ZANZIBAR.
Jaji Mkuu wa
Tanzania Mohammed Othman Chande amesema endapo serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itatunga
sheria za kuwatambua wasaidizi wa sheria kutaimarisha uelewa wa haki na sheria
kwa jamii.
Jaji Chande
ameyasema hayo huko katika Ukumbi wa Mikutano wa Eackrotanal katika mahafali ya
pili ya wahitimu wasaidizi wa sheria Zanzibar.
Amesema
kuwepo kwa sheria inayowatambua kutawawezesha wasaidizi hao wa sheria kufanya
kazi bila ya woga na kujiamini wakati wote wa utekelezaji.
Aidha Jaji
Mkuu huyo wa Tanzania amewataka wasaidizi wa sheria Zanzibar kufanya kazi kwa
mujibu wa maadili yao yanavyoelekeza kwa lengo la kuisaidia jamii kujua wajibu
wao wa kufualilia haki zao kwa mujibu wa sheria.
Kwa upande
wake Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu amesema kuwepo kwa wasaidizi wa
sheria kumeweza kuisaidia mahakama kupunguza mrundikano wa kesi mahakamani.
Amesema
majukumu waliyonayo wasaidizi wa sheria ya kutoa elimu kwa jamii juu ya kujua
misingi ya sheria na kufuatilia haki zao katika vyombo vya sheria ni
muhimu,hivyo hawana budi kuendana na maadili ya kisheria.
Jumla ya
wahitimu 65 waliohitimu mafunzo ya miaka miwili ya usaidizi wa sheria kupitia
Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar,wamekabidhiwa vyeti vya uhitimu, ambapo
kati ya hao 42 ni kutoka Unguja na 23 kutoka Kisiwani Pemba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni