Hawa ndiyo baadhi ya ng`ombe wanaokabiliwa na maradhi ya ngozi yanayojulikana kitaalam kwa jina la "Lamp Skin Deasess"(LSD) ambayo yamepelekea ng`ombe zaidi ya 10 kufa Wilaya ya Chake Chake.
Na Is-haka
Mohammed,Pemba.
Maradhi ya ngozi yanayowakabili ng`ombe
katika maeneo ya Wilaya ya Chake Chake kisiwani Peemba yamewatia hofu baadhi ya wafugaji baada ya mifugo yao hiyo
kuendelea kuugua na wengine kuanza kupoteza maisha.
Baadhi ya
wafugaji hao wameieleza blog hii jinsi ya maradhi hayo yanavyowaathiri ng`ombe kwa kupata homa kali inayowasababishia
kutoweza kutembea,kula na hatimae baadhi yao kufa.
Khamis Moh`d
Khamis anayefanyia shughuli zake za ufukaji katika eneo la Mwanamwaja amesema
kuwa magonjwa hayo ya ngozi yamekuja kutokana na mifugo hiyo kutopatiwa chanjo
kwa muda mrefu.
“Unajua
inakaribia mwaka wa tano saivi ng`ombe hawajapatiwa hizi chanjo kwa hivyo tuna
wasiwasi ya kuwa hilo ndiyo sababu kubwa ya kuwepo kwa magonjwa haya”Alisema
Khamis.
Alisema kuwa
baada ya ng`ombe kupata maradhi hayo hupata homa kali na kuonekana dhaifu huku
wakishindwa kutoa maziwa.
Naye Rashid
Omar Moh`d wa kijiji cha Mbuni ambaye tayari ng`ombe wake watatu wenye gharama
ya zaidi ya shilingi milioni tatu wameshakufa kutakana na maradhi hayo
yanayoambukiza.
“Mimi kwa
kweli magojwa haya yameniathiri kwani hadi sasa ng`ombe watatu wameshakufa na
wengine wawili wanaendelea na maradhi,kwa kweli nimekata tama”Alisema Rashid
kwa Masikitiko.
Aidha Rashid
alisema kuwa hivi sasa yeye na wafugaji wenzake wamekosa raha hasa baada ya
madaktari kutowaweka wazi juu ya tiba sahihi ya maradhi hayo.
“Tunaiomba
serikali ituangalie na sisi wafukaji wa hali ya chini maana tunategemea katika
ng`ombe wetu lakini ndo hivyo maradhi yanawamaliza ni vizuri wakafanya utafiti
wa tatizo hili” Alisisitiza Rashid.
Mfugaji Mzee
Ame yeye amesema kuwa ipo haja kwa Idara
ya Mifugo kuanzisha chanjo kila kipindi ili kuweza kuepusha magojwa hayo
yanayoweza kuwamaliza ng`ombe wao.
Mzee huyo
alisema kutokana na kutokuwepo kwa tiba ya uhakika wamelazimika kutumia dawa
mbadala ya kuwaogeshwa kwa maji ya chumvu katika sehemu zilizoathirika na kuwachemshia
na kuwanwesha mwarubaini ambapo wamedai wengine zimekuwa zikiwasaidia.
Akizungumzia
suala hilo Afisa Mifugo na Tiba Wilaya ya Chake Chake Dk Hemed Suleiman Hemed amethibitisha
kuwepo kwa tatizo hilo linalowakumba ng`ombe hapa kisiwani Pemba na kudai yanasababishwa
na vimelea vinavyoambukizwa kwa kwa ng`ombe tu.
Alisema
magonjwa hayo yapo zamani kisiwani Pemba lakini kipindi kirefu yalipotea baada
ya chanjo ambayo ilitolewa kwa ng`ombe hata hivyo katika kipindi cha miezi
miwili iliyopita yamerudi tena katika maeneo mbali mbali ya wilaya ya Chake
Chake.
Alisema
maradhi hayo yanapompata ng`ombe hufanya maboge katika mwili na mgongoni na
endapo hatapata chanjo kwa muda uliohitajika ng`ombe anaweza kupoteza maisha.
“Hivi sasa
tunaendelea na kutoa chanjo kwa ng`ombe katika maeneo tofauti ya wilaya ya
chake na zaidi ya ng`ombe 2000 wameshapatiwa chanjo hiyo ya kuzuia maambukizi”Alifahamisha
Dk Hemed.
Aidha kwa
upande mwengine amewaelekezea lawama wafugaji kwa kushindwa kuchukua hatua za
kuwapatia chanjo ng`ombe wao na kutoa wito kwa kuwapatia chanjo ili kuepusha
maambukizi zaidi kwa ng`ombe ambao hawajaathirika.
Clip………………………Dk Hemed
Ng`ombe
wapatao 10 wa maziwa wamesharipotiwa kufa kutokana na maradhi hayo hapa wilaya
ya chake chake, na baadhi ya wafugaji wamedai kuchelewa kwa chanjo ndiko
kulikopelekea kusambaa kwa maradhi hayo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni