha na kuelimisha jamii kupitia mitandao ya kijamii. Alikuwa mfano wa kuigwa kwa wanawake wengine wa Kiuyu na Pemba kwa ujumla.

ATHARI ZA MRADI
Mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya wanawake na uongozi umeleta mabadiliko makubwa kwa wanawake vijijini. Kwa Bikombo, mradi huu umemsaidia kubadilisha mtazamo wake wa maisha na kumpa ujasiri wa kushiriki kikamilifu katika uongozi na maendeleo ya jamii. Kupitia mitandao ya kijamii, amekuwa daraja la kuunganisha wanawake na wadau wa maendeleo, na sauti yake imekuwa ikisikika zaidi ya mipaka ya kijiji chake.
Kwa sasa Bikombo anaendelea kusubiri ,mafanikio makubwa katika kilimo mseto ambacho alianza hivi karibuni  mara baada ya kuzinduliwa kulima kilimo kinachokabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi na programu hiyo ya zanz adapt.
mwisho

Hitimisho
Simulizi ya Bikombo Faki Ali ni ushuhuda wa nguvu ya elimu, mafunzo na teknolojia katika kubadilisha maisha ya wanawake vijijini. Kutoka kuwa mkulima wa kilimo mseto na mfanyabiashara mdogo, amekuwa mwanaharakati na kiongozi wa kijamii anayehamasisha wanawake kushiriki kikamilifu katika uongozi. Mitandao ya kijamii, hususan WhatsApp na Facebook, imekuwa nyenzo muhimu ya kufanikisha harakati zake.

Ingawa hakufanikiwa kushinda nafasi ya udiwani, Bikombo amefanikiwa kushinda mioyo ya wanawake na jamii yake kwa ujumla. Ameonyesha kwamba uongozi si lazima uwe na vyeo, bali ni uwezo wa kuhamasisha na kuleta mabadiliko chanya katika jamii. Mradi wa Zanz Adapt, kwa msaada wa TAMWA Zanzibar na wadau wake, umeandika historia mpya ya wanawake vijijini kama Bikombo, historia ya ujasiri, uthubutu na matumaini ya kesho iliyo bora zaidi.

Bikombo  Faki Ali  anaejivunia kujengewa uwezo wa kuvitumia vyombo vya Habari  ,waandishi  na mitandao ya kijamii kwa Matumizi Sahihi  ili kuendeleza harakati zake anazozifanya za kupambana na athari za mabadiliko ya  ambae  anaamini  ndio fursa pekee iliyobaki kwakwe kujikomboa na shughulo zake bila woga.



MAFUNDISHO YA KIDINI,KWA USAWA WA KIJINSIA NA UDHIBITI WA RASILIMALI.



Na,Is haka Mohamed Rubea .

KATIKA   jamii nyingi  Tanzania  , dini imekuwa na nafasi kubwa katika kuunda maadili, mila na desturi. 
Huku mafundisho ya kidini mara nyingi yakiendelea kutumika kama mwongozo wa maisha ya kila siku, na huathiri namna watu wanavyohusiana, kushirikiana na kugawana rasilimali. 
Hata hivyo, changamoto kubwa imekuwa jinsi mafundisho haya yanavyoweza kuendana na dhana ya kisasa ya usawa wa kijinsia, hasa katika mila na desturi za kijamii, pamoja na udhibiti wa rasilimali.
Mafundisho ya Kidini ndio hutoa miongozo na Maadili ya Jamii ,Dini nyingi, ikiwemo Uislamu, , hufundisha kuhusu haki, heshima na mshikamano wa kijamii,Mafundisho haya mara nyingi yanasisitiza umuhimu wa upendo, mshikamano na usawa mbele ya Mungu.

Hata hivyo, tafsiri za mafundisho ya kidini hutofautiana kulingana na jamii na wakati, na mara nyingine hutumika kuhalalisha mfumo wa kijamii unaoweka  jinsia moja juu ya nyingine.

Mafundisho hayo y a dini na husaidia usawa wa kijinsia katika mila na desturi za kijamii, pamoja na udhibiti wa rasilimali.”
Usawa wa Kijinsia katika Mila na Desturi,Mila na desturi za kijamii mara nyingi huakisi historia na utamaduni wa jamii husika.

Katika baadhi ya jamii, wanawake wamekuwa wakipewa nafasi ndogo katika maamuzi ya kifamilia na kijamii.
Hali hii imekuwa ikipingwa na harakati za kijamii na kisiasa zinazosisitiza usawa wa kijinsia, ambapo wanawake na wanaume wanapaswa kushiriki kwa usawa katika maamuzi na fursa za maisha.

Amina Ahmed  Mohd  ni Kaimu mratibu Chama cha waandishi wa habari wanawake TANZANIA ,TAMWA ZANZIBAR,ambayo ni miongoni mwa taasisi isyoya kiserikali inayoendelea kutetea na kusimamia haki za wanawake ili kufikia usawa wa kijinsia yey anasema kuwa ‘’ mila desturi na tamaduni zilizojengeka katika baadhi ya maeneo ndani ya jamii ,yamekuwa sababu ya kurudisha nyuma harakati hizo za kufikia usawa wa kijinsia hususan katika maswala ya umiliki wa rasilimali ikiwemo ardhi

‘’ Bado kuna changamoto kubwa Katika jamii kuhusu maswala ya umiliki wa rasilimali na usawa wa kijinsia ,ikiwemo ardhi kwa wanawake kwa usawa , huku wengine wakiona suala hilo ni kwamujibu wa dini jambo ambalo dini limeweka miongozo na maelekzo ya kufuata iwapo ’’ 
‘’Katika hili sisi kama taasisi tunaendelea kutoa elimu kupitia vyombo vya habari ili jamii izidi kuelimika na kuweza kuufikia usawa wa kijinsia katika kumiliki rasilimali’’alimaliza

MIONGOZO YA DINI 
Mafundisho ya kidini, yanapotafsiriwa kwa mtazamo wa haki na usawa, yanaweza kuwa chachu ya kuondoa Kutokuwepo kwa usawa wa kijinsia  na kuimarisha mshikamano wa kijami,kwa mitazamo 
Katika Qur’an, Mwenyezi Mungu anasema katika Sura An-Nisai (4:32) Mwenyezimungu anasema,“Wanaume watapata sehemu ya walichokichuma, na wanawake watapata sehemu ya walichokichuma”.

Aya hii inaweka msingi wa kisheria wa kidini kwamba kila mtu ana haki ya kumiliki mali bila ubaguzi wa kijinsia .

Huku miongozo hiyo hiyo ya dini kwa upande wa dini ya kikiristo  katika Biblia (Mithali 31:16), mwanamke jasiri anatajwa kuwa “hununua shamba kwa matunda ya kazi yake,” ikionesha wazi kuwa umiliki wa ardhi ni haki halali ya wanawake wa dini ya  Kikristo.

WANAWAKE 

Bikombo  Faki  Khamis ,ni mama wa watoto 8 Mkaazi wa Kiuyu minungwini wilaya ya wete Mkoa wa kaskazini Pemba ,mkulima alibadili mfumo na utaratibu wake wa kulima kilimo cha mazoea na kuanza kulima kilimo  kinachoendana na hali ya hewa na kinachohimili mabadiliko ya tabia ya nchi ,akiwa moja  kati ya wanufaika wa mradi wa ZANZ ADAPT  unaotekelezwa  na  Jumuia ya uhufadhi wa misitu Pemba CFP,jumuia ya uhifadhi wa mistu kimataifa  CFI ,NA  chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania  Zanzibar TAMWA  KWA UFADHILI WA CANADA  GLOBAL AFFAIR  katika suala hili la usawa wa kijinsia katika suala hili la usawa wa kijinsia na udhibiti wa rasilimali anaeleza kuwa
‘’ Mwazoni nilipoanza kulima kilimo hichi ambacho ni mchanganyiko ,mume wangu aliniambia sina kazi  kiufupi alinibeza ,lakini kwa sasa nashukuru ananisaidia   tunafanya kazi hii kwa pamoja pale ambapo nakwama katika kilimo ananisaidia ’’.
Natumia kilimo  hicho katika ardhi yao ya familia lakini yeye anaisimamia kuhakikisha Napata haki yangu juu ya nguvu zangu zote ninazoendlea kutumia, alinifyekea yey pori na mengine mengi anakubali nimshirikishe kila hatua kwangu ni mafanikio kwa vile awali alikuwa hana utayari’’

Katika jamii pia mashirikiano Napata ,na mumewangu ananiunga mkono Zaidi ,niligombea udiwani wa wadi yangu ,ingawa sikubahatika kuingia katika mchakato lakini alionesha mashirikiano makubwa na kunisapoti,Kwenye biashara pia tunasaidiana’’ alimaliza Bikombo 
Fatma Shaaban  ni mnufaika mwengine mradi wa Zanz ADAPT  anasema kuwa  Udhibiti wa Rasilimali, Rasilimali ni pamoja na ardhi, mali, elimu na hata nafasi za uongozi,kwakwe umekuwa na msaada mkubwa kutoka kwa mume wake ambae amekuwa mshauri, msaidizi na msimamizi wa maendeleo yake  katika kilimo anachoendelea kulima  huku akiamini kuwa rasilimali zinazozalishwa katika shamba hilo  ni faida yake na watoto wake hapo baadae.

Katika jamii nyingi, udhibiti wa rasilimali umekuwa ukiegemea zaidi kwa wanaume, huku wanawake wakiachwa nyuma.
Hali hii imekuwa ikisababisha pengo kubwa la kiuchumi na kijamii kati ya wanaume na wanawake.

Mafundisho ya kidini yanaposisitiza haki na usawa, yanaweza kutumika kama msingi wa kugawanya rasilimali kwa njia ya haki, bila kujali jinsia kama hapa MR Robert Migue  Kiongozi wa dini ya kikiristo lakini pia mwanaharakati maswala ya wanawake kutoka vitongoji  anavyosema 
‘’Usawa wa kijinsia katika umiliki wa rasilimali ni suala ambalo limewekewa mipaka yake kisheria  ni vyema ikafuatwa ili kuona hatuwaachi nyuma wanawake ‘’

Wapo baadhi ya viongozi wamekuwa wakipotosha bila kufafanua ipasavyo wakiona kuwa  wanaona usawa wa kijinsia kama tishio kwa mila na desturi za jadi wakiacha kutoa miongozo ya dini na maelekezo yake yanavyosema .
WANAJAMII .

Uelewa mdogo wa jamii kuhusu tafsiri pana ya mafundisho ya kidini inayosisitiza haki na usawa,Bado baadhi ya watu katika jamii wanashindwa kutofautisha dini ,mila na desturi katika maswala haya  ,tunaomba elimu izidi kutolewa ili mwisho wa siklu rasilimali za wanawake ziweze kumilikiwa na wao wenyewe alisema Riziki Khamis hamad  kaazi wa  Kiuyu .

Mfumo wa kisheria na kiutawala ambao mara nyingine haujengi  mazingira ya usawa wa kijinsia katika udhibiti wa rasilimali,unapelekea kuwaona wanawake hususan ni huku vijijini waonekane kama hwastahiki kuwa na haki katika rasilimali ndio mana waliowengi wamezisabilia’’alisema Khamis Abass Khamis  mkaazi wa minungwini.

MAONI 

Katika baadhi ya nchi za Kiafrika, mafundisho ya kidini yametumika kuhamasisha elimu kwa wasichana, jambo ambalo limeongeza usawa wa kijinsia katika sekta ya elimu.

Mashirika ya kidini yamekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha wanawake kushiriki katika uongozi wa kijamii na kisiasa.

Jumuiya za kidini pia zimekuwa zikihamasisha mshikamano wa kijamii kwa kusisitiza kwamba rasilimali ni zawadi yakila mtu  na zinapaswa kugawanywa kwa usawa.

Wadau maswala ya wanawake na usawa wa kijinsia wanaendelea kusiadia kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa usawa katika umiliki wa rasilimali na usawa wa kijinsia ndio njia pekee itakayosaidia kumkomboa mwanamke  na aweze kuwa huru bila utegemezi.

Hitimisho Mafundisho ya kidini, yanapochukuliwa kwa mtazamo wa haki na usawa, yanaweza kuwa chachu ya mabadiliko makubwa katika jamii. 

Kusaidia usawa wa kijinsia katika mila na desturi za kijamii, pamoja na udhibiti wa rasilimali, si tu suala la kisiasa au kijamii bali pia ni suala la kiimani. Jamii inayojengwa juu ya misingi ya usawa na haki ni jamii yenye mshikamano, maendeleo na amani.
MWISHO

Jumanne, 9 Desemba 2025

NAFASI YA WANAWAKE NA MCHANGO WA MAENDELEO KATIKA JAMII.

NA IS HAKA  MOHAMED  RUBEA

WANAWAKE  wamekuwa nguzo muhimu katika jamii kwa karne nyingi. Kauli kwamba “Wajibu wa wanawake unatambuliwa kuwa muhimu katika kazi za jamii na maendeleo ya kijamii zinaendelea kusikika hata kwa viongozi wa juu wa nchi na inabeba uzito mkubwa, kwani inatambua mchango wa wanawake si tu katika familia bali pia katika nyanja za kijamii, kiuchumi uongozi na kisiasa.
 Katika makala hii, tutachambua wajibu wa wanawake kwa kina, tukitoa mifano hai kutoka Tanzania na ulimwengu kwa ujumla, ili kuonyesha namna mchango wao unavyoendeleza jamii na kuchochea maendeleo endelevu. 
 MIFANO YA KUIGWA NA JAMII. 
 Tukianza wajibu wa Wanawake kama Msingi wa Familia,Familia ni kitovu cha jamii, na mara nyingi wanawake ndio wanaobeba jukumu la kuhakikisha familia inakuwa na malezi bora. 
 Malezi ya watoto, Mwanamke ndiye mwalimu wa kwanza wa mtoto, Kupitia malezi yake, mtoto hujifunza maadili, lugha na utamaduni. Vijiji vya Pemba na Tanzania kwa ujumla, mama hutumia muda mwingi kuwafundisha watoto wake kusoma Qur’an, kuimba nyimbo za kitamaduni, na kuwafundisha stadi za maisha kama kupika na kushona,kulima kulinda mila na tamaduni ,ikiwa kama sehemu ya urithi wa kijamii unaoendelezwa kizazi hadi kizazi. Mchango wa Wanawake katika Elimu Elimu ni nguzo ya maendeleo ya kijamii. Wanawake wanapopewa nafasi ya kusoma, jamii nzima hunufaika kwani mara nyingi huonekana kama wategemezi,hivyo wanapoapta furs ya elimu husaidia Kupunguza ujinga,Wanawake waliosoma huweza kufundisha watoto wao na kuhimiza familia nzima kuthamini elimu na mabadiliko hupatikana katika jamii nzima,Kama ambavyo Malala Yousafzai kutoka Pakistan alivyosimama kidete kupigania haki ya wasichana kupata elimu. na Harakati zake zimekuwa mfano wa kimataifa kwamba mwanamke mmoja anaweza kuleta mabadiliko makubwa. Wanawake katika Uchumi Wanawake wanashiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi, kuanzia kilimo, biashara ndogo ndogo, hadi uongozi wa jamii na mashirika makubwa. 
 Katika kilimo Wanawake wengi vijijini ndio wanaolima mashamba ya chakula, ambayo inahakikisha familia na taifa linapata chakula cha kutosha ukilinganisha na wanaume. MIFANO Katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha,ndani ya hiiTanzania wanawake wamekuwa mstari wa mbele katika kilimo cha kahawa , huku Biashara ndogo ndogo, zikiongozwa na Wanawake mijini huendesha biashara za sokoni, kuuza matunda, nguo na bidhaa mbalimbali,ambapo bila shaka mwanamke ni zaidi ya injini ya uchumi wa kila siku. Wanawake katika Afya na Huduma za Jamii , Wanawake pia ni wahudumu wakuu wa afya na ustawi wa jamii. 
 Wauguzi na wakunga,Wanawake wengi hufanya kazi kama wauguzi na wakunga, wakihakikisha mama na mtoto wanapata huduma bora,mfano hai Katika hospitali za vijijini Tanzania, wakunga wanawake ndio wanaosaidia akina mama kujifungua salama,Bila wao, vifo vya uzazi vingekuwa vingi zaidi. Upande wa Huduma za kijamii,Wanawake hushiriki katika vikundi vya kijamii kama vikoba, ambavyo husaidia familia kupata mikopo midogo na kujiendeleza kiuchumi. 
 Wanawake katika Uongozi na Siasa Wanawake wanaposhiriki katika uongozi, maamuzi yanakuwa jumuishi na yenye kuzingatia mahitaji ya jamii Ellen Johnson Sirleaf, Rais wa zamani wa Liberia, alionyesha dunia kwamba mwanamke anaweza kuongoza taifa na kuliletea amani baada ya vita. 
 Wakati Tanzania,Rais Samia Suluhu Hassan nae ni kielelezo cha mchango wa wanawake katika siasa, Uongozi wake umeweka Tanzania katika ramani ya kimataifa na kuonyesha kuwa wanawake wana uwezo wa kusimamia maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Jee Wanawake na Kulinda Utamaduni Wanawake ni walinzi wa utamaduni na mila katika jamii ,watekelezaji wa mila na warithisha mila hizo kwa kwa upamde wa hapa kisiwani Pemba, wanawake hushiriki katika utengenezaji wa mikeka na vikapu vya mkonge,ngoma za kimila ,ususi,ushoni Hii si tu sanaa bali pia ni chanzo cha kipato na utambulisho wa jamii. 
 CHANGAMOTO KWA WANAWAKE Changamoto Wanazokabiliana Nazo Licha ya mchango wao mkubwa,walionao katika harakati zote zinazohusu maendeleo ndani ya jamii lakini bado w wanawake hukumbana na changamoto nyingi ikiwemo Ubaguzi wa kijinsia, Wanawake mara nyingi hupunguzwa nafasi katika uongozi na ajira Kama hapa anavyosimulia Hadia Faki Mkaazi wa Kiuyu minungwini ,mwabamke mjasiriamali biashara ndogo ndogo,Mkulima wa kilimo mseto mke na mama wa watoto 8 . 
 "Najishughulisha na shughuli mbali mbali kilimo na biashara ndogo ndogo za ushoni wa mikoba,makawa, ladu,mafuta ya mwani singo ,lakini pia ni mkulima na mnufaika wa Zanz adapt program na nendelea na kilimo msitu" Nimegombea lakini sijui imekuaje mpaka nimeshindwa kuingia hata katika hatua za mapema nimekosa fursa ,bado jamii haioni umuhimu wa sisi kutushirikisha hata tukizitafuta fursa " "Ukosefu wa mitaji, kazi yangu ninayoitegemea kupata kipato ni kilimo na hapa kwetu Wanawake wengi hawana uwezo wa kupata mikopo ya kifedha kwa ajili ya biashara licha ya kuwa mstari wa mbele katika kila jambo la maendeleo lakini zinapokuja fursa kama hizo tunasahauliwa.
 SULUHISHO 
 Elimu kwa wote,Uwezeshaji kiuchumi,Sheria na sera, Serikali kuweka sera zinazolinda haki za wanawake dhidi ya ubaguzi na unyanyasaji. Kwani wanawake wanapopata fursa wanafanya vizuri mfano ni Programu za kukopa na kuweka vikoba na SACCOS ambazo kwa asilimia kubwa zinaendeshwa na wanawake zimekuwa zikiwasaidia kujiendeleza kiuchumi na kijamii. Kauli kwamba “Wajibu wa wanawake unatambuliwa kuwa muhimu katika kazi za jamii na maendeleo ya kijamii” si maneno matupu bali ni ukweli unaojidhihirisha kila siku.
 Wanawake ni walimu, wakulima, viongozi, wahudumu wa afya, na walinzi wa utamaduni na mazingira Bila mchango wao, jamii isingeweza kusonga mbele. Ni wajibu wa kila mtu kuhakikisha wanawake wanapewa nafasi sawa na wanaume ili kuendeleza jamii na kufanikisha maendeleo endelevu,kama ambavyo mradi wa Zanzibar women leadership climate change and adaptation ZANZ ADAPT unaotekelezwa na Community Forest Pemba CFP ,CFI NA TAMWA ZANZIBAR ulivyokuja kuwakomboa wanawake kutimiza malengo yao ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi kushiriki katika uongozi pamoja na kuwakomboa kiuchumi. 
MWISHO

Jumatatu, 2 Juni 2025

ENEO LA EKA 10 LAKABIDHIWA KWA WAZIRI ADOLF MKENDA, NI KWA AJILI YA UJENZI WA SKULI YA UFUNDI KAMBINI-KOJANI

 

Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema  ujenzi wa Skuli ya Ufundi itakayojengwa hivi karibuni  kambini kisiwani Pemba ni kuunga mkono serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika uimarishaji maendeleo ya elimu inayoendelea kuimarishwa  kwa kiwango kibwa na serikali ya amwanu ya Nan echini ya Rais Dr. Hussein Ali Mwinyi

Prefesa Mkenda ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa jimbo la Kojani katika hafla la makabidhiano ya eneo la ujenzi wa Skuli ya Ufundi Kambini Kichokochwe lililokabidhiwa na mbunge wa jimbo hilo Hamad Hassan Chande  itakayoanza kujengwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teklojia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ambapo jumla ya ekari kumi zimekazibiwa kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho .

Aidha Pro, Mkenda amesema Wizara yake itaendelea kufanyakazi kwa pamoja na Wiara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar ili kuona sekta ya elimu inaendelea kuimarika visiwani.

Amesema Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatambua juhudi kubwa zinazofanywa na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika sekta ya elimu ikiwemo ujenzi wa kujenga Skuli za ghorofa kila katika maeneo mbali mbali ili kurahisisha watoto kusoma kwa utulivu.

Aidha amesema kuwa Wizara yake imekuwa ikishirikiana bega kwa bega na Wizara ya Elimu na Mfunzo ya Amali Zanzibar, lengo ikiwa ni kuona suala la maendeleo ya elimu linawanufaisha wananchi wa pande zote mbili.

Akimkaribisha Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia kuzungumza na wananchi, Mbunge wa Jimbo la Kojani ambaye ni Naibu Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hamad Hassan Chande.



Amesema ujenzi wa kituo hicho utaleta manufaa makubwa kwa vijhana wa jimbo la Kojani na wengine wengi wanaotoka maeneo tofauti ya kisiwani Pemba.

Aliwataka wananchi wa jimbo la Kojani kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan na ya Zanzibar inayoongozwa na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa juhudi kubwa wanazochukua kuwafikishia wananchi huduma mbali mbali za maendeleo.

Aidha Chande aliongeza kwa kusema kuwa ujenzi wa Skuli hiyo ya Ufundi ambayo itakuwa ya kwanza kwa Mkoa wa Kaskazini Pemba itafungua zaidi milango ya elimu kwa vijana wa jimbo la  Kojani na Pemba kwa ujumla.

Afisa Mdhamini wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba Moh`d Nassor Salim ameahidi kuwa Wiraya ya Elimu Zanzibar itakuwa karibu kutoa ushikiano wa Skuli hiyo.

Amesema Wizara ya Elimu ya Zanzibar imekuwa ikishirikiana kwa karibu na Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekbolojia katika masuala tofauti ya kielimu ikiwemo bodi za mikopo ya elimu ya juu.

Nao kwa upande wao baadhi ya wazee wa Shehia ya Kambini wamesema ujenzi wa mradi huo wa Skuli ya Ufundi wameupokea kwa mikono miwili na watatoa ushirikiano kwa wajenzi.

Mzee Hamad Khamis Kombo wa Kambini ameishukuru Serikali kwa hatua ya ujenzi wa kituo hicho katika Shehia ya Kambini kwa kusema kuwa pamoja kuwa na vijana wengine wa jimbo la kojani watasoma kwenye skuli hiyo lakini wao ndio wanufaika wakubwa.



Naye Bakari Ali Hassan wa kijiji cha Kangagani amesema suala la kujengwa skuli ya ufundi kitatoa fursa mbali mbali kwa wenyeji wa jimbo la kojani hasa kambini.

 Rauhiya Khatib Juma ni kijana wa Shehia ya Kambini amesema skuli hiyo ya ufundi itasaidia kwa kiasi kikubwa kwa vijana wa mikoa miwili ya Kusini na Kaskazini Pemba na kumshukuru ubunge wa jimbo la Kojani Hamad Hassan Chande kwa juhudi zake zilizopelekea kujengwa kwa kituo hicho.