Taarifa kutoka Dodoma zinaarifu kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME (SACP) amewataka wamiliki wa Hotel na Nyumba za kulala wageni (Guest House) kuhakikisha kwamba wageni wanaotarajia kuingia mkoani humo haswa wajumbe wa bunge la Katiba linalotarajia kuanza tarehe 18/02/2014 kuwahakikisha usalama wao katika kipindi hiki.
Kamanda huyo ameyasema hayo wakati akizungumza na wafanyabiashara ambao ni wamiliki wa Hotel na Nyumba za kulala wageni Mkoani humo na kusisitiza kubandika namba za viongozi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma ili kuweza kutoa taarifa za kihalifu pamoja na kupata huduma haraka ya kipolisi.
Pia Kamanda MISIME amesema kulingana na kukua kwa sayansi na teknolojia amewashauri wamiliki wa nyumba hizo kwa baadaye waboreshe huduma zao kwa kufunga CCTV – Camera kwenye korido, kaunta na nje ya Hotel na nyumba zao ili kuweza kurekodi na kutunza kumbukumbu za matukio katika maeneo yao ya biashara.
Na kuuongeza kuwa wahudumu wa nyumba hizo pamoja na Hotel wanatakiwa kuwa makini kwani katika kipindi hiki ndipo matapeli na wezi huwa wakiongezeka kwa kasi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni