Na Is-haka
Mohammed,Pemba. 23/09/2013 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali
Zanzibar Ali Juma Shamuhuna amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
itaendelea kukabiliana na changamoto mbali mbali zinazoikabili sekta elimu ili
kuimaeisha sekta hiyo nchini.
Amesema
serikali inatambua kuwepo kwa tatizo la uhaba wa walimu wa Sayansi na walimu
wengine katika skuli mbali mbali lakini Wizara imekuwa ikifanya juhudi kubwa
kulipatia ufumbuzi tatizo hilo.
Waziri
Shamhuna ameyasema hay oleo huko Gombani Chake Chake wakati akiwahutubia
wanafunzi,walimu wazazi na wananchi mbali mbalii katika kilele cha maadhimisho
yamiaka 49 kutokea kutangazwa kwa Elimu bila ya malipo Zanzibar.
Amesema katika
kulipatia ufumbuzi tatizo la walimu nchini serikali imeimarisha fursa ya nafasi
za wanafunzi watakaosomea ualimu wa fani zote katika vyuo vikuu vilivyopo
Zanzibar.
Aidha
amesema serikali inaendelea kuimarisha maslahi ya walimu nchini ili kuhakikisha
kuwa watapata maslahi mazuri na kuweza kufundisha kwa ustadi zaidi na kutoa
wanafunzi wazuri watakaokuja lisadia taifa hapo baadaye.
Kwa upande
mwengine Waziri huyo wa elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Juma Shamuhuna amesema tatizo la utoro
maskulini ni moja kati ya mambo yanayochangia kwa wanafunzi wengi kushindwa
kufanya vizuri katika mitihani yao ya taifa.
Amesema kuwa
utafiti uanaonyesha kuwa wimbi kubwa la wanafunzi wamekuwa wakikwepa kwenda
skuli,huku wengine wakishindwa kushughulikia masomo yao wawapo skuli au hata
majumbani .
Amewapongeza
walimu katika skuli mbali mbali kwa kujitolea kwa kusomesha kwa moyo mkunjufu licha ya kuwepo kwa changamoto
nyingi zinazowakabili.
Waziri huyo
amesema serikali inatambua changamoto zinazowakabili walimu hasa katika upande
wa maslahi yao,na kuwataka kuendelea kuvuta subira kwa vile muda mfupi ujao
wataanza kuona mabadiliko kwa upande wa maslahi yao.
Hata hivyo
amewataka walimu kuendelea na bidii katika kuwapatia elimu wanafunzi bila ya kuchoka huku serikali nayo ikiwa katika hatua za mwisho kurekebisha
maslahi ya walimu nchi kote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni