Habari

Jumatatu, 30 Septemba 2013

Kizi na Chipukizi hawachekani wote wapigwa mbili katika ligi kuu ya Grand Malt Zanzibar.

IMG_6082

Timu ya Kizimbani imeshindwa kutamba katika ligi kuu ya Zanzibar"Zanzibar Grand Malt Premier Legue" baada ya kukubali kupokea tena kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa mabaharia wa KMKM katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Gombani hapo jana.

Iliwachukua takriban dakika 7 tu tokea kuanza kwa mchezo huo kwa mabaharia wa KMKM kujibatia goli la kwanza lililofungwa na mshambuliaji wake Maulid Ibrahim Kapenta baada ya kazi kubwa iliyofanywa na kiungo Abdi Kassim (Baby) kwa kumpa pande safi.

Hata hivyo bao hilo halikuwavunja moyo Kizimbani ambayo imeonekana kufanya vibaya kila ikishuka dimbani,kwani walijipanga na kupeleka mashambulizi katika lango la wapinzani wao,lakini hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika KMKM walikuwa na goli 1 na Kizimbani 0.

Timu zote mbili zilikianza kipindi cha pili kwa kasi kwa kizimbani kutaka kusawazisha,huku kwa upande wa KMKM wakiimarisha katika safu ya ulinzi kulilinda bao hilo huku wakifanya mashambulizi ya kushtukiza kuweza kujipatia goli jengine.

Ikiwa baadhi ya mashabiki wameshaanza kutoka kiwanjani na kudhani matokeo yatabaki kuwa  ni 1-0, Abdi Kassim Baby aliwanyanyua mashabiki wa KMKM kwa kupachika goli la pili katika dakika ya 90 ya mchezo huo.

Na hadi mwisho wa mchezo huo Mabaharia wa KMKM 2 na Kizimbani 0.

Kwa matokeo hao KMKM wamefikisha point 13 la kukalia usukali wa ligi hiyo huku Kizimbani wakibakia la alama 4 baada ya kucheza michezo 7 ambapo ilishinda mmoja na kutoka sare mmoja.

Nayo timu ya Chipukizi pia kutoka kisiwani Pemba imeshindwa kutamba katika uwanja wa Mao baada ya jana kulala kwa mogoli 2-1 kutoka kwa Masarahange wa Malindi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni