Habari

Jumatano, 8 Aprili 2015

TIGO YAADHIMISHA SIKU YA KARUME ,Zanzibar

Mfalme wa vichekesho Tanzania, kwa jina maarufu King Majuto akiwa na msanii mwenziwe wakiwachekesha wakaazi wa Zanzibar, waliohudhuria katika tamasha la Tigo, la kuadhimisha siku ya Karume katika viwanja vya kufurahisha watoto,Kariakoo, Zanzibar.
.
 Kikundi cha D6 kikiwatumbuiza maelfu ya wakaazi wa Zanzibar, katika tamasha la Tigo,lililofanyika katika viwanya vya kuwafurahisha watoto, kariakoo,Zanzibar

Jumatatu, 2 Machi 2015

Tunzo za wasanii bora wa Muziki Zanzibar.

Mkurugenzi wa Biashara Zanzibar Nd. Mohamed Baucha wa kulia akimkabidhi Tunzo ya Video bora ya mwaka muziki wa kizazi kipya Nassir Hassan (Vanila) mara baada ya kuibuka mshindi, tunzo hizo zimeandaliwa na Kampuni ya Zanzibar Media Corporation LTD katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Mjini Zanzibar.

Jumatatu, 22 Desemba 2014


Na Fatma Haji Pemba.                                                                                                                 Waziri wa Biashara ,Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazrui ameitaka jamii zilizo na watu wenye ulemavu kuitikia wito wa serikali ya kuwasajili ili waweze kutambulika na kujumuishwa katika mipango ya serikali kama ilivyo kwa watu wengine wenye ulemavu.

Waziri huyo ameyasema hay oleo alikuwa akiwahubia wananchi mbali mbali waliojumuika katika maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu duniani ambayo kitaifa kwa upande wa Zanibar yameadhimishwa katika uwanja wa Tennis Chake Chake.
Amesema serikali imekuwa na mipango madhubuti ya kuwasaidia watu wenye ulemavu ikiwemo kuwapatia elimu,visaidizi na huduma nyengine mbali mbali hivyo sio vyema kwa jamii kuendelea kuwaficha watoto wao wenye ulemavu.

Hata hivyo amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Awamu ya Saba imeendelea kudumisha amani na utulivu katika nchi ili kutoa fursa kwa watu wote wakiwemo watu wenye ulemavu kuishi katika maisha ya amani.

Mapema Akisoma risala kwa niaba ya watu wenye ulemavu wa mikoa mitano ya Zanzibar  Bi Attie Suleiman Nassor wameiomba serikali   kuzidisha mashirikiano na jumuiya za watu wenye ulemavu na ulinzi katika kupambana na gharama za kupanda kwa maisha ili wafaidike muundo wa hifadhi ya jamii iliyopo.

Aidha Bi Attie ameiomba serikali  kuwasaidia watu wenye ulemavu  kwa kuingiza mahitaji yao katika mipango ya serikali ili kuweza kushiriki kikamilifu katika mipango ya kimaendeleo, sambamba na kutaka mfuko wa watu wenye ulemavu uweze kuwasaidia watu wenye ulemavu katika sekta ya elimu.


Baadhi ya wananchi waliofika katika maadhimisho hayo wamesema bado kuna changamoto kwa baadhi ya jamii ya kutowapeleka watoto wenye ulemavu katika vituo vyenye kutoa huduma za watoto wenye ulemavu  sambamba na kuwatambua watu wenye ulemavu wa aina tofauti.

Wamesema kuwa baadhi ya changamoto zinazoendelea kuwakumba watu wenye ulemavu ni kutothaminiwa na baadhi ya madereva wanaoendesha vyombo vya moto hasa gari za abiria wakidai kuwa huondosha magari hata ikiwa mtu mwenye ulemavu ajakaa katika siti au wakati mwengine kuwapitisha katika maeneo ya kushikia.