Zanzibar.
JESHI LA POLISI MKOA WA KASKAZINI UNGUJA JANA LIMEFANYA OPERESHENI YAKUSHUSHA BENDERA ZA JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YAKIISLAM KATIKA MAENEO MBALI MBALI YA MKOA HUO.
JESHI HILO LIMETEREMSHA BENDERA HIZO ZILIZOKUWA ZIMEPACHIKWA KATIKA MITI ILI KUTEKELEZA AGIZO LA MAKAMO WAPILI WA RAIS WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI ALIYEWATAKA MKUU WA MKOA WA KASKAZINI UNGUJA,MKUU WA WILAYA YA KASKAZINI A NA B PAMOJA NA VIKOSI VYA ULINZI NA USALAMA KUHAKIKISHA NDANI YAKIPINDI CHA WIKI MOJA BENDERA HIZO ZINASHUSHWA.
LICHA YAKUSHUSHWA KWA BENDERA HIZO VIJANA WALIOPACHIKA BENDERA HIZO WALIKUWA KATIKA HALI YA UTULIVU WAKATI ZOEZI HILO LIKIENDELEA.
MIONGONI MWA VIJIJI VILIVYOENDESHWA ZOEZI HILO NI PAMOJA NA MAENEO YA NUNGWI,TAZARI,POTOA NA MKWAJUNI.
NAO VIJANA WA MKOA WA KASKAZINI UNGUJA WAMESEMA KUWA KUSHUSHWA KWA BENDERA HIZO SIO MWISHO WAKUUNGA MKONO HARAKATI ZAKUDAI MAMLAKA KAMILI YA ZANZIBAR ZILIZOKUWA ZIKIENDESHWA NA JUMUIYA NA TAASISI ZAKIISLAM ZANZIBAR.
MAPEMA WIKI ILIYOPITA AKITOA AGIZO LAKUSHUSHWA BENDERA HIZO MAKAMO WAPILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI ALIBAINISHA KUWA BENDERA ZINAZOTAMBULIWA KISHERIA NI ZILE ZA TAASISI ZA UMMA PAMOJA NA VYAMA VYA SIASA VILIVYOPATA USAJILI NA RIDHAA KUTOKA KWA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni