Habari

Jumamosi, 31 Januari 2026

BINAADAMU NA MCHANGO WA MABADILIKO YA TABIANCHI.


Na,TIME KHAMIS PEMBA.
  Binaadamu wana mchango mkubwa katika mabadiliko ya tabianchi, hasa kupitia shughuli zao za kila siku. Mabadiliko ya tabianchi yanamaanisha mabadiliko ya muda mrefu katika hali ya hewa kama ongezeko la joto duniani, mabadiliko ya mvua, na matukio ya hali ya hewa ikiwemo jua kali. 
Jinsi binaadamu wanavyochangia Matumizi ya nishati ya mafutakuchoma makaa ya mawe, mafuta ya petroli na gesi asilia (kwa usafiri, viwanda, na umeme) hutoa gesi chafuzi kama  kobondiaxyde  (CO₂) ambazo zinaongeza joto duniani. 
Ukataji wa misitu unofanywa na Binaadamu huchangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko hayo kwani kuwepo kwa misitu husaidia kunyonya CO₂, na  inapokatwa, uwezo huo hupungua na gesi chafu  huongezeka. Kwenye shughuli za Kilimo na ufugaji baadhi ya mbinu za kilimo na ufugaji hutoa gesi kama methani (CH₄), hasa kutoka kwa mifugo ambayo nayo huchangia kupatikana na mabadiliko tabia nchi kama gesi hiyo haikuwa na udhibiti. Aidha Uzalishaji wa taka taka  ovyo zikioza bila kudhibitiwa hutoa gesi chafuzi na Athari za mabadiliko ya tabianchi huongezeka kwa joto na ukame ,mafuriko na mvua zisizotabirika,kupungua kwa uzalishaji wa chakula,Athari kwa afya ya binadamu na viumbe hai               SULUHISHO NA HATUA ZA KUCHUKUA Kutumia nishati mbadala (jua, upepo, maji),kupanda miti na kulinda misitu, kuboresha mbinu za kilimo endelevu,kupunguza taka na kusindika upya (recycling),kuelimisha jamii na kuhimiza sera rafiki kwa mazingira kwa kifupi, binaadamu ni sehemu ya tatizo lakini pia wanaweza kuwa sehemu ya suluhisho kwa kuchukua hatua zinazolinda mazingira.       
   MOJA YA MBINU ZA KUZUWIA ATHARI HIYO Mradi ZanADAPT
 ni mpango wa utekelezaji unaolenga kusaidia jamii za Zanzibar kupambana na athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa njia ya kujenga ustahimilivu wa mazingira, kijamii na kiuchumi, hasa kwa wanawake na familia zao.                
       MRADI  HUO  UNAVYOSAIDIA: 
 Kujenga ustahimilivu wa mazingira kupitia njia za asili na za mitaaMradi unatumia mbinu za nature-based adaptation (urejesho wa mazingira), kama vile: Kulinda na kurejesha misitu ya mikoko, ambayo husaidia kupunguza athari za hali ya hewa kama mafuriko, kuzuia ukame, na kuhifadhi vyanzo vya uhai pwani.  
Misitu ya mikoko pia huingiza gesi chafu kama dioksidi ya kaboni, hivyo kuchangia kupunguza mabadiliko ya tabia nchi.  Kilimo mseto na kilimo chenye ustahimilivu wa hali ya hewa, ambacho hutoa chakula na kipato kwa wakazi huku kinapambana na athari za mabadiliko ya tabia nchi. 
 Kuendeleza mazao na mbinu za kilimo rafiki kwa mazingira ili kuimarisha ardhi na kuongeza ustawi wa ardhi kwa wakati wa mvua nyingi au ukame.        
  MBINU NYENGINE ZINAZOTUMIWA NA MRADI.  
  Uwezeshaji wa wanawake na utekelezaji wa kijamii ,moja ya malengo makuu ya mradi ni kuongeza ushiriki na uongozi wanawake katika shughuli za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, Kuwawezesha wanawake kupata ujuzi na nafasi za uongozi kwenye juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na usimamizi wa rasilimali. 
 Kuunda vikundi vya wanawake wanaojifunza na kushirikiana kuhusu mbinu za kilimo, uhifadhi wa misitu, na maamuzi ya utunzaji wa ardhi.  
Kupitia mradi, wanawake wengi wameweza kushika nafasi za uongozi ndani ya vikundi vya wakulima na utekelezaji wa shughuli za mazingira.   Kujenga uwezo na elimu kuhusu mabadiliko ya tabia nchiZanADAPT inajenga uwezo kwa kutowa mafunzo kwa wadau. Mafunzo na uhamasishaji wa wakazi kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, jinsi ya kuyakabili, na umuhimu wa kutunza mazingira kwa ustawi wa maisha yao.  Kupitia vikundi vya wakulima, wadau hupata ujuzi wa mbinu rafiki za kilimo na usimamizi wa maliasili.  
Mradi pia unalenga kuboresha ufahamu wa kijamii juu ya usawa wa kijinsia na nafasi za wanawake katika juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.            USHAHIDI WA HILO  MRADI 
wa usawa wa kijinsia, utunzaji wa mazingira na ustawi wa kijamii na kiuchumi ‘Zanz Adapt’ umewapa mafunzo ya ujasiriamali wa kusarifu bidhaa mashambani wanawake wa shehia zilizofikiwa na mradi huo. Shehia hizo ni  Chwale, Kiuyu, Mchangamdogo na Kambini Wilaya ya Wete ambapo mafunzo yaliyotolewa ni pamoja na upikaji wa sambaro la embe, chai masala, utengenezaji wa makwaru ya ndizi na pilau masala ambazo zinatokana na mazao yanayolimwa kupitia kilimo msitu. 
Anazungumza na Mwandishi wa Makala hii Afisa kilimo msitu  na usawa wa kijinsia  kutoka taasisi ya CFP Sada Juma Segeja amesema hatua hiyo ni miongoni mwa kuwawezesha wanawake wa vijijini  kufikia fursa mbalimbali za kiuchumi na kujipatia kipato. Analifahamisha lengo la kufanya mafunzo hayo  ni kuongeza thamani  ya zao la ndizi, maembe kwa kufanya achari, viungo (spices) ambayo ni katika mazao yanayolimwa katika kilimo msitu  na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.“Katika kufanya harakati hizi za ujasiriamali zitasaidia kukata miti ya mikandaa kwa shughuli za kujipatia kipato, yanayochangia maji kupanda juu , kuuwa mazalio ya samaki na kukosekana kwa mvua na kusababisha mabadiliko ya tabia nchi”alisema.
JEE NAO WASHIRIKI WA MAFUNZO WANASEMAJE
Washiriki wa mafunzo hayo Maryam Mbarouk  Khamis na Subeha  Suleiman Sultan walisema mafunzo hayo yatawakomboa  kiuchumi na kimaisha huk  wakivitaka vyombo vya habari kuhakikisha wanazisemea changamoto zao zinazorejesha nyuma maendeleo ya maisha yao. Mafunzo hayo ya usarifu wa mazao ni miongoni mwa utekelezaji wa mradi wa usawa wa kijinsia, utunzaji wa mazingira na ustawi wa kijamii na kiuchumi Zanz Adapt unaotekelezwa Chama cha waandishi wa habari TAMWA, wanawake Zanzibar CFI na jumuiya ya misitu  ya jamii Pemba CFP kwa ufadhili wa serikali ya Canada.     
MATOKEO YA MRADI HADI SASA 
Kwa mfano, matokeo yaliyorekodiwa (kabla ya 2025) ni pamoja na Kuunga mkono wanawake wasiopunguwa  14000  (hasa wanawake) katika kufanya kazi za kulinda mikoko, kuanzisha kilimo cha mseto, na usimamizi endelevu wa ardhi.  Kuunda vikwazo vya mafunzo vya wakulima kwa mazoea ya hali ya hewa,kushiriki wanawake zaidi katika maamuzi ya kijamii na mazingira ndani ya jamii .
Mradi ZanADAPT unasaidia kupambana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kuhifadhi na kurejesha misitu ya mikoko kwa ustawi wa mazingira, kuendeleza kilimo chenye ustahimilivu wa hali ya hewa.    Kukuza ujuzi na uwezo wa jamii kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi, kuinua wanawake kiuchumi na kijamii katika juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.             
         MKUFUNZI KUTOKA MRADI WA ZAN ADAPT .
 Ofisa kutoka mradi wa ZanAdapt Meiya  Mbarouk Mussa alisema endapo wanawake   watajishughulisha na ujasiriamali wataweza kujikomboa katika hali duni na kuweza kuongeza kipato kitakachowakimu katika maisha yao.“Niwaombe munapotayarisha bidhaa zenu kufuata sheria ikiwemo ya usafi binafsi na eneo husika, usalama na uhakika wa munachokizalisha kufanya hivyo mutapata mafanikio na mutajiwezesha zaidi”, alisema.Aidha kwa vile Binaadamu mwenyewe ameshafahamu juu ya uharibifu anaofanya unavyomuathiri kimazingira wameanza kuchukuwa juhudi ya kuhifadhi mazingira kwa kukabiliana na tabia nchi .Kikundi cha Uhifadhi wa Mazingira katika kiji cha Shengejuu mkoa wa Kaskazini Pemba kimeamuwa kupanda miti ya mikoko ipatayo elfu kumi kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko tabia nchi.             
    JAMII NA TAASISI ZA KIMAZINGIRA.
Katibu wa kikundi hicho Hamad Omar Salim akizungumza na Makala hii anasema wameamuwa kufanya hivyo baada ya kuona mashamba ambayo walikuwa wanayatumia kwa kilimo cha Mpunga huko katika eneo la Ambasha Shengejuu kuvamiwa na maji ya Chumvi na hivyo kuwakosesha wananchi kupata eneo la Kilimo.‘’ Mwanzo eneo hili wazazi wetu walilitumia kwa kilimo lakini baada ya wanaadamu wenyewe kuliathiri kwa kukata miti , ya mikoko na majani mengine makubwa yaliokuwa yanahifadhi maji yasipande juu tumekuwa na athari kubwa sana’’, anasema.Katibu wa jumuiya ya uhifadhi wa mazingira ( JIKEUMA) Kisiwa panza wilaya ya Mkoani Pemba Juma Ali Mati wakati anazungumza na mwandishi wa Makala hii anasema ene la Kisiwa panza limeathirika sana na mabadiliko tabia nchi kutokana na matumizi mabaya yanayofanywa na binaadamu mwenyewe ikiwemo kukata mikoko na kuchukuwa mchanga sambamba na Sunami iliathiri maeneo mengi ya Kisiwa cha Pemba. Anaeleza kuwa kutokana na athari hizo za mabadiliko tabia nchi jumla ya familia 100 zimekosa sehemu za kilimo na hivyo walitumia shilingi milion 500 ambazo walipatiwa kupitia mfuko wa kusaidia nchi maskini.Hata hivyo anasema fedha hizo zilitumika kwa kupunguza uharibifu wa maeneo yalioathiriwa na mabadiliko tabia nchi lakini sio kuondosha tatizo hilo , hivyo Binaadamu anawajibu wa kuhakikisha anapambana kwa kila hali ili kudhibiti mabadiliko hayo.                             MWISHO.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni