Na ,Amina Ahmed Moh'd
Kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964, elimu ya maandalizi Unguja na Pemba haikuwa rasmi wala jumuishi. Ilitolewa kwa upendeleo wa kijamii na kikabila, na iliwafikia wachache wa tabaka la juu maeneo ya mijini pekee.
Watoto wa maskini, wakulima na wavuvi walikosa fursa
Hakukuwa na skuli za serikali za maandalizi
Vijijini, watoto walitegemea (Madrasa) elimu ya dini pekee
Hakukuwa na utaratibu wa lishe, walimu walikuwa wachache na wengi wageni wasio kuwa wazawa
Mfumo wa elimu ya maandalizi ulikuwa wa kikoloni na kisultani, elimu ikiwa si haki ya kila ZANZIBAR
LAKINI BAADA YA MAPINDUZI YA 1964 – MIAKA 62 BAADAYE (2026)
Mapinduzi yameleta mageuzi makubwa katika elimu ambapo
Elimu ndani ya miaka 62 ya Mapinduzi kupitia serikali ya awamu ya nane iliyo chini ya Dk Hussein Ali Mwinyi imekuwa ni haki ya kila mtoto bila ubaguzi wa kidini, itikadi za siasa ,uchumi ,maumbile wala hali za maisha kama ilivyokuwa kabla ya Mapinduzi yam waka 64 .
Huku Zaidi ya skuli 262 za maandalizi Unguja na Pemba ndani ya miaka 62 ya Mapinduzi
Skuli 97 zimekarabatiwa, 36 mpya zinajengwa maeneo mbali mbali .
Walimu wapya 889 wameajiriwa ndani ya miaka 62 mwaka (2025/26)
Wanafunzi wapatao 105,101 (82.5%) wameandikishwa jambo ambalo awali kabala miaka 62 ya Mapinduzi halikuwepo
Wanafunzi 63,099 (50%) wanapata lishe maskulini kupitia ruzuku maalum ya serikali
ZANZIBAR YA LEO katika elimu ina mfumo jumuishi wa elimu, miundombinu bora, walimu wenye sifa na huduma za kijamii maskulini ,lishe na mazingira yaliorafiki kwa wote
________________________________________
Miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia serikali ya awamu ya nane inayoongozwa na Dk Hussein Ali Mwinyi ni ushahidi kuwa: Elimu si upendeleo bali Elimu ni haki kwa watu wa aina zote kuanzia madarasa ya awali.
Mapinduzi yameifanya haki hii kufika kwa kila mtoto wa Zanzibar popote alipo mjini na Vijijini
Maono ya kiongozi bora huonekana pale elimu inapokuwa haki ya kila mmoja huku Taifa imara hujengwa na viongozi wanaothamini elimu bila ubaguzi kwani Uongozi bora huacha alama kupitia elimu jumuishi na yenye usawa kuanzia ngazi ya awali hadi vyuo vikuu .
JEE WAJUWA Kabla ya Mapinduzi (1964)
• Elimu ya maandalizi haikuwa rasmi wala jumuishi.
• Iliwafikia wachache wa tabaka la juu mijini pekee.
• Watoto wa maskini, wakulima na wavuvi walikosa fursa.
• Hakukuwa na skuli za serikali za maandalizi.
• Vijijini, watoto walipata elimu ya dini kupitia madrasa pekee.
• Walimu wachache, wengi wakiwa wageni wasio wazawa.
• Mfumo ulikuwa wa kikoloni na kisultani, elimu si haki ya kila mtoto.
Baada ya Mapinduzi (1964–2026)
• Elimu imekuwa haki ya kila mtoto bila ubaguzi wa dini, siasa, au hali ya maisha.
• Skuli za maandalizi 262 zimeanzishwa Unguja na Pemba.
• Skuli 97 zimekarabatiwa na 36 mpya zinajengwa.
• Walimu wapya 889 wameajiriwa.
• Wanafunzi 105,101 (82.5%) wameandikishwa.
• Wanafunzi 63,099 (50%) hupata lishe shuleni kupitia ruzuku ya serikali.
• Mfumo wa elimu sasa ni jumuishi, wenye miundombinu bora, walimu wenye sifa, na mazingira rafiki.
Hitimisho
Mapinduzi ya Zanzibar yamebadilisha elimu kutoka upendeleo wa kikoloni hadi haki ya kila mtoto. Leo, elimu jumuishi na yenye usawa imejengwa kuanzia madarasa ya awali hadi vyuo vikuu, ikionesha maono ya uongozi bora unaothamini elimu kwa wote.
FREELANCER
AMINA AHMED MOH`D – ( BIYAYA)
0776 -859 184
minnah1202@gmail.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni