Na Is-haka Mohammed,Pemba. Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Juma Shamuhuna amesema Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kukabiliana na changamoto mbali mbali
zinazoikabili sekta elimu ili kuimaeisha sekta hiyo nchini.
Amesema
serikali inatambua kuwepo kwa tatizo la uhaba wa walimu wa Sayansi na walimu
wengine katika skuli mbali mbali lakini Wizara imekuwa ikifanya juhudi kubwa
kulipatia ufumbuzi tatizo hilo.
Waziri
Shamhuna ameyasema hay oleo huko Gombani Chake Chake wakati akiwahutubia
wanafunzi,walimu wazazi na wananchi mbali mbalii katika kilele cha maadhimisho
yamiaka 49 kutokea kutangazwa kwa Elimu bila ya malipo Zanzibar.
Amesema
katika kulipatia ufumbuzi tatizo la walimu nchini serikali imeimarisha fursa ya
nafasi za wanafunzi watakaosomea ualimu wa fani zote katika vyuo vikuu
vilivyopo Zanzibar.
Aidha
amesema serikali inaendelea kuimarisha maslahi ya walimu nchini ili kuhakikisha
kuwa watapata maslahi mazuri na kuweza kufundisha kwa ustadi zaidi na kutoa
wanafunzi wazuri watakaokuja lisadia taifa hapo baadaye.
Waziri wa
elimu na Mafunzo ya Amali Zanziba Ali Juma Shamuhuna amesema tatizo la utoro
maskulini ni moja kati ya mambo yanayochangia kwa wanafunzi wengi kushindwa
kufanya vizuri katika mitihani yao ya taifa.
Waziei
Shamhuna ameyasema hay oleo huko Gombani Pemba katika kilele cha maadhimisho ya
kutimia miaka 49 tokea kutolewa tamko la elimu bila ya malipo hapa visiwani
Zanzibar.
Amesema kuwa
utafiti uanaonyesha kuwa wimbi kubwa la wanafunzi wamekuwa wakikwepa kwenda
skuli,huku wengine wakishindwa kushughulikia masomo yao wawapo skuli au hata
majumbani .
Amewapongeza
walimu katika skuli mbali mbali kwa kujitolea kwa kusomesha kwa moyo mkunjufu licha ya kuwepo kwa changamoto
nyingi zinazowakabili.
Waziri huyo
amesema serikali inatambua changamoto zinazowakabili walimu hasa katika upande
wa maslahi yao,na kuwataka kuendelea kuvuta subira kwa vile muda mfupi ujao
wataanza kuona mabadiliko kwa upande wa maslahi yao.
Aidha
amesema tatizo la uhaba wa walimu wa sayansi na wa kada nyengine kwa baadhi ya
skuli serikali kupitia wizara hiyo wanaendelea kulipatia ufumbuzi .
Hata hivyo
amewataka walimu kuendelea na bidii katika kuwapatia elimu wanafunzi bila ya kuchoka huku serikali nayo ikiwa katika hatua za mwisho kurekebisha
maslahi ya walimu nchi kote.
Siku kama ya
leo miaka 49 iliyopita rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amaan
Karume alitangaza elimu bure visiwani hapa,ikiwa na lengo la kutoa fursa ya
kupata elimu kwa wananchi wote bila ya kujali matabaka,rangi au ukabila pamoja
la kutoa fursa kwa watoto wa wakwezi na wakulima kupata elimu ambapo kabla ya
mapinduzi ya 64 walibaguliwa katika kupata elimu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni