Habari

Alhamisi, 20 Novemba 2014

Zoezi la utoaji fomu za Zan ID Pemba



 
: MWAKILISHI wa Jimbo la Ole wilaya ya Wete Pemba Mhe: Massoud Hamad Massoud, akizungumza na vijana wa Jimbo lake juu ya umuhimu wa kupatiwa kitambulisho cha ukaazi cha Zanzibar, wakati mwakilishi huyo alipokuwa na ziara ya kutembelea zoezi la utoaji wa fomu hizo kwa msheha(picha na Haji Nassor, Pemba)

 
KULIA ni Mwakilishi wa Jimbo la Ole Mhe: Hamad Massoud Hamad akisalimiana na sheha wa shehia ya Ole Mussa Ali Kombo, wakati mwakilishi huyo alipofanya ziara maalumu ya kuangalia zoezi la ugawaji wa fomu za kuombea kitambulisho cha ukaazi kwenye Jimbo lake (picha na Haji Nassor, Pemba)

 
WAKATI baadhi ya masheha wa Jimbo la Ole wakidaiwa kukataa kutoa fomu za kuombea kitambulisho cha ZANID, sheha wa shehia ya Ole Mussa Ali Kombo, amekuwa akigawa fomu hizo kwa wananchi wa shehia yake, kama alivyokutwa na mpiga picha wetu shehiani humo (picha na Haji Nassor, Pemba)

 
KULIA ni mwakilishi wa Jimbo la Ole Mhe: Hamad Massoud Hamad akimuonyesha vyeti vya kuzaliwa sheha wa shehia Mjini Ole Khamis Shaaban vya wananchi wa shehia wa shehia hiyo, baada ya sheha huyo kudai hakuna mwananchi mwenye cheti aliekosa fomu za kuombea kitambulisho za ZANID, wakati mwakilishi huyo alipotembelea zoezi la ugawaji wa fomu hizo jimboni mwake (picha na Haji Nassor, Pemba)

 
WANANCHI wa shehia ya Kigongoni Jimbo la Ole, wakiwa wamesimama kwenye ofisi ya sheha wao majira ya saa 11: 50 jioni wakimsubiri sheha wao Juma Haji Omar, ili kuwapatia fomu za kuombea kitambulisho cha ZANID, ambapo baadhi ya masheha jiomboni wamepanga kila Ijumaa ndio siku ya kutoa fomu hizo (picha na Haji Nassor, Pemba)

 MWAKILISHI wa Jimbo la Ole Mhe: Hamad Massoud Hamad akizungumza na waandishi wa habari kwenye shahia ya Minungwini Jimboni humo, mara baada ya kumaliza ziara ya kuangalia zoezi la utaoji wa fomu za kuombea kitambulisho cha ukaazi ZANID (picha na Haji Nassor, Pemba)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni