Habari

Jumapili, 24 Novemba 2013

ZIARA YA DK SHEIN PEMBA ILIVYOZIDI KUNOGA

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na watoto wa Kijiji cha Chonga,wakati alipofika kijijini hapo kufungua kituo kipya cha Ununuzi wa Karafuu cha ZSTC,akiwa katika ziara ya Mkoa wa Kusini Pemba kutembelea vituo mbali mbali. [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] 

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Mama Mwanamwema Shein (katikati) pamoja na viongozi aliofuatana nao wakipata maelezo kutoka kwa Mpasishaji wa karafuu katika Kituo cha ZSTC Mkoani  Khamis Nassor Mohamed,alipotembela kituo hicho akiwa katika ziara ya Mkoa wa Kusini Pemba.



 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Mama Mwanamwema Shein (katikati) pamoja na viongozi aliofuatana nao,walipotembela kuangalia hatua za Ujenzi wa Ikulu ya Mkoani,wakati alipofanya ziara katika Mkoa wa Kusini Pemba.


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akitoa maelekezo kwa wahusika wa Ujenzi wakati alipotembelea maendeleo ya ujenzi wa Ikulu ya Mkoan, alipofanya ziara katika Mkoa wa Kusini Pemba.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipotembela madarasa ya Skuli ya Kengeja Msingi baada ya kuyafungua rasmi,(kushoto) Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Zahra Ali Hamadi,na (kulia) Msaidizi Mwalimu Mkuu Issa Ali Hamadi,ufunguzi huo ulifanyika jana alipokuwa akiendelea na ziara yake katika Mkoa wa Kusini Pemba.

Baadhi ya Wanafunzi na Wazee wa Kijiji cha Kengeja waliohudhuria katika sherehe za Ufunguzi wa madarasa 7 ya Skuli ya Kengeja msingi,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) alipokuwa akitoa hutuba yake jana,na kuwataka Wazee waache tabia ya kuwaozesha Watoto wao wakiwa bado wadogo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni