JEE ! WAJUWA KABLA Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964, elimu ya maandalizi ndani ya visiwa vya unguja na Pemba haikuwa rasmi, na nathubutu kusema haikuwepo kabisa ! hukukatika maeneo iliyokuwepo ilitolewa kwa upendeleo wa kijamii na kikabila, na watoto wengi wa tabaka la chini watoto wa mskini, wakwezi na wakulima hawakupata nafasi ya kujiunga na skuli za maandalizi ,huku Elimu ikibaki kuwa ya kikundi kidogo cha watotokutoka familia za wenye uwezo na si haki ya kila mtoto.Yote hayo sababu kubwa ilikuwa Mfumo wa elimu ulikuwa ni wa kikoloni na wakisultani, ukilenga zaidi watoto wa tabaka la juu mijini, huku vijijini kukikosekana kabisa huduma za elimu ya awali ambayo kwa sasa inatambulika kama elimu ya maandalizi .HISTORIA YA ELIMU YA MAANDALIZI ZANZIBAR KABLA YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR YA MWAKA 64 UPATIKANAJI WA ELIMUElimu ya maandalizi haikuwa sehemu ya sera ya serikali ya kisultani. Hakukuwa na mtandao wa skuli za serikali kwa watoto wote; badala yake skuli nyingi zilikuwa za binafsi na nyentine zikiwa kidini.Elimu ya awali haikujulikana kwa kiwango cha kitaifa, bali ilikuwa ni ya kikundi kidogo cha watu wenye uwezo na maeneo yaliyokuwa rafiki kufikika maeneo ya unguja mjiniWatoto wachache wa tabaka la juu, hasa wa asili ya Kiarabu na kiswahili wa mjini, ndio waliopata nafasi ya kujiunga na skuli za awali,huku Vijijini, watoto walitegemea madrasa na elimu ya dini kama njia pekee ya skuli za maandaliz katika kujifunza .Mfumo wa elimu ulikuwa wa kikoloni na kisultani, ukilenga zaidi watoto wa tabaka la juu.Skuli chache zilikuwepo, nyingi zikiwa mijini na hazikuwafikia watoto wa vijijini.Elimu ya maandalizi haikuwa rasmi, watoto wengi walijifunza kupitia madrasa au elimu ya jadi.Uwiano wa walimu kwa wanafunzi ulikuwa duni, walimu wachache na wengi wakiwa wageni.Huduma za kijamii skulini hazikuwepo, hakuna lishe shuleni wala ruzuku kwa wanafunzi.Uandikishaji ulikuwa mdogo sana, idadi kubwa ya watoto wa Zanzibar hawakupata nafasi ya kusoma elimu ya maandalizi . Walimu wachache walikuwepo, wengi wakiwa wageni au wa tabaka la juu.Idadi ya watoto waliopata elimu ya maandalizi ilikuwa ndogo sana, ikilinganishwa na idadi ya watoto wa Zanzibar.Hakukuwa na mafunzo maalum ya ualimu wa maandalizi; walimu walitegemea uzoefu wa madrasa au elimu ya msingi ya kikoloniELIMU BAADA YA MAPINDUZI 1964– ILIPOFIKIA MIAKA 62 MWAKA HUU 2026)Kuna mageuzi makubwa mabadiliko na maendeleo ya elimu yamefikiwa miongoni mwa hayo ni pamoja na Elimu sasakuwa haki ya kila mtoto,kwa lazima bila ubaguzi wa kijamii,dini siasa wala uchumi . Kabla ya Mapinduzi ya mwaka 1964, elimu ya maandalizi Zanzibar haikuwa rasmi, haikuwa jumuishi, na iliwafikia wachache tu wa tabaka la juu mijini. Mapinduzi ya Zanzibar yalibadilisha hali hii kwa kuifanya elimu kuwa haki ya kila mtoto bila ubaguzi, na kuanzisha mtandao wa shule za maandalizi na msingi unaofadhiliwa na serikali. Skuli zimeongezeka kwa kasi ndani ya miaka 62 ya Mapinduzi ya mwaka 1964 Kwa sasa kuna zaidi ya 262 za maandalizi zinazopata ruzuku ya Serikalikatka kutoa huduma bora kwa wananchi za serikali na binafsi ..Ndani ya miaka 62 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar kuna Ukarabati na ujenzi mpya: Skuli 97 za maandalizi zinazojumuisha na a msingi zinaendelea kukarabatiwa, na ujenzi wa shule mpya 36 (21 za maandalizi, 15 za msingi)ukiendelea katika maeneo mbali mbali Unguja na Pemba.Ongezeko la Walimu wapya,889 wamepangiwa kazi mwaka 2025/26 pekee, wakisaidia kupunguza uwiano wa walimu kwa wanafunzi jambo ambalo kabla ya miaka 62 ya mapinduzi ya ya 1964 hayakuwepo .Kuna ongezeko la Uandikishaji wa Wanafunzi , Wanafunzi 105,101 sawa na asilimia (82.5%) wameandikishwa katika skuli maandalizi maeneo yote Unguja na Pemba hadi kufikia miaka 62 ya mapinduzi matukufu ya Zanzibar yalioasisiwa na Hayat mzee Abeid Aman Karume .Ambapo huduma za lishe Maskulini kabla ya miaka ya Miaka 62 ya Mapinduzi ya Mwaka 1964 hazikuwepo kabisa lakini kwa ndani ya miaka 62 ya Mapinduzi hayo Matukufu huduma za lishe zimeongezeka na kufikia asilimia 50 na wanafunzi wapatao 63,099 .hupata lishe bora kupitia ruzuku ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Sekta ya elimu ya maandalizi na msingi Zanzibar imepiga hatua kubwa baada ya Mapinduzi ya mwaka 1964, ikilinganishwa na hali ya elimu kabla ya Mapinduzi. Leo, miaka 62 ya Mapinduzi hayo hku idadi ya mageuzi na mabadiliko katika upatikanaji wa Haki hiyo zikionesha kuongezeka kupatikana huduma bora za elimu ya maandalizi kwa uandikashaji wa wanafunzi bila ubaguzi wa aina yeyote, Lishe, elimu bora, waalimu , majengo bora ya kupata elimu Mapinduzi yam waka 1964 hadi kufika kilele cha miaka 62 mwaka huu 2026 january 12 kumekuwa na mageuzi makubwa katika elimu ya maandalizi na msingi kutoka mfumo wa kikiloni uliokuwa wa kibaguzi na wenye upatikanaji mdogo wa utoaji elimu ufinyu wa maeneo ,lishe ,uwandikishaji duni na matabaka wa waalimu wachache mitaala isyorasmi hadi sasa kuwa kasi ya mageuzi kutoka kadhia hizo na kuwa Zanzibar ya miaka 62 ya mapinduzi yenye mfumo mjumuishi wa elimu ,takwimu thabiti za uandikishaji zenye kuangalia hali za wananchi,waalimu bora, miundombinu bora huduma za kijamii skulini yote hayo ni mafanikio ya miaka 62 y MapinduizI ya Zanzibar katika kuinua maisha ya wananchi kupitia elimu bora ambayo ndio ufunguo wa mafanikio ya taifa na mtu mmoja mmoja baadae
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni