Habari

Ijumaa, 11 Aprili 2014

Habari za Kimataifa

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limeishutumu Kenya kwa kuwatumia wasomali kama kisingizio katika msako wao wa kuwasaka washukiwa wa ugaidi,msako ambao umesababisaha kukamatwa kwa maelfu ya watu na wengine kurejeshwa Somalia. 
Afisa wa Human Rights Watch Gerry Simpson amesema hatua ya kuwanyanyasa wasomali kufuatia mashambulizi ya kigaidi ambayo yameikumba Kenya haitawakikishia wakenya,wasomali na watu wengine nchini humo usalama wao na kwamba hakutatokea mashambulizi zaidi.
Kundi hilo la kutetea haki za binadamu limesema kurejeshwa kwa wasomali nchini mwao bila ya kuwaruhusu kuwasilisha maombi ya hifadhi ni kukiuka haki zao.
Human Rights Watch limesema limezuru vituo vya polisi vya Pangani na Eastleigh na kujionea mamia ya waliokamatwa wakiwa wamejazana  katika vizuizi vinavyopaswa kuwazuai kiasi ya watu 20.Waziri wa usalama Joseph Ole Lenku amesema kiasi ya watu 4,000 wanazuiwa na 82 kati yao wamerejeshwa Somalia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni