Gunia za karafuu zilizokamatwa katika kijiji cha Makangale Wilaya ya Micheweni zikiwa katika kituo cha polisi cha Wilaya ya Micheweni Pemba.
Na Is-haka Mohammed,Pemba.
Vikosi vya ulinzi na usalama Wilaya ya Micheweni vimefanikiwa kukamata
magunia 20 ya karafuu kavu zikiwa katika harakati ya kutaka kusafirishwa nje ya
nchi kwa njia ya magendo.
Akizungumza
na Zenji FM Radio Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Juma Abdalla Ali amesema karafuu
hizo zilikamatwa usiku wa kuamkia tarehe 31 huko Makangale Wilaya ya Micheweni
Pemba.
Amesema kuwa
taarifa za kukamatwa karafuu hizo zilipatikana baada ya wananchi raia wema
kutoa taarifa kwa vikosi vya usalama na ndipo juhudi za kudhibiti zilipochukuliwa
kwa haraka.
Amesema
karafuu hizo zilipatika katika nyumba moja ambayo ipo karubu na fukwe za bahari
maeneo hayo ya makangale.
Abdalla
amedai kuwa hadi sasa hakuna mtu
anayeshikiliwa kutokana na tukio hilo ila ameeleza kuwa watu wanaokisiwa
kufikia saba walikimbia baada ya kuvamiwa katika nyumba zilizokuwa karafuu hizo
ambapo ni mita kama 20 kutoka katika ufukwe wa bahari.
Hata hivyo
Mkuu wa Wilaya huyo amesema kuwa hadi sasa
thamani halisi ya karafuu hizo bado hazijajulikana hadi pale zitakapopimwa
na kujulikana daraja lake na zipo kilo ngapi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni