Habari

Jumanne, 11 Novemba 2014

Ukosefu wa usimamizi makini wa shughuli za serikali katika ngazi ya mikoa na wilaya ni miongoni mwa matatizo yanayorejesha nyuma utoaji wa huduma kwa wananchi


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema ukosefu wa usimamizi makini wa shughuli za serikali katika ngazi ya mikoa na wilaya ni miongoni mwa matatizo yanayorejesha nyuma utoaji wa huduma kwa wananchi.

Dk. Shein amesema hayo leo wakati akifungua Warsha ya Siku Tatu kuhusu Mahusiano na Mwingiliano kati ya Siasa na Utendaji kwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Makatibu Tawala wa Mikoa ya Zanzibar na baadhi ya Tanzania Bara uliofanyika hapa Zanzibar.
Amewataka viongozi hao kuchukua hatua za kukabiliana na hali hiyo ili Serikali ifikie malengo yake kama yalivyoainishwa katika mipango mbali mbali ya maendeleo na Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala.
Hata hivyo amewataka kuhakikisha kuwa fedha zinazopelekwa katika mikoa, wilaya na halmashauri zinatumika kulingana na matumizi yaliyopangwa na kusimamia ukusanyaji wa mapato ili kuongeza mapato ya serikali.
Mapema Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph Semboja amesema lengo la warsha hiyo ni kutoa fursa kwa washiriki kubadilishana uzoefu na kujifunza mbinu mpya kuongeza maarifa katika kutekeleza majukumu yao .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni