Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Waziri wa
Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema ujenzi wa Skuli ya Ufundi itakayojengwa hivi
karibuni kambini kisiwani Pemba ni
kuunga mkono serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika uimarishaji maendeleo ya
elimu inayoendelea kuimarishwa kwa
kiwango kibwa na serikali ya amwanu ya Nan echini ya Rais Dr. Hussein Ali
Mwinyi
Prefesa
Mkenda ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa jimbo la Kojani katika
hafla la makabidhiano ya eneo la ujenzi wa Skuli ya Ufundi Kambini Kichokochwe
lililokabidhiwa na mbunge wa jimbo hilo Hamad Hassan Chande itakayoanza kujengwa na Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teklojia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ambapo jumla ya ekari
kumi zimekazibiwa kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho .
Aidha Pro,
Mkenda amesema Wizara yake itaendelea kufanyakazi kwa pamoja na Wiara ya Elimu
na Mafunzo ya Amali Zanzibar ili kuona sekta ya elimu inaendelea kuimarika visiwani.
Amesema
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatambua juhudi kubwa zinazofanywa na
serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika sekta ya elimu ikiwemo ujenzi wa
kujenga Skuli za ghorofa kila katika maeneo mbali mbali ili kurahisisha watoto
kusoma kwa utulivu.
Aidha amesema kuwa Wizara yake imekuwa ikishirikiana bega kwa bega na Wizara ya Elimu na Mfunzo ya Amali Zanzibar, lengo ikiwa ni kuona suala la maendeleo ya elimu linawanufaisha wananchi wa pande zote mbili.
Akimkaribisha
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia kuzungumza na wananchi, Mbunge wa Jimbo
la Kojani ambaye ni Naibu Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Hamad Hassan Chande.
Amesema
ujenzi wa kituo hicho utaleta manufaa makubwa kwa vijhana wa jimbo la Kojani na
wengine wengi wanaotoka maeneo tofauti ya kisiwani Pemba.
Aliwataka
wananchi wa jimbo la Kojani kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania inayongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan na ya Zanzibar inayoongozwa
na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa juhudi kubwa wanazochukua kuwafikishia
wananchi huduma mbali mbali za maendeleo.
Aidha Chande
aliongeza kwa kusema kuwa ujenzi wa Skuli hiyo ya Ufundi ambayo itakuwa ya
kwanza kwa Mkoa wa Kaskazini Pemba itafungua zaidi milango ya elimu kwa vijana
wa jimbo la Kojani na Pemba kwa ujumla.
Afisa
Mdhamini wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba Moh`d Nassor Salim
ameahidi kuwa Wiraya ya Elimu Zanzibar itakuwa karibu kutoa ushikiano wa Skuli hiyo.
Amesema
Wizara ya Elimu ya Zanzibar imekuwa ikishirikiana kwa karibu na Wizara ya
Elimu, Sayansi na Tekbolojia katika masuala tofauti ya kielimu ikiwemo bodi za
mikopo ya elimu ya juu.
Nao kwa
upande wao baadhi ya wazee wa Shehia ya Kambini wamesema ujenzi wa mradi huo wa
Skuli ya Ufundi wameupokea kwa mikono miwili na watatoa ushirikiano kwa
wajenzi.
Mzee Hamad
Khamis Kombo wa Kambini ameishukuru Serikali kwa hatua ya ujenzi wa kituo hicho
katika Shehia ya Kambini kwa kusema kuwa pamoja kuwa na vijana wengine wa jimbo
la kojani watasoma kwenye skuli hiyo lakini wao ndio wanufaika wakubwa.
Naye Bakari
Ali Hassan wa kijiji cha Kangagani amesema suala la kujengwa skuli ya ufundi kitatoa
fursa mbali mbali kwa wenyeji wa jimbo la kojani hasa kambini.
Rauhiya Khatib Juma ni kijana wa Shehia ya
Kambini amesema skuli hiyo ya ufundi itasaidia kwa kiasi kikubwa kwa vijana wa mikoa
miwili ya Kusini na Kaskazini Pemba na kumshukuru ubunge wa jimbo la Kojani Hamad
Hassan Chande kwa juhudi zake zilizopelekea kujengwa kwa kituo hicho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni