Jeshi la polisi Mkoa wa Mjini Magharibi limeannzisha mradi
wa kuhamasiha kupunguza matokeo ya uhalifu katika familia na jamii.
Kamanda polisi mkoa
huo Mkadamu Khamis Mkadamu amesema lengo la mradi huo ni kuisaidia jamii kufahamu umuhimu wa
kuimarisha mifumo ya malezi bora ambayo ni njia pekee salama ya kuzuia ukuaji
wa uhalifu.
Amefahamisha kuwa mradi huo wa familia yetu hamna uhalifu
umezingatia kwa kuwa wengi wa wahalifu wenye umri mdogo familia zao
hazikuzingatia malezi bora pamoja na uslama watoto wao.
Akizungumzia kuhusu operesheni za kukamata wahalifu ameeleza
kuwa jumla watu kumi na saba wamefikisha mahakamani kwa makosa mbalimbali
ikiwemo utimiaji wa dawa za kulevya na kufanya biashara haramu ya pombe ya
kienyeji.
Kamanda Mkadamu ameongeza kuwa jeshi hilo linaendelea
kufanya operesheni ya pamoja na wananchi wa shehia mbalimbali kwa lengo la
kuimarisha hali ya usalama ndani ya mkoa wa mjini Magharibi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni