Baadhi wa askari wa jeshi la kujenga uchumi Zanzabar(JKU) wakimsikiliza Mkuu wa jeshi hilo alipokuwa akizungumza na wapambanaji hao huko katika Ofisi za JKU zilizopo Wawi Cake Chake Pemba.
Mkuu wa jeshi la kujenga uchumi Zanzibae(JKU) akisalimiana na askari wa jeshi hilo alipofika 0fisi kuu ya JKU zilizopo Wawi Chake ChakePemba.
Mkuu
wa jeshi la kujenga uchumi Zanzibar (JKU) Kanal Soudi Haji Khatib amewataka maafisa na wapiganaji wa jeshi hilo kisiwani
Pemba kudumisha nidhamu wakati wote ili kuondokana na matatizo ambayo yanaweza
kuzuilika wakati wanapokuwa ndani na nje ya kazi.
Akizungumza na Maafisa na wapiganaji hao huko katika Ofisi
kuu za JKU Wawi Chake Chake Kanal Soud amesema
nidhamu ndio njia pekee itakayowaweka askari hao katika kulitumikia kwa ari
jeshi hilo na taifa kwa ujumla.
Aidha amewataka Askari hao kuacha tabia ya kupikiana majungu
na kujiepusha na kufanya mambo yasiyoendana na taratibu za kijeshi kiasi
ambacho yanaweza kuwaingiza katika matatizo makubwa.
Amewahimiza wajenga uchumi hao kuzidisha bidii katika
uzalishaji mali ili kuliongezea kipato Taifa na wananchi wake.
Mapema mkuu wa Idara ya Mipango wa jeshi hilo Luteni Kanal
Ali Hassan Hamadi amewataka Maafisa na wapiganaji hao kuwa na tabia ya kubuni
miradi ambayo itakayoweza kulisaidia jeshi hilo.
Amesema jeshi la kujenga uchumi lina jukumu kubwa la
uzalishaji hivyo bila ya kuwa na ubunifu wa kweli litaendelea kutumia njia
zilizopitwa na wakati na kuzidi kuporomoka katika uzalishaji.
Hata hivyo Hassan amewaomba askari wa JKU kujiepusha na matumizi
mabaya ya mitandao ya simu,computer na mitandao ya kijamii kwani kuitumia
vibaya inaweza kuwa chanzo cha kujiingiza matatizoni.
mwisho
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni