Shamsi Vuai Nahodha Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameelezea kushangazwa kwake na hatua za kutochukuliwa watu waliohusika na ufisadi wa Sh60 bilioni wakati wa utawala wa Rais Amani Abeid Karume.
Akihutubia mkutano wa hadhara mjini Unguja, Nahodha amesema ufisadi huo ulibainika baada ya uchunguzi wa Kamati Teule ya Baraza la Wawakilishi.
Nahodha amesema ripoti hiyo ilitaja hadi waliohusika na ufisadi huo lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa hadi leo.
Nahodha ametoa tuhuma hizo licha ya ukweli kuwa kipindi cha utawala wa Rais Karume, alikuwa Waziri Kiongozi kwa miaka 10.
Waziri huyo wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wa Tanzania amesema kuwa, dhana ya kufanyika Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 ilikuwa ni kuimarisha huduma za jamii kama utoaji wa elimu bure, umiliki wa ardhi kwa wananchi wanyonge na kupinga vitendo vya ubaguzi na matabaka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni