Habari

Jumatatu, 30 Septemba 2013

Watu 74 hawajulikani walipo baada ya boti 3 za uvuvi kuzama nchini China

Mamlaka za bahari zimethibitibisha kuwa jumla ya watu 74 hawajulikani walipo, baada ya boti tatu za uvuvi kuzama jumapili mchana kutokana na kimbuka, karibu na visiwa vya Xisha katika bahari ya kusini ya China.
Kwa mujibu wa habari, hadi leo mchana watu 14 walionusurika wameokolewa. Wakati huohuo serikali ya mji mpya wa Sansha imewahamasisha wakazi wa kisiwani pamoja na meli kushiriki katika juhudi za kutafuta na kuwaokoa waathirika. Lakini kwa mujibu wa kituo cha uokoaji kazi ya uokozi imekwama kutokana na upepo mwingi na mawimbi makali baharini.
Habari zaidi zinasema rais wa China Xi Jinping ametaka zifanyike juhudi zote za uokoaji. Katika maelekezo hayo maalumu rais Xi amezitaka mamlaka za huko kujitahidi kuwatafuta watu waliopotea na kupunguza idadi ya waathirika. Kwa upande wake waziri mkuu Li Keqiang pia ametoa wito kama huo na kuzitaka mamlaka kuhakikisha usalama wa watu wanaofanya kazi ya uokozi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni