Habari

Jumamosi, 14 Desemba 2013

Kongamano la Maimamu wa Misikiti ya Zanzibar


Shekh.Shamimu mweye koti akitowa Mada katika Kongamano hilo inayohusiana na Uislam ni Dini ya kati na kati naUadilifu, katika kongamano la Maimamu kuhusiana na Njia Mpya za Kulingania Uislam Zinazoendana na Hali Halisi katika Jamii, lililofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Utamaduni Rahaleo. 
                      Shekh. Shamim, akisisitiza jambo wakati akiwasilisha Mada yake katika Kongamano                                                                        hilo.



Mtoa Mada Shekh Suweid Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha SUZA,akitowa Mada kuhusiana na Mchango wa Maimamu katika Jumuiya ya Kiislam.Kongamano Hhilo likizungumzia Njia Mpya za Kulingania Uislamu Zinazoendana na Hali Halisi katika Jamii, limeandaliwa na Jumuiya ya Kulingania Uislam Duniani   (LIBYA)

               Maimamu wakifuatilia madaczinazowasilishwa na wahusika katika Kongamano hilo

Muuongozaji wa Kongamano la Maimamu Zanzibar Shekh. Shaban Jongoo, akisoma dua baada ya kumalizika kwa Mada ya siku ya kwanza zilizotolewa na Mashekh. Shamimu na Dkt Seweid, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha SUZA.
Baadhi ya Maimamu  wa Miskiti ya Zanzibar wakiitikia dua baada ya kumaliza kwa kongamano hilo la siku tatu lililowashirikisha Maimamu wa Miskiti ya Unguja. Limeandaliwa na Jumuiya ya Kulingania Uislam Duniani, kongamano hilo limafanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Utamaduni Jengo la zamani la Redio Rahaleo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni