Habari

Ijumaa, 11 Aprili 2014

Waziri adaiwa kumshambulia ofisa usalama uwanja wa ndege

Waziri wa Fedha wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Omar Yussuf Mzee, amefunguliwa mashtaka polisi akituhumiwa kumshambulia Afisa Usalama wa Uwanja wa Ndege wa Zanzibar, Maulid Shabani, kwa kumkwida na kumtupa chini kisha kumkandamiza kwenye dimbwi la majitaka baada ya ‘kummwagia’ matusi ya nguoni.

Mzee, ambaye amewahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, na Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nyakati tofauti, anadaiwa kufanya shambulizi hilo kwa kushirikiana na dereva wake.

Kutokana na tukio hilo, afisa huyo amefungua jalada namba RB/183/2014 katika kituo cha polisi cha uwanja huo, akilalamika kushambuliwa na Waziri Mzee kwa kushirikiana na dereva wake.

Mbali na kufungua jalada hilo, polisi walimpa hati maalumu ya polisi ya matibabu, maarufu kama “PF3” namba EZB/26153 na kwenda kutibiwa katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja, mjini Unguja.

Habari zilizolifikia NIPASHE jijini Dar es Salaam kutoka Zanzibar zinadai kuwa Waziri Mzee alifanya kitendo hicho juzi saa 2.40 asubuhi, akipinga gari lake kuzuiwa kutoka katika uwanja huo.

Inadaiwa gari hilo aina ya Prado lilizuiwa ili maofisa usalama wamueleze namna yeye na dereva wake walivyokiuka taratibu za uwanja huo kwa kushuka katika eneo, ambalo kiusalama haliruhusiwi mtu yeyote kushuka wala kushusha mzigo.

Maulid (45) aliliambia NIPASHE kuwa baada ya kufika uwanjani hapo, aliteremka kutoka kwenye gari lake katika eneo, ambalo haliriuhusiwi mtu yeyote kutelemka.

Alisema baada ya kuteremka, Waziri Mzee alikwenda kwenye ofisi za Shirika la Ndege la Precisionair kutafuta nafasi ya ndege, ambayo ilitarajiwa kuondoka jana mchana kwenda jijini Dar es Salaam na kuliacha gari lake likiwa limeegeshwa na dereva wake katika eneo, ambalo pia haliruhusiwi.

“Nilimfuata dereva wake nikampa maelekezo, lakini akaniambia ameambiwa na waziri amshushe eneo hilo. Nikamwambia waziri akirudi amfahamishe hilo, lakini waziri aliporudi, akaondoka naye,” alisema.

Alisema alipoona hivyo, aliwasiliana na maofisa wenzake walioko kwenye geti la kutokea kwa simu ya upepo, ambao walilizuia gari hilo kutoka.Waziri adaiwa kumshambulia ofisa usalama uwanja wa ndege

Alisema alipoona hivyo, aliwasiliana na maofisa wenzake walioko kwenye geti la kutokea kwa simu ya upepo, ambao walilizuia gari hilo kutoka.

Maulid alisema baada ya mawasiliano hayo alikwenda kwenye geti hilo na kukuta waziri huyo akilumbana na maofisa hao.

Alisema aliingilia kati kutaka amueleze waziri taratibu za uwanja huo, lakini yeye na dereva wake wakaanza kumtukana, huku wakimwamuru aondoke eneo hilo.

Maulid alisema kwa vile walishindwa hawakutaka kumsikiliza, aliamua kufunga geti hilo.

“Mheshimiwa waziri akashuka kutoka kwenye gari lake na kunikamata na kunitupa chini na kumkandamiza kwenye dimbwi la maji. Nikaripoti ofisini kwangu.

Nilipewa mtu wa kunipeleka polisi nikaandika maelezo. Baadaye, nikaenda kutibiwa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja. 

Alipoulizwa na NIPASHE jana, Waziri Mzee alithibitisha kutokea tukio hilo, lakini akakana kuhusika.

“Ugomvi huo ni wake yeye (afisa usalama) na dereva. Yeye alianza kumtolea maneno dereva. (Ugomvi huo) Siyo wangu mimi, anatumia jina langu, anataka kuuza story (habari),” alisema Waziri Mzee.

Alipotakiwa kueleza hatua alizochukua baada ya kuzuka tukio hilo, Waziri Mzee alisema: “Nilimwambia dereva tuondoke zetu.”

Chanzo:http://www.ippmedia.com/

You might also like:

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni