KATIKA dunia inayokumbwa na majanga ya mara kwa mara—kutoka kwa mafuriko, vimbunga, hadi matetemeko ya ardhi—ni muhimu kuhakikisha kuwa kila mtu anapata ulinzi sawa.Hili linakuwa la dharura zaidi kwa watu wenye ulemavu, ambao mara nyingi huachwa nyuma katika mipango ya dharura na usimamizi wa maafa. Zanzibar, kama sehemu ya Tanzania, imechukua hatua kadhaa kuunda sera ya maafa inayolenga kujenga jamii jumuishi.Lakini je, sera hiyo inazingatia kwa kina mahitaji ya watu wenye ulemavu? Makala hii inachambua kwa undani suala hilo, ikihusisha sauti za watu wenye ulemavu, jamii, jumuiya zao, wataalamu wa maafa, na sera yenyewe.
MUKTADHA WA ZANZIBAR NA CHANGAMOTO ZA MAAFAZanzibar ni visiwa vinavyokumbwa na changamoto za kijiografia na hali ya hewa, ikiwemo mafuriko, vimbunga, na kuongezeka kwa kina cha bahari. Kwa mujibu wa Tume ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar, majanga haya yamekuwa yakiongezeka kwa kasi, na hivyo kuhitaji sera madhubuti za kukabiliana nayo.
WATU WENYE ULEMAVU
Adil Mohammed mwenye ulemavu wa uoni anasema,watu wenye ulemavu wanakabiliwa na changamoto za kipekee ikiwemo kukosa taarifa kwa wakati kuhusu maafa.Anasema changamoto nyengine Miundombinu isiyo rafiki ya barabara kwa watu wenye ulemavu kupelelkea siku za maafa kupata changamoto za usafiri na mara nyengine kulazimika kupata misaada.Anafahamisha kuwa ukosefu wa huduma za dharura zinazozingatia mahitaji yao maalum kipindi cha majanga haujapewa kipaumbele hivyo kuwanyima haki zao.Bi Asha Suleiman, mkazi wa Mwera na mlemavu wa miguu, anasema wakati wa mafuriko mwaka jana, walipewa taarifa kupitia redio. “Mimi siwezi kusikia vizuri, na hakuna mtu aliyenifahamisha kwa wakati. Nilijikuta nimezingirwa na maji bila msaada.” alisema.Ushuhuda kama huu unaonesha pengo kati ya sera na uhalisia. Watu wenye ulemavu wanahitaji mifumo ya mawasiliano mbadala—kama vile ujumbe wa maandishi, alama, au hata wahamasishaji wa kijamii.
JUKUMU LA JAMII NA JUMUIYA ZA WATU WENYE ULEMAVUJumuiya kama Zanzibar Association of People with Disabilities (ZAPD) imekuwa mstari wa mbele katika kutetea haki za watu wenye ulemavu. Kwa mujibu wa ZAPD, inaeleza utaratibu wake wa kutoa mafunzo kwa vikundi vya dharura kuhusu jinsi ya kuwahudumia watu wenye ulemavu, kupendekeza ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu katika kamati za mipango ya maafa na uundaji wa vituo vya dharura vinavyofikika kwa urahisi.“Tumejadiliana na Tume ya Maafa kuhusu kuingiza mahitaji yetu katika mipango ya dharura. Kuna maendeleo, lakini bado kuna kazi kubwa ya kufanya.”Ushirikishwaji wa Watu Wenye Ulemavu Katika MipangoSera ya Maafa Zanzibar inasisitiza ushirikishwaji wa jamii, bado watu hao wanalalamika kuhusu kukosa fursa ya kujumuishwa kikamilifu. Baraka Hassan mwenye ulemavu wa viungo anasema wanahitaji nafasi ya kutoa maoni katika mikutano ya mipango.
kuwajumuisha katika kamati za utekelezaji na Walitoa maoni yao wakisema Maafa Hayachagui, Lakini Mipango Inaweza Kutoa Ulinzi Sawa, wakati majanga yanapotokea, ni muhimu watu hao kupata taarifa kwa wakati, huduma sahihi, au miundombinu inayowafaa, ili kuweka usalama wa maisha yao.Jamii, jumuiya za watu wenye ulemavu, wataalamu wa maafa, na serikali wanapaswa kushirikiana kwa dhati. Maafa hayachagui nani wa kumdhuru—lakini sisi tunaweza kuchagua kuwa jumuishi, wenye huruma, na wenye haki.
JUMUIYA YA WATU WENYE ULEMAVU ZANZIBAR (JUWAUZA)
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Salma Haji Saadat anasema,Zanzibar imebarikiwa kuwa na sheria nyingi za watu wenye ulemalu licha ya kuwa utekelezaji wake ni mdogo jambo ambalo linawakosesha fursa watu hao.Utekelezaji wa sheria hauna muamko wa kutosha kwani mambo mengi yanagharama na yanakuwa magumu kutekelezwa kwa sababu yanakuwa na gharama kubwa.
SERA YA MAAFA ZANZIBAR
Kwa mujibu wa Mtendaji wa ofisi inayohusika na maafa Zanzibar, alijitambulisha kwa jina la Fahad anasema Sera ya Maafa Zanzibar (Disaster Risk Reduction Policy) imeundwa kwa lengo la kupunguza hatari za maafa, kuimarisha uwezo wa jamii kukabiliana na majanga, kuhakikisha ushirikishwaji wa makundi yote ya kijamii.Aidha alisema katika nyaraka za sera hiyo, kuna marejeo ya makundi maalum kama vile wanawake, watoto, na watu wenye ulemavu. Hata hivyo, changamoto ni jinsi utekelezaji unavyofanyika kwa vitendo.
SHERIA YA MAAFA YA ZANZIBAR YA MWAKA 2015—ZANZIBAR DISASTER RISK REDUCTION AND MANAGEMENT ACTSheria hii ina sehemu mbalimbali zinazohusu mipango ya kitaifa, kamati za usimamizi kuanzia ngazi ya shehia hadi taifa, na wajibu wa wadau mbalimbali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni