KATIKA jamii nyingi duniani, watu wenye ulemavu wamekuwa wakionekana kama kundi linalohitaji msaada wa kudumu, mtazamo huu umekuwa ukichochea dhana potofu kwamba hawawezi kujitegemea kiuchumi.
Hali hii si tofauti kwa Zanzibar, ambako baadhi ya wananchi bado wanaamini kuwa watu wenye ulemavu ni tegemezi na hawawezi kuishi bila ya vikopo vya misaada barabarani. Hata hivyo, ushahidi unaonyesha kuwa wanawake na wanaume wenye ulemavu wana uwezo mkubwa wa kujitegemea kiuchumi endapo watapatiwa mitaji, mafunzo na mazingira rafiki ya biashara.
TAKWIMU ZA WATU WENYE ULEMAVU
Viashiria ya kijamii, uchumi na mazingira vilivyojitokeza katika sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2022, vinaonyesha kuwa Zanzibar watu wenye ulemavu kuanzia miaka 7 na kuendelea ni 114 kwa kila 1000.Ripoti inaonesha idadi ya watu wenye ulemavu imeongezeka kwa watu 39 kwa kila 1,000 kati ya sensa ya mwaka 2012 na ya 2022.
HALI YA KIUCHUMI KWA WATU WENYE ULEMAVU
Wanawake na wanaume wenye ulemavu wameanzisha biashara ndogondogo ikiwemo ufumaji wa bidhaa za mahoteli, ushonaji wa nguo na ujasiriamali.
Hii ni ishara tosha kwamba ulemavu si kikwazo cha mafanikio ya kiuchumi.Aisha Ali Abdallah, mlemavu wa uoni ni mjasiriamali anaetengeneza na kuuza bidhaa za vipodozi, sabuni na mafuta anajitegemea kuendesha maisha yake na mara kadhaa amekua akitoa msaada kwa wazazi wake.anasema ni vyema kuwekwa mazingira rafiki ya biashara hasa kupatiwa mitaji na masoko ili kukuza uchumi wao bila kutegemea misaada.“Changamoto kubwa inayotukabili watu wenye ulemavu ni ukosefu wa mitaji, bila ya mitaji, hata wazo bora la biashara haliwezi kutekelezwa” anasema.
Ili kupiga hatua za kimaendeleo anasema ni vyema kuhamasisha jamii kupitia vyombo vya habari kuhusu uwezo wa watu wenye ulemavu, anashauri serikali Kushirikisha jumuiya za watu wenye ulemavu katika kutunga sera na mipango ya maendeleo.Fatma Ali, Mjasiriamali Mlemavu wa Miguu ameanzisha biashara ya ushonaji nguo katika eneo la Mwera, Unguja. Biashara yake imekua na sasa anatoa ajira kwa wanawake wengine, wakiwemo wenye ulemavu.Anasema anafanya kazi kwa kutumia mashine za kushona na hujipatia kipato cha kutosha kuendesha maisha bila kutegemea misaada.
MITAZAMO YA JAMII
Hanifa Mohammed Said anasema, umefika wakati jamii kuachana na dhana walioijenga muda mrefu kuwa watu wenye ulemavu ni kundi linalohitaji msaada wa kudumu.Anashauri seriakali kuandaa mikakati ya kuona wadau na wahisani wenye uwezo kuwapa mitaji ya kuwawezesha ili kufanya biashara na shughuli za kuwaingizia kipato ili kukidhi mahitaji yao ya kila siku na sio kuwapa chakula cha siku chache kisha kukosa shughuli za kufanya.“Wanahitaji kupatiwa mitaji ya kufanya kazi zenye muendelezo wa kukuza uchumi wao ili kuondokana na kadhia ya kila siku kupokea msaada mdogo ambao hauwezi kukidhi mahitaji zaidi ya siku tatu kwenye familia zao” anasema.Khamis Saleh Khamis anaeleza kuwa hali ya sasa imesababisha baadhi ya wananchi kuamini watu wenye ulemavu hawawezi kujitegemea kiuchumii, jambo ambalo si tu linawadhalilisha bali pia linazuia fursa za maendeleo kwa watu hao.“Mitazamo ya jamii kwamba watu wenye ulemavu ni tegemezi imejengwa kwa miaka mingi kutokana na ukosefu wa elimu na uelewa” anasema. Mwanakheri Rajab Hilali anasema iIli kubadilisha mitazamo mibaya kwa jamii elimu inahitajika kubainisha uwezo wa watu wenye ulemavu na kuimarishwa kupitia vyombo vya habari, mashule, na taasisi za dini.Anasema ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu katika shughuli za kijamii na kiuchumi unapaswa kupewa kipaumbele, pamoja na kuonesha mafanikio ya wafanyabiashara wenye ulemavu kama mfano wa kuigwa.
JUMUIYA YA WANAWAKE WENYE ULEMAVUMwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wenye Ulemavu Zanzibar Salma Haji Saadat, anasisitiza jamii kuwatizama watu hao katika mtizamo chanya kuona kwamba wanaweza kuleta mabadiliko katika kuchangia mapato ya nchi na kukuza uchumi wao.“Tunashuhudia watu wenye ulemavu wakiwa na vikopo vyenye rangi moja wakiomba pesa katika maeneo mbali mbali ya zanzibar hili sio jambo jema na linasikitisha hasa kutokana na mila na desturi za Kizanzibari” anasema.Anasema watu wenye ulemavu wana uwezo wa kufanya kazi kama ilivyo watu wengine au zaidi ya watu wa kawaida kutokana na uwezo waliobarikiwa.“utawakuta Watu wenye ulemavu wametapakaa kila kona hasa maeneo ya mjini wakioneka kazi yao ni kuomba tu ili kupata kipato chao bila ya kuangalia uwezo wao wa kazi” anasemaAnasema miongoni mwa changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu ni kukosa masoko, mikopo ya 4.4.2 ili kujiendeleza kuichumi.Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania-Zanzibar (TAMWA)Afisa Programu na Mawasiliano Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania-Zanzibar (TAMWA) Khairat Haji anasema TAMWA kwa kushirikiana na taasisi mbali mbali imewezesha watu wenye ulemavu kuanzisha miradi ya sabuni za maji, vipodozi, ushonaji wa mikoba na nguo, na kilimo cha mboga za majani ili kunyanyua uchumi wao.Anatolea mfano mradi wa Kijaluba Isave, ulioendeshwa na TAMWA Zanzibar kwa kushirikiana na SHIJUWAZA, ambao watu wenye ulemavu wamewezeshwa kuunda vikundi vya kuweka na kukopa ili kukuza uchumi wao na kuacha kuwa tegemezi.(WAKALA WA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI ZANZIBAR (ZEEA) inasema imechukua hatua za kuwawezesha watu wenye ulemavu kwa kutoa mikopo kwa masharti nafuu, kutoa mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa fedha.Kwa mujibu wa taarifa za ZEEA, takriban watu wenye ulemavu 170 wamepatiwa mikopo ya 4.4.2 kuanzia mwaka 2024 hadi sasa.Kati yao wanawake 93 na wanaume 79 hatua inayolenga kuondoa utegemezi wa misaada ya huruma na kuwezeshwa kiuchumi.SHERIA,MIKATABAKuhusu uwezeshaji wa kiuchumi kwa watu wenye ulemavu, Tanzania ina mwongozo kupitia Sheria ya Watu Wenye Ulemavu ya mwaka 2010 (Persons with Disabilities Act, 2010).sheria hiyo inaeleza kuwa kila mtu mwenye ulemavu ana haki ya kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi,kijamii na kisiasa.serikali na mamlaka husika zitahakikisha kuwepo kwa sera, programu na mikakati ya kuwawezesha watu wenye ulemavu kupata ajira, mikopo,mafunzo ya ujuzi, na fursa nyengine za kujipatia kipato, bila ubaguzi wowote kutokana na hali ya ulemavu.Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Watu Wenye Ulemavu (CRPD, 2006)Kifungu cha 27: Kinahusu Haki ya Kazi na Ajira. Kinaeleza kuwa watu wenye ulemavu wana haki ya kufanya kazi kwa uhuru, kuchagua ajira wanayoipenda, na kufanyiwa mazingira rafiki bila ubaguzi.Kifungu cha 28: Kinahusu Haki ya Kiwango Bora cha Maisha na Ustawi wa Kijamii, ikiwemo upatikanaji wa huduma, mikopo, na fursa za kiuchumi.Nchi wanachama (ikiwemo Tanzania) zinapaswa kuweka sera na programu za kuwawezesha kiuchumi, ikiwemo mafunzo ya ufundi, mikopo midogo, na ajira zenye staha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni